Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

mkuu bado nasubir kwenye matumiz ya gear 1,2,3 baada ya D kwenye subaru forester

Mfumo ni ule ule kuwa baada ya D inayofuatia ni kwa ajili ya mwinuko, tifutifu, na utelezi kama kuna maelezo tofauti nitakujulisha
 
Kwa mfano kosa la kutofunga mkanda wa usalama halina madhara kwa wengine bali ni kwa usalama wako kwahiyo kinachotakiwa ni elimu na kuonywa

Mkuu samahani mimi nina maswali haya mawili ambayo yananitatiza sana:-
1: Over drive inakuwa ON na OFF muda gani kwa kuzingatia kuzima na kuwaka kwa taa ya dashboard?
2: kati ya vvt-i engine na 1g kavu ni ipi bora kwa kuzingatia yafuatayo?
A. Fuel consumption
B. Uimara
 
O/D unaiwasha mwenyewe na mara nyingi kuepuka confusion wengi huwa wanaiwasha moja kwa mojamoja na inapokuwa on huwezi kuona kwenye dashboard ila ikiwa off! Penguin baadhi ya magari inaonyesha on na off

VVTI ni nzuri sana kwa fuel consumption ila uangalizi wake unatakiwa wa karibu zaidi kuliko 1G kavu
 
Duu asante kaka,hebu ngoja nkaonane na fundi,ila timing belt yake ni zile za cheni,kama ya baiskeli hv,na zile huwa zinachokaga?naomba kujuzwa kwa hili Mkuu,ubarikiwe sana

Je yako hiyo ina milage ngapi~ila nachofahamu cheni yawezwa badilishwa kwenye 150,0000km ushauri huu ni kulingana na maintanance schedule ya toyota kuhusu hizo chains~lakini wanakuambia pia si lazima kwani hazikatiki~wanakuambia kama ni lazima ibadilishwa ni muhimu iwepo sababu ya kufanya hivo na sababu hiyo iwe-developed na toyota dealers wenyewe kwani kinyume na hapo unatafuta tatizo ambalo ni ngumu kulitatua na hasa kama utaibadilisha kwa mafundi wa vichochoroni

La muhimu tafuta fundi mzuri~aangalie hiyo check engine kwa nini inatoa hiyo warning!

Na fundi mwenyewe awe ni hawa wanaongalia system za gari kwa kutumia computer
 
Hili wameligomea hata sijui kwa nini, tumeomba sana sana!!!!
Linaweza punguza hata ajali za barabarani pia sababu tutakutana huko na kupeana ushauri!!!
MANI, RRONDO, Kaizer! !!
mshana jr kazi nzuri sana kaka, Invisible japo sticky meanwhile

Halafu nilitegemea niikute hii sredi sticky au iwe na jukwaa lake labda kule tekolojia na magadgets?
 
Last edited by a moderator:
Je yako hiyo ina milage ngapi~ila nachofahamu cheni yawezwa badilishwa kwenye 150,0000km ushauri huu ni kulingana na maintanance schedule ya toyota kuhusu hizo chains~lakini wanakuambia pia si lazima kwani hazikatiki~wanakuambia kama ni lazima ibadilishwa ni muhimu iwepo sababu ya kufanya hivo na sababu hiyo iwe-developed na toyota dealers wenyewe kwani kinyume na hapo unatafuta tatizo ambalo ni ngumu kulitatua na hasa kama utaibadilisha kwa mafundi wa vichochoroni

La muhimu tafuta fundi mzuri~aangalie hiyo check engine kwa nini inatoa hiyo warning!

Na fundi mwenyewe awe ni hawa wanaongalia system za gari kwa kutumia computer

Check Engine haiwaki kwa ajili ya timing belt, aende kwa fundi mwenye diagnostic tool nzuri amsomee hiyo code, wengi huwa hawajui kuzitumia hivyo wanadanganya tu.
 
Are you sure mate? Ukiweka N inabeep na kuashiria something is wrong. Kumbuka hii ina diff, na inavuta nyuma mzee
Jerrymsigwa yani ujue najibu kufuatana na nilichokiona hapo ningekuwa na demo nigeweza kuwa na majibu sahihi zaidi kwa hili naweza nisiwe sahihi sana
 
Last edited by a moderator:
Check Engine haiwaki kwa ajili ya timing belt, aende kwa fundi mwenye diagnostic tool nzuri amsomee hiyo code, wengi huwa hawajui kuzitumia hivyo wanadanganya tu.

Kwa uzoefu wangu hasa gari za kijapan kwanza life time ya timing belt ni km laki 1, na mara nyingi inapozidi hapo hiyo taa huanza kuwaka na kuzima japo magari ya siku hizi yenye sensors nyingi check engine yaweza kuwaka kutokana na fault nyingine pia lakini inayohusika na engine
 
Kumekuwa na mada nyingi kuhusu mambo yote yahusuyo magari, nikaona basi na sisi tuwe na Uzi huu ambapo habari zote zihusuzo magari kuanzia kuchagua, kuagiza, kuuza, kubadili nyaraka, matengenezo utunzaji na kadhalika.

Watu wengi wametapeliwa kwenye mauzo na manunuzi, kwenye nyaraka, kwenye vipuri kwenye matengenezo na hata matumizi.

Kwa Uzi huu basi kila mwenye ujuzi, uzoefu, ushauri au mwenye maswali na tatizo lolote linalohusiana na magari hapa ndio pawe uwanja wake

Karibuni sana

View attachment 225786

Mkuu mshana jr tunashukuru kwa proffessional response. Mimi naomba kuuliza ninapoweka gari on alama ya oil warning light inakuwa red na engine warning light inakuwa njano but ninapostart gari alama zote hupotea. Je happ kuna tatizo lolote?
 
Habari.
Gari langu (Will VS 1790cc) lilikuja toka Japan na spark plugs zenye muundo kama butu hivi, nikaitumia mwezi mmoja nikaipeleka kwa fundi just for check up. Bila kuangalia, akaniambia vitu vya kubadili ikiwemo oil na spark plugs. Akatoa hizo zenye umbo kama butu kwenye ncha (NGK-R BKR5EYA) akaweka NGK Iridium. Baada ya hapo nikaanza kuona kama fuel consumption imeongezeka. Je, kuweka plugs aina tofauti na zile zilizokuja na gari zaweza kuwa sababu ya fuel consumption kuongezeka?
NGK1.jpgiridium.jpg
 
Safiiii! Nafikiri kuna umuhimu wa kufikiria hata mambo ya NSSF, na mifuko mingine kwa mabeki 3!

Kwanza ulivotaja NSSF nimepata hasira ghafla.
Kama una hamu sana ya kujadili hao mahausigel si uanzishe na wewe uzi wako wa mahausigel, Mrs Kilewo atakuja kukusoma usihofu atakutangaza na kwenye TV!!??
Hii tabia ya kudandia nyuzi makini za watu ili upate umaarufu humu ndani akati ID yako fake haiwezi kukupa kick.
Tuache siye tujadiliane magari, we na ukuwadi wako wa NSSF mtafute mzee Majuto mjadiliane kule, siyo hapa.
Asumpta we...
 
Kwa madereva wa bus/gari ya abiria unaruhusiwa kugonga kama huwezi kusmima au kumkwepa mtu au mnyama mmoja akiwa upande wako wa kuendeshea ili kuokoa wengi.
 
Mkuu mshana jr tunashukuru kwa proffessional response. Mimi naomba kuuliza ninapoweka gari on alama ya oil warning light inakuwa red na engine warning light inakuwa njano but ninapostart gari alama zote hupotea. Je happ kuna tatizo lolote?

Kimsingi ndiyo ilivyo kuwa unapoweka switch on taa zote za alama mbali mbali kwenye dashboard lazima ziwake kisha gari ikashaka zizime itakayobaki on ndio inatayokujulisha tatizo
 
Kwa madereva wa bus/gari ya abiria unaruhusiwa kugonga kama huwezi kusmima au kumkwepa mtu au mnyama mmoja akiwa upande wako wa kuendeshea ili kuokoa wengi.

Sometimes dereva mzuri ni yule anayeepusha ajali na si yule anayefuata sheria
 
Habari.
Gari langu (Will VS 1790cc) lilikuja toka Japan na spark plugs zenye muundo kama butu hivi, nikaitumia mwezi mmoja nikaipeleka kwa fundi just for check up. Bila kuangalia, akaniambia vitu vya kubadili ikiwemo oil na spark plugs. Akatoa hizo zenye umbo kama butu kwenye ncha (NGK-R BKR5EYA) akaweka NGK Iridium. Baada ya hapo nikaanza kuona kama fuel consumption imeongezeka. Je, kuweka plugs aina tofauti na zile zilizokuja na gari zaweza kuwa sababu ya fuel consumption kuongezeka?
View attachment 226995View attachment 226996

Hilo ndio tatizo tafuta plug zake original au fanyia service za zamani tatizo litakwisha
 
Mshana hongera sana kwa uzi huu. Nina shida moja, naendesha noah hizi za zamani kidogo, sasa naweza niko speed 80 hivi, nikawa niko kwenye mteremko kidogo mara inabadili gear na kuingia gear kubwa zaid, inabidi nibonyeze over drive kwa maana ya ku off na ku on kwa mara moja, ndio inaingia gear ndogo, au wakati wa kuondoka ikang'ang'ania kwenye namba 3 hadi ubonyeze hiyo batan ya off na on kwa wakati mmoja. Nimeservice gear box, bado tatizo lipo.
 
Yani shayookoko usijaribu tena hata siku moja ku dis-engage O/D gari ikiwa speed 80+!!! Vile vile gari yeyote ya auto haihitaji msaada wa wa mwendeshaji zaidi ya kupunguza mwendo au kuongezeka.! Sana sana ni na kati za ku engage extra power nk
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom