Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Vilevile mamseri kuwa makini sana na kuagiza gari mtandaoni wameumizwa wengi sana kwa njia hii
Kinachotokea ni hiki kuna watu hapo Japan Hongkong China Dubai na kwingineko wamehack emails za ma dealers wakubwa wa magari wanaoaminiwa na wana accounts nyingi tu za kimagumashi

Wao kazi yao ni kufuatilia maelfu ya emails kila siku za wale madealer, kuanzia kuchagua gari mapatano mpaka kutuma kianzio ambacho mara nyingi ni 20-50%

Sasa inapofika wakati wa kutuma pesa wao huingilia mawasoliano na kudivert kwao na kukupa sababu anuwai kwa mabadiliko ya ghafla ya account na kukuomba utume kwenye account hiyo mpya

Ukiingia kingi ukatuma utaendelea kuwasiliana nao huku wakiendelea kutoa vidingizio kibao mpaka siku unayochoka na kuamua kupiga simu kwa dealer wako! Ndo hapo unapokuja kugundua kama ushaingizwa cha shoga which by then its too late
 
Last edited by a moderator:
Nini tofauti ya rav 4 L na J? Kodi ya rav 4 L 5door ya waka 2005 ni kiasi gani? Nataka gharama kutokana na uzoefu sio theoretical ya tra calculator maana hawazifuati zile mshana jr
 
Mmh hili Hapana wehoodie sina utaalam kivile ila kuna mtaalam asubuhi nitamwalika hapa Mazoko tafadhali ukiona hii post tia neno
 
Last edited by a moderator:
Mfikilwa big horn ni magari nyanya mno na likichakaa linachukiza mno, landrover japo spare zake ni ghali lakini ni gari ya uhakika zaidi
Tunaondoka kwenye kizazi cha manual hivyo chukka tu auto na uzi gate service

Maelezo yako hayako kitaalam.
Inategema unanunua gari kwa matumizi gani,mfano hiyo big horn sio gari ya field kwa maana haiko imara kwenye barabara zenye msukosuko wakati td5 iko kwaajiri ya kazi
Kuchakaa kwa gari nimatunzo
 
Last edited by a moderator:
Jamani kati ya Mark X na Nissan Fuga ipi iko poa, kwenye stability, uimara, na utumiajiafuta. Nawskilisha
 
Mazoko maelezo yangu ni ya binafsi zaidi kutokana na uzoefu binafsi lakini tukishirikiana kama hivi inakuwa bora zaidi ndio maana kuna huu uzi lakini kwa hizi gari mbili bado big horn ni nyanya kwa td5
 
Last edited by a moderator:
mkuu gearbox mpya za landcruiser 1h zinapatikana bongo hii wapi..
 
mkuu gearbox mpya za landcruiser 1h zinapatikana bongo hii wapi..

Toyota Tanzania ila bei yake kiama! Nakushauri kama una access na Nairobi agiza huko
 
Swala langu linafanana sana Na Born again Pagan!
 
Jamani kati ya Mark X na Nissan Fuga ipi iko poa, kwenye stability, uimara, na utumiajiafuta. Nawskilisha

Nissan models nyingi zina sifa nzuri ya fuel consumption na ndani yana nafasi kubwa japo mara nyingi body ni jepesi
 
Jamani nataka kuagiza Altezza sasa nataka ya 4c siyo ya 6c nazitofautishaje na je ipi ni nzuri ya 4c au ya 6c maana nasikia ya 6c ni balaa inakata wese vibaya

Hamna mtaalam ya hili?
 
Wakuu nauliza nina gari yangu Rav 4,2000 model mtaani wanaita KILITIME,Engine D4,sasa issue ni kuwa nikiwasha gari engine ikiwa haijapata heat taa ya check engine inawaka,ila ikishatembea km chache inazima na haiwaki,tatizo ni nn?ila Kwenye performance ya engine Haina shida kabisa.
 
Vipi wakuu,Naomba ushauri,gari ya 1500 cc Mfano toyota premio au allion ulaji wake wa mafuta upoje na je ni economy kwa mazingira ya dar?natanguliza shukrani
 
Hiyo ni tahadhari ya timing belt, imechoka ni ya kubadili kuna wakati itakuwa inawasaidia moja kwa moja hapo ujue inaweza kukatika muda wowote
 
Vipi wakuu,Naomba ushauri,gari ya 1500 cc Mfano toyota premio au allion ulaji wake wa mafuta upoje na je ni economy kwa mazingira ya dar?natanguliza shukrani

Gari yeyote yenye cc chini ya 1500 ni nzuri kwa misele ya mjini
 
Duu asante kaka,hebu ngoja nkaonane na fundi,ila timing belt yake ni zile za cheni,kama ya baiskeli hv,na zile huwa zinachokaga?naomba kujuzwa kwa hili Mkuu,ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…