mkuu unaposema mafuta Super unamaanisha nini? fafanua hapoNi kweli mkuu, D4 ni super engine, ila ukiweka mafuta 'super' unaua engine...mm hata kwa gari yangu VVT-i huwa siweki mafuta Super maana siyaamini nayaona km ubora wake uko chini sana#
Ila cku hizi naona kuna gari ni D4-VVT-i, hizi unaweza kuweka Mafuta yyt yake..mfano Toyota wish nyingi ni hizo!
Wakuu heshima kwenu.
Nina gx 110 ya mwaka 2001. Ukiwa kwenye speed zaidi ya 100 km/hr alafu ukakanyaga brake uskani unatetemeka. Speed inapopungua mpaka 80 km/hr usukani unatulia. Tatizo linaweza kuwa ni nini wakuu?
Kafanya wheel balance na alignment mkuu gari itakaa poa.
Wakuu nina Hillux 1995, ya petroli 1998cc niliagiza japan ikiwa na km 150,000. Bado iko katika hali nzuri sana, ila fuel consumption ni km 7.5 kwenye lami high way km 60 hadi 80 kwa saa, sijawasha a/c. Nimenda Bosch wakashauri nibadilishe fuel filter, badoo. Nifanyaje?
Fuata ushauri wao wako vizuri wale na kwa asilimia kubwa hawababaishi
Fuata ushauri wao wako vizuri wale na kwa asilimia kubwa hawababaishi
Wadau gari yangu Toyota Ipsum taa ya engine check imewaka ina mwezi sasa,nimepeleka kwa fundi amepima kwa kutumia computerised diagnostic system ameniambia ni oxygen sensor imekufa ila haina madhara kwenye engine.Kuna mwenye kujua chochote kuhusu hili!
Wadau gari yangu Toyota Ipsum taa ya engine check imewaka ina mwezi sasa,nimepeleka kwa fundi amepima kwa kutumia computerised diagnostic system ameniambia ni oxygen sensor imekufa ila haina madhara kwenye engine.Kuna mwenye kujua chochote kuhusu hili!
hahahaha mkuu kumbe na wewe bado unasujudia majina???
kwani Bosch ni wakinani hasa??
haya kwa utaalam wako wamemwambia abadilishe petrol filter.kabadili lakini bado ???.
shikamooo diagnosis machiney zimeharibu mafundi wengi sana aisee.na mm ilibakia kidogo niangukie huko aisee.nikaamua kutoitegemea kabisaa.
sasa hivi mafundi mmekuwa wazembe na wavivu sana ukimpa FUNDI Gari kama haiwaki TAA ya check engine basi ujue imekula kwako lazima atoke kapa hapo
Toyota Sienta, taa ya check engine imewaka takriban wiki tatu sasa, pia gari ukianza kuondoka inajivuta kama ina sense obstacle mbele, yaani ukikamyaga mafuta inasita kisha inafumguka hata ukiachia, fundi amecheck na kubaini fuel filter imeziba kwa uchafu. Inakuwaje wakati ameisafisha ikawa sawa kwa wiki moja tu tatizo limejirudia, au nimelenga asiye adui?
Naomba ushauri wataalam.
Kwanza fuel filter huwa ni ya kubadili na si ya kusafisha hilo ni kosa pia checki na fundi aangalie gearbox
Wadau kati ya raum new model n spacio IPI nzuri