Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #141
Pata petrol auto, ni rahisi kwa maintenance, VX za gear huja kusumbua baadae kwenye syncroniser za gear japo bado gari zote ni nzuri inategemeana tu na utunzaji kufuata taratibu za matumizi, uangalizi na service kwa muda sahihi na kutumia vitu genuine
Vilevile mamseri kuwa makini sana na kuagiza gari mtandaoni wameumizwa wengi sana kwa njia hii
Kinachotokea ni hiki kuna watu hapo Japan Hongkong China Dubai na kwingineko wamehack emails za ma dealers wakubwa wa magari wanaoaminiwa na wana accounts nyingi tu za kimagumashi
Wao kazi yao ni kufuatilia maelfu ya emails kila siku za wale madealer, kuanzia kuchagua gari mapatano mpaka kutuma kianzio ambacho mara nyingi ni 20-50%
Sasa inapofika wakati wa kutuma pesa wao huingilia mawasoliano na kudivert kwao na kukupa sababu anuwai kwa mabadiliko ya ghafla ya account na kukuomba utume kwenye account hiyo mpya
Ukiingia kingi ukatuma utaendelea kuwasiliana nao huku wakiendelea kutoa vidingizio kibao mpaka siku unayochoka na kuamua kupiga simu kwa dealer wako! Ndo hapo unapokuja kugundua kama ushaingizwa cha shoga which by then its too late
Last edited by a moderator: