Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Habari wana Jf, naomba ushauri kwa watalaamu wa magari, nataka kununua Daihatsu Terios vipi kuhusu ubora wake na kwa matumizi ya TZ.
 
Ahsante mkuu mshana mungu akubariki
Swali langu la nyongeza mimi gari yangu ni Toyota Duet kila nikiiwasha lazima ioneshe taa zote pale kwenye dashboard ikiwemo na hiyo ya ABS lkn huwaka kwa muda tu pindi ninapoondoka au kuwa silence haiwaki je hilo ni tatizo la break system?
Lkn pia gari yangu ina tatizo la kuvuta upande wa kushoto yani ukiwa unaendesha halafu ukaachia usukani utaona gari inaelekea upande wa kushoto
 
mbogyo taa za dashboard huzima mara baada ya kuwasha gari , taa itakayobaki inawaka ni tahadhari ya kukuambia kuna tatizo kwahiyo ABS yako iko vizuri
Ishu ya gari kuvuta upande mmoja inabidi ufanye wheel alignment na wheel balancing au pia uangalie upepo kama uko sawa kwa tairi zote mbili
 
Last edited by a moderator:
Halafu tujue wewe he au she.

Naomba msininukuu vibaya jama hivi vigari naona vimekaa kike sana unless uwe mwanafunzi wa chuo.
 
Hivi vina tofauti na Toyota Cami?
Terious KID na Terious ina tofautti?
spea zake available?
 
Ni aina moja ila wametofautisha majina tu,kwamba moja ni Terrios Kid nyingine Terrios Cami ila ziko sawa na spare zake zipo but bei zake ni kubwa kiasi chake,yaani tuseme service atakayofanya mtu mwenye Terrios kwa ajili ya mizunguko ya kawaida mjini cost yake inalingana(inaweza kupita) na service atakayofanya mtu mwenye Spacio au Corona Premio kwa ajili ya long safari. the boss
 
Last edited by a moderator:
habari wadau,nahitaji fundi anayeweza kubadilisha mfumo wa freelander 2 manual 4wd nakuniwekea wa rav4 3s manual 4wd
 
Naona tumejikita zaidi kwenye mambo mengine na kusahau hili la rangi za magari na utunzaji wake
Kwanza kwenye gari kuna rangi za aina mbili metallic paints na non metallic paints
Utunzaji wa metallic paints(rangi za mng'ao) ni mgumu/ghali zaidi kuliko ambazo sio metallic, na ndio maana metallic paints kwa asilimia 95 utazipata kwenye magari madogo na ya starehe au matumizi binafsi huku yale ya non-metallic yakiwa ya biashara

Ni jambo la kawaida ni ada kuliweka gari lako katika hali ya usafi na kung'aa muda wote lakini bahati mbaya sana kwa kutofahamu usafi huo kama hauzingatii kanuni basi rangi huchoka haraka sana

Kumbuka Hays unapoosha gari yako
-hakikisha maji yanayotumika si ya kisima kifupi wala mitaroni, mengi yana chumvi na chemikali nyinginezo ambazo ni sumu kubwa kwa bati na rangi ya gari
-hakikisha unakuwa na sabuni maalum ya kuoshea magari(car shampoo) epuka kutumia sabuni za unga ambazo kemikali zake ni kwa ajili ya nguo, vyombo nk
-epuka kutumia material yoyote ngumu kukaushia gari mara baada ya kuosha hasa rangi za metallic ambazo hupata michubuko haraka
-epuka kuishindisha gari juani kila siku
-kama gari si chafu kivile osha kwa kuifuta na kitambaa laini na maji tupu
-Fanya car waxing walau mara moja au mbili kwa mwezi
-Fanya fullbody washing walau mara 2 kwa mwezi
Ukizingatia hayo rangi yako itadumu na kubaki na mng'ao wake wa asili
 
Waone hawa.... nimekopi hii thread kutoka jukwaa kazi;

Yesterday
sisi ni vijana watatu kutoka toyota tz
,tunatengeneza
engine aina zote hasa za V8.Yeyote mwenye
kuhitaj huduma yetu tuwasiliane no.0766981308
tunakufuata ulipo DAR

habari wadau,nahitaji fundi anayeweza kubadilisha mfumo wa freelander 2 manual 4wd nakuniwekea wa rav4 3s manual 4wd

Fanya mawasiliano na hao
 
Naona tumejikita zaidi kwenye mambo mengine na kusahau hili la rangi za magari na utunzaji wake
Kwanza kwenye gari kuna rangi za aina mbili metallic paints na non metallic paints
Utunzaji wa metallic paints(rangi za mng'ao) ni mgumu/ghali zaidi kuliko ambazo sio metallic, na ndio maana metallic paints kwa asilimia 95 utazipata kwenye magari madogo na ya starehe au matumizi binafsi huku yale ya non-metallic yakiwa ya biashara

Ni jambo la kawaida ni ada kuliweka gari lako katika hali ya usafi na kung'aa muda wote lakini bahati mbaya sana kwa kutofahamu usafi huo kama hauzingatii kanuni basi rangi huchoka haraka sana

Kumbuka Hays unapoosha gari yako
-hakikisha maji yanayotumika si ya kisima kifupi wala mitaroni, mengi yana chumvi na chemikali nyinginezo ambazo ni sumu kubwa kwa bati na rangi ya gari
-hakikisha unakuwa na sabuni maalum ya kuoshea magari(car shampoo) epuka kutumia sabuni za unga ambazo kemikali zake ni kwa ajili ya nguo, vyombo nk
-epuka kutumia material yoyote ngumu kukaushia gari mara baada ya kuosha hasa rangi za metallic ambazo hupata michubuko haraka
-epuka kuishindisha gari juani kila siku
-kama gari si chafu kivile osha kwa kuifuta na kitambaa laini na maji tupu
-Fanya car waxing walau mara moja au mbili kwa mwezi
-Fanya fullbody washing walau mara 2 kwa mwezi
Ukizingatia hayo rangi yako itadumu na kubaki na mng'ao wake wa asili

Shukrani mkuu mshana...
 
Hizi gari ni nzuri kwa ulaji wa mafuta na mizunguko ya mjini tu, kwa safari ndefu hazifai ni nyepesi,kupata spea zake ni shida mno,kwenye used ndo usiseme ukienda tu kuuliza watakuambia hizo spea utahangaika sana labda ubahatishe,mm steering reck to iliisha nilitafuta mpya nikakosa nikaenda used kila sehemu sikupata,nikaulizia hadi japan wakaniambia hakuna labda upate gari iliokatwa,baadhi ya spea ambazo utabahatisha huku bei yake iko juu sana
 
Hivi vina tofauti na Toyota Cami?
Terious KID na Terious ina tofautti?
spea zake available?

Hakuna tofauti kati ya cami na terious na hata spea ya cami ukiuliza kwa jina la cami hupati!uliza kwa jina la terious.tofauti ya toyota cami,terious na terious kid ni cc,toyota cami na terious ni cc1246 wakati terious kid ni cc 660
 
Gari ambayo naona kidogo imekaa vizuri ni DAIHATSU BE-GO,cc 1490,ki muonekano iko sawa na Rush,na hata injini yake na rush iko sawa
 
Halafu tujue wewe he au she.

Naomba msininukuu vibaya jama hivi vigari naona vimekaa kike sana unless uwe mwanafunzi wa chuo.

Unauwa mkuu, hivi vigari mbona havina male or female, havijaandikwa kwenye registration? Ikiwa 3 doors inakalia kike not 5 doors. 😁
Gari ni economy sana
 
Habari wana Jf, naomba ushauri kwa watalaamu wa magari, nataka kununua Daihatsu Terios vipi kuhusu ubora wake na kwa matumizi ya TZ.

Nunua bwana, gari nzuri kwa mahitaji yetu Tanzania kutokana na uchumi wetu wa kimaisha, hazina tatizo la engine, ni service tu inahitajika.
 
Nashukuru kwa maswali na majibu ambayo yamenifungua upeo wangu wa kuelewa magari,nina swali kwa wadau,nimesafiri na gari yangu Noah kwenda mkoa tatizo ni pale nikiwa kwenye speed zaidi ya 80 kila nikigusa break gari inatingishika mno,je nini tatizo???
 
Viashiria ni vingi kuchoka kwa break pads, ball joints lakini pia kuna wakati ni tatizo la alignment na balancing ya front tyres(I may be corrected)
 
Back
Top Bottom