Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Ni kweli kabisa,huu uzi uko makini sana asanteni sana wataalamu kwa kutuelimisha.binafsi napata uelewa mkubwa sana kupitia hapa
 
Ahsante mkuu. Kuna rafiki angu aliniambiaga kuwa mazuri ni unleaded,na ndio most yanayojazwa ktk vituo vya puma. Nitaanza kuzingatia aina za mafuta na petrol station za kujaza mafuta,na sio kujaza mafuta ovyo ovyo ktk petrol station.

Yeah utaratibu mzuri uwe na vituo unavyoviamini kwa hapa Tz puma na total mi nawa-rate nafuu hawa wengine wasiwasi wengine wanasema victoria pia sio wachakachuaji

Yeah Puma, Total na Engen at least you can rely on them! Niliwahi kutembelea makao makuu ya Engen Tanzania pale kurasini nilivutiwa mno na jinsi wanavyoyatunza mafuta yao kuanzia kwenye visima na matanki yao! Kuna kila aina ya precautions

Matank mengi na magari yanayohifadhi na kubeba mafuta hayana viwango na mengi huliwa na kutu haraka huku yakiruhusu leakage ambapo aidha mafuta hupotea au kupoteza nguvu au huruhusu maji na kutu kuchachanyika na mafuta hivyo kuleta matatizo makubwa kwenye mfumo wa engine
Engen wana kila kitu cha kulinda hiyo hali kwahiyo hata kama tank limefukiwa ardhini lakini limefungwa detectors za kudetect chochote ambacho kitaathiri ubora na utunzaji wa mafuta husika, naamini hata Puma formally BP na TOTAL wana hiyo mifumo
 
Nafikiri tayari iko sticky! Binafsi ufahamu wangu kuhusu magari umeongezeka maradufu, nafuatilia kila post kwa makini mno na kwakweli wachangiaji wengi wamekuwa serious kwenye kutaka kufahamu hili au lile na vilevile wale wenye ufahamu nao wamekuwa na weledi na upendo mkuu kushare kile wengine wasichokijua

Kweli mkuu hata ukifuatilia forums za magari za wenzetu huko mbele hawabaniani uelewa wa magari mf kuelekezana mahali zilipo spea fulani,jinsi ya kuepuka engines vimeo,uwezo wa gari,sheria za traffic nk kiukweli ktk threads makini hii mojawapo mkuu
 
Mkuu naomba ushauri kuhusu pajero GDI io kuna MTU anataka aniuzie coz anashida so nataka kujua ubora na udhaifu wake...

Sorry najua ulimwuliza lusungo lakin naweza weka langu moja...injiniwise hakuna tatizo ni economy na inatengenezeka kirahisi suala uzingatie matengenezo na pia injini yake ipo kwenye kundi la zile zinazochoma moja kwa moja shida yake huwa ni bodi,bodi la pajero iO huwa ni delicate sana mengi tunayoyashughulikia hapa yanakuwa yameliwa na kutu kwenye maungio ya bodi na fremu ila injini usiwe na waswasi
 
Nashukur sana kaka kwa ushauri pia ni kampuni gani nzuri kuagizia

Kama ni muagizaji mpya nakushauri uwaone Be forward wanakushughulikia kila kitu kuanzia Japan hadi gari linakufikia pia wana clearing agency hapa Tanzania pale jirani na ocean roads hsptl na unaweza ukaagizia gari lako pale ofisini kwao BFT na kupata technical advice zaidi kutoka kwao they're professional na wako serious kwenye business, pia bei zao ni nzuri na wana magari mengi kuchagua
 
Shukran mkuu ijumaa ntaenda kuwaona
 
Kinachonikera hawa jamaa ni kubandika sticker zao kwenye magari wanayouza, nafikiri si kila mtu anapenda kuwa na vitu kama hivyo kwenye gari
Kama watapita huku naamini ujumbe huu utawafikia, ni vema kumuuliza mteja kama anapenda au la
 
Ni kweli mkuu huwa wanaweka stickers kubwa lakini siku hizi wameziboresha ni ndogo,muhimu ni kuing'oa baada ya kulipokea then unasafisha na Colgate
 
Wakuu nahitaji Noah ambayo ni manual gear..naweza kuipata?
 
Naomba kufahamu tyre ya gari inasomwa vp kujua imetengezwa muda gani
 
Kinachonikera hawa jamaa ni kubandika sticker zao kwenye magari wanayouza, nafikiri si kila mtu anapenda kuwa na vitu kama hivyo kwenye gari
Kama watapita huku naamini ujumbe huu utawafikia, ni vema kumuuliza mteja kama anapenda au la

Hata mi sipendi mastika...niliagiza gari.ilipofika pale ofisini kwao nikatoa stika zote
.walipouliza.nikawaambia ile si ubao wa matangazo pia sina makubaliano kuwatangazia.over
 
Hata mi sipendi mastika...niliagiza gari.ilipofika pale ofisini kwao nikatoa stika zote
.walipouliza.nikawaambia ile si ubao wa matangazo pia sina makubaliano kuwatangazia.over

😀 ulitisha mkuu,tunawapromote bure hawa dealers sema na baadhi ya watu wanadhan ni ujiko kuweka mabango!
 
Wakuu nataka kununua Paso kwa mizunguko ya mjini tu. Je inafaa? vp uimara wake na ulaji wa mafuta?
Au ni gari ipi ndogo ambayo ni bora zaidi.
Nb. Bei iwe kama ya Paso au ikizidi basi isizidi mil 8.
 
Wakuu nataka kununua Paso kwa mizunguko ya mjini tu. Je inafaa? vp uimara wake na ulaji wa mafuta?
Au ni gari ipi ndogo ambayo ni bora zaidi.
Nb. Bei iwe kama ya Paso au ikizidi basi isizidi mil 8.

Hapa ngoja N'yadikwa aje
 
Last edited by a moderator:
Hivi gongo chura zinapatikana wapi? Ni zile za kizamani, nahitaji mpya sasa sijui bado zinatengenezwa, je kuna uwezekano wa kuagiza?
 
Hongera mshana jr...naona mada imekuwa sticky...
Wakuu, kuna subaru forester 2004 inasumbua kwenye giabox...tatizo gia kuingia inakuwa shida...ukiweka D inapiga resi tu...na ikiondoka ni kwa shida..
msaada tafadhali!
 
Kwa uzoefu wa kawaida gearbox inahitaji service lakini vema pia ukaonana na wataalam wa Subaru wafanye uchunguzi wa kina
 
Back
Top Bottom