Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mliooa mnakwama wapi? maana kila baharia nayemkuta na mchepuko bar,nikimuuliza kwa nini anachepuka utasikia ooo!!! mke wangu mjamzito,ooo!!mke wangu amejifungua,ooo!! mara mke wangu yupo siku zake mwezini,ooo!! mara mke wangu ana kelele sana, nyumbani hapakaliki,utasikia mara ooo!! mke wangu ameenza kuzeeka ili siwezi kumwacha sababu nimetoka nae mbali, mabaharia mnafeli wapi????? mabaharia nini kinawashinda kwenye ndoa???
Mi sijui ni asili yangu!Ni siku nyingine tena imepita, tumerudi salama majumbani mwetu, kuungana tena na wapendwa wetu, familia na watoto pia... Baadhi yetu hatujarejea, tuko mishe na viti virefu... Baadhi tuna sababu za msingi na nyumbani wanafahamu na tumewapa taarifa, wanatusubiri watupokee kwa upendo, kwa furaha kwa bashasha kuu
Baadhi hali ni tofauti, hatungependa kuchelewa nyumbani.... Tungependa tuwahi, tuungane na familia, tuimalize jioni kwa furaha kuu kabla hatujaungana kwa dinner na maombi ya usiku.... Lakini hali ni tofauti tunapoteza muda nje saa zisogee ili tukifika tu ni chakula kuoga na kulala... Tunakimbia kero na malumbano yasiyoisha
Ndoa haina furaha.... Ndoa haina amani, majuto ni mengi mno moyoni.. Kila mmoja anajutia kivyake... Hakuna upendo tena... Hakuna kuaminiana tena... Ni mwendo wa kutuhumiana na kuviziana.... [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]baba ana chumba chake.. Mama naye ana chake... Ama la chumba ni kimoja lakini kila mmoja ana kitanda chake...
Hakuna upendo, hakuna sharing, hakuna majadiliano ya changamoto, ya maumivu ya kushinda na kushindwa, ya kutiana moyo na kufarijiana... Kila mtu kivyake... Kila mtu na lwake... [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji24][emoji17][emoji17][emoji17]
Karibuni wanandoa wote.. Ni mada ya kupeana faraja na kushare maumivu... Itambueni nguvu ya kuongea... Kuongea hupunguza maumivu mengi... Kupitia mada hii utajiona hauko pekeyako na pengine utaona kuwa kumbe wewe una nafuu kubwa ukisikia ya mwenzako. Jisikie huru ufunguke....
Funguka kwenye ndoa yako iliyoumizwa na kujeruhiwa sana, iliyotiwa vidonda na makovu ya kila aina
Ya usaliti
Ya kuchapiwa
Ya kusingiziwa
Ya kunenewa mabaya
Ya kudharauliwa kutukanwa na kudhalilishwa
Funguka upate nafuu
Funguka upate faraja
Funguka upunguze sumu mwilini
Funguka upate kupona sasa....
Karibuni wanandoa wote
Jr[emoji769]
Na kipindi hicho ndicho kusalitiana huwa ni rahisi sanakwa upande wangu naona ndoa ni uvumilivu, na kikweli ili muweze kudumu lazima mmoja ajishushe, ila mkiwa wote juu lazima hamta dumu na ndoa itashambaratika, kuna kipindi inatokea mnakuwa na migogoro, mnalala kitanda kimoja ila hata salamu akuna hichi nikipindi kibaya sana.
Yan hakuna sekta ngum km ndoa...!!sema reason kuu naamini ni uvumiliv kukosekana...ndoa n uvumiliv
Kingne mwanamke anaolewa na juma wakat moyoni kuna rama!!.....yan ingkuwa mtu uloanza nae ndo unaoana nae ndoa ingkuwa tam saana
Ila unaoana na mtu mwenye network kibao lazma ulie...!!ukizima umeme mwenzio anawasha jenereta
Kwanza nikupe hongera na pongezi nyingi kwa uvumilivu muda wote huo!1. Alikua anataka kunitawala yaani yeye awe juu mimi niwe chini yake, yaani mimi niwe kama mwanamke na yeye awe mwanaume
2. Tendo la ndoa mpaka atake yeye au ajisikie
3. Jeuri na kiburi vyote vyake ana majibu ya hovyo yaani anaweza kunijibu anavyotaka kama anamjibu mwanae
4. Alikua anatabia ya kunikorofisha makusudi nikichukia ananisema vibaya kwa majirani na ndugu zake mwisho mimi naonekana mbaya ( HII NDIYO SABABU KUU ILIYOPELEKEA NIMUACHE )
Yaani naweza kusema yeye alikua akifurahi kuniona mimi nikiwa matatizoni maana kama kuna mtu ananidai basi yeye atasimama kidete utadhani yeye ndo anayenidai
5. Mbishi...ukimwelekeza kitu kwa nia ya kumwelewesha ye hataki anajiona mjuaji kwa kila kitu
Yaani yeye akishasema kitu ndo kasema hivyo anachotaka ni utekelezaji tu(FINAL SAY )
6. Hataki kusemwa au kukosolewa pindi anapokosea ( kuna kipindi alikua akionea watoto wa dada yangu kumbe wale watoto mmoja ambaye ni mkubwa alikua akiwaambia wazazi wake Baba na Mama ila wao walikua hawamwambii kwa kuhofia ataonekana hapendwi ila siku mtoto akaja kushtaki kwangu nikamchana kwamba anachokifanya sio kitu kizuri....AKANUNA HUYOOO...akaona haitoshi akajitenga yeye na mtoto wetu wa kwanza akawa anamtenga asicheze na wenzie, kuona hivi nikamwita tena kisha nikamwambia tena mbele ya Dada, alichosema dada ni kwamba hizo taarifa ye aliambiwa muda tu ila alishindwa kuniambia mimi kwa kuhofia nitaona anamchukia wifi yake )
7. Mbinafsi...Changu chake....chake ni chake hata kama mimi ndo nilipambana au nilifanikisha mpaka akakipata ila ni mwiko kunishirikisha...( Kuna kipindi alikua akifanya biashara flani sijawahi kushirikishwa kuhusu mapato wala nini yaani akimaliza biashara hela inafichwa hukooo...ila mimi nikirudi kazini nikitoka tu akawa anasachi mifuko ya suruali zangu ajue kuna pesa kiasi gani akikuta pesa, kesho yake ataanza kuniambia anadaiwa nikimwambia sina hela atanijibu zipo kiasi fulani kwenye suruali yangu yaani hata kama tayari ipo kwenye bajeti ya kodi ya nyumba ye atataka itumike anavyotaka yeye mwisho wa siku naanza kuhangaika peke yangu ye ananiangalia tu )
8. Anaigiza....yaani yeye anaishi ili kuwafurahisha majirani au watu, yupo tayari kwenda kumsaidia kazi jirani huku zilizopo ndani hakuzimaliza kisha baadae anaanza kulalamika kuchoka nikimwambia ananijibu mimi MSHAMBA WA MAISHA
9. Ameharibiwa na vipindi vya kwenye runinga hasa hivi vya kina Mama Terry bila kusahau na Bongo Movie
10. Anapenda kujionyesha....yaani anataka kuonekana yeye yupo juu kwa lugha nyepesi hataki kuishi katika uhalisia anataka kuonekana anaishi maisha fulani hivi ya hadhi ya juu
N.B;
KIPINDI CHA UCHUMBA TABIA HIZI SIKUWAHI KUZIONA MAANA NILIANZA NAE MAHUSIANO 2014 HADI 2018 MWISHONI NDO TULIFUNGA NDOA
vipi jamaa anachepuka??,kipi kilikufanya umtilie mashaka huyo jamaa?
wanasema ukimuonesha upendo mwanamke anakuona fala!!
Duh! Sidhani kama kweliHapana mkuu,mwanamke akiwa sahihi kwako na akakupenda kweli hakika ukimuonyesha upendo ndo utafurahi zaidi maana atakuona kama nuhu kwake
Kuoa lazima mkuu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3],watu na ndoa zao shida tu,mimi sidhani kama nitaoa
Si kuna mtoto na mmejenga wote, hiyo anaishi tu hawezi kuuzaaisee,utamwachiaje nyumba mwanamke wewe??
Tatizo lipo hivi unaweza kuta mke hana shida yeyote ila sasa muoaji hasomeki mambo huanzia hapo, wanawake huvumilia madhira mengi kuliko wanaumeHapana mkuu,mwanamke akiwa sahihi kwako na akakupenda kweli hakika ukimuonyesha upendo ndo utafurahi zaidi maana atakuona kama nuhu kwake
Duh! Sidhani kama kweli
Hapana sio kweliNdiyo ukweli mkuu