Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Jamani natafuta corolla 110 iwe katika hali nzuri isiwe rangi nyeupe bajeti ml 3 mwenye nayo ani pm au 0754 065573

punda wa kazi huyo mkuu.Kila la kheri.Akikusumbua kupata huyo ongezea choice kwa kaka yake anaitwa "mtakatifu corolla sprinter se vintage limited" au ukihangaika sana kuna mwenzie "very cute" wa miaka ya 99/2000 anaitwa se vintage riviere.Injini ni zile zile kama 110 za 4e au 5a-fe.Unakuta kamechoka hadi kanatoa moshi nyuma na bado kanakunywa lita 1 kwa km 12,13!corolla ni bahili sana.Huyo E 100 ndio tobaa,gari inapoteza sifa zote za kuitwa gari na bado inatembea!Sprinter itakufa kila kitu hata juu ya mawe utaiweka lakini utakuta kiyoyozi bado kinagandisha!Yaani kama ni kabila,basi huu ukoo wa corolla una asili ya wapare!samahani sana braza Mshana sijakusudia kukukwaza.
 
Natafuta fundi mzuri wa Nissan X trail inasumbua Throtle sensor nimebadilisha sensor Ila bado inasumbua! Naomba kama kuna Mtu alikuwa na tatizo Hilo na alipata wapi fundi!

Gari ikipita kwenye rough road inazima zima na kuonyesha check engine.

Msaada kwenye tuta
 
Uko Dar?
 
Kuna ya kwetu nimeiendesha huu ni mwaka wa nne inawasha taa ya check engine lakini ipo njema sana dar arusha imezoea na haijawahi sumbua chochote mafundi ni waongo wanabuni tuu ila ngoja tuwasubiri humu
 
Swala sio Check engine gari inazima kabisa ingekuwa haizimi sio issue
 
Wakuu habari, naomba kuuliza jambo, hivi ukiagiza gari nje wakati Wa kulipia ushuru Wa TRA, Load licence inakuwa included or inalipiwa separately??
 
Wakuu habari, naomba kuuliza jambo, hivi ukiagiza gari nje wakati Wa kulipia ushuru Wa TRA, Load licence inakuwa included or inalipiwa separately??

Utalipa vyote papo hapo, assessment ya ushuru ikitoka itaonesha malipo yote unayotakiwa kufanya.
 
Kwangu Mimi, ukinambia pajero mini haitaki shida, nashangaa, Mimi ninayo, marafiki zangu wanaiita hardworker. Niliyonayo ni ya mwaka 1995, nasafiri nayo rough road na kwa hivi imeinuka kidogo, inadunda vizuri tu sana name safari zangu nyingi ni ndefu zaidi ya km elfu moja, name huwa sipumziki. Naipenda sana, sema kwa udogo wake, comfortability take so nzuri.
 
Wadau, mwenye uzoefu na Mazda tribute, uimara wake husasani rough road name safari ndefu, comfortability yake na fuel consumption.
 
Wadau gari bmw318i nimebadili oil seal ya gear box nikitembea mida onagoma kubadili gear inasimama. Kwenye dashboard inawaka taa ya alama hii ! Kuna Fundi ananiambia nifanye diagnosis. Naomba usaidizi wenu
 
Duu hiyo ni shida kubwa kwenye system fanya hiyo diagnosis utapata majibu yote
 
Wadau, mwenye uzoefu na Mazda tribute, uimara wake husasani rough road name safari ndefu, comfortability yake na fuel consumption.

Ni gari nzuri lakini zenye kuhitaji uangalizi wa Karibu
 
Niko arusha mkuu na no mgeni naomba wenyeji wanisaidie wapi naweza pata hii huduma na gharama zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…