Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

DONDOO YA LEO KUHUSU TAIRI:
»»»»Hakikisha kiwango cha upepo kwenye matairi yako hakiwi cha juu kabisa "yaani kile cha mwisho"
KWANINI:
1-Hatari ya kupasuka huwa kubwa zaidi.
2-Uwezo wa tairi kunasa vema barabara unapungua
3-Mara nyingi tairi huchakaa katikati kwa sababu ukijaza sana upepo kuna umbile la karai dome shape hujitengeneza eneo la katikati hivyo kona za tairi hugusa chini kidogo na kusababisha uchakavu katikati.
3-Udhibiti wa kona na breki hususani za haraka hupungua gari huweza kuserereka na hata kusababisha ajali.
Asanteni...psi recommended ni Kati ya psi 30-35 hata hivyo rejea operational manual yako Hakikisha unazingatia hilo usijaze upepo bila kujua kiwango cha upepo uliomo ktk gari.
.....Usipime upepo tairi zikiwa za moto Subiri zipoe au pima na kujaza upepo wakati ukiiamsha gari asubuhi.
MUHIMU: Tairi la gari yako ni kiungo kikubwa sana cha usalama wako...zaidi waone MAKANIKA WATAALAMU wa matairi wakupe ushauri stahiki.
MWISHO: Usisubiri kubadili tairi likiwa chakavu kabisa na wakati wote sisitiza tairi orijinali achana na bandia au mkono wa pili ni hatari.
 
Very well saidi kiongozi
 
Tazama picha jinsi ya kufahamu tairi lako lilitengenezwa mwaka gani.

Katika hiyo picha ZINGATIA: DOT U2LL LMLR5107
51=wiki ya 51 ya mwaka.
07=2007[mwaka].

KANUNI hii ya utambuzi umri wa tairi inatumika tangu Y2K

Sasa ili kufahamu umri wa tairi lako maandishi hayo yapo pembeni ya tairi lako...USITUMIE TAIRI ZAIDI YA MIAKA 5.(wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti).
 
Attachments

  • 1429114303598.jpg
    1429114303598.jpg
    12.4 KB · Views: 349
Tazama picha jinsi ya kufahamu tairi lako lilitengenezwa mwaka gani.

Katika hiyo picha ZINGATIA: DOT U2LL LMLR5107
51=wiki ya 51 ya mwaka.
07=2007[mwaka].

KANUNI hii ya utambuzi umri wa tairi inatumika tangu Y2K

Sasa ili kufahamu umri wa tairi lako maandishi hayo yapo pembeni ya tairi lako...USITUMIE TAIRI ZAIDI YA MIAKA 5.(wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti).

Gari nyingi za diplomats na viongozi wanafunga genuine n brand new tyres na zikitembea kati ya km 30-40 elfu zinabadilishwa bila kujali upya wake.
 
Kibongobongo tunanunua mkono wa pili au kutumia ya bei chee nadhani ni sababu ya ukata

Kuna mambo mawili muhimu ambayo hatuzingatii
1. Kutotaka kufanya mwenyewe, unamtuma kijana akanunue genuine brand new lakini anakupiga

2.wapande wanakukoleza kuwa used ndio genuine, na kwakuwa hujui mambo ya tairi unaingia mkenge
 
Mambo ya 10% mkuu njaa kali
 
Mkuu hayo yote ni magari poa kabisa japokuwa Mazda Tribute watu wanaziogopa bure Tribute zinaingiliana spare nyingi tu na Suzuki Escudo/vitara kama nayoisukuma japo Dar sio nyingi lakini ni suv poa kabisa urari wake ni kwamba zote ni imara sana na spare zake zinapatikana bila wasiwasi,mapenzi yake tu yaamue asiiogope,spare za hayo yote zipo,Subaru hata siizungumzii coz zipo hapa town za kutosha hivo hata asiogope. Tribute ni genre moja na Suzuki Escudoz so mwambie asiogope hayo yote yanatengenezeka vizuri kabisa.

Mkuu asante kwa hili.
Vipi MAZDA AXELA SPORT kuhusu ubora,uimara , upatikanaji wa spea na uingilianaji wa spea na aina nyingine za magari?

Asante in advance.
 
Sina ujuzi sana kwenye hili lakini nafikiri kuna kitu kinaitwa sleeves, au Cylinder head gasket imechoka, mwenye ujuzi zaidi anaweza kuja tafadhali

Kaka nashukuru sana na wengine wanaotupa darasa hapa wote asanteni, nilikwenda kwa fundi baada ya kueleza tatizo la gari(bila kumwambia chochote nlichoshauriwa hapa JF) alipofungua kuangalia akakuta cylinder head gasket imeungua na top cover nayo ilishakwisha kazi yake nimevibadilisha sasa hivi mwendo mdundo.

Hapo mafundi wengine walishaniambia ninunue engine mpya dah!
 
Wadau habarini,jamani hizi ajali ajali unapokuwa na vigari vidogo hivi jamii ya passo na wenzake risk inakuwa kubwa zaidi,bora turudi kwenye malori yetu tuu ma vitara,.
Naombeni mnijuze bei ya suzuki vitara au escudo model ya zamani jamani., yard na pia kama ukiagiza inakuwa milion ngapi maana hizi biashara za kununua magari kwa mtu ni shida.sana,jamaa zangu kadhaa wanajuta kununua gari kwa waswahili,labda uotee upate ya muhindi.
 
Mkuu unaposema zamani una maanisha nini?ImageUploadedByJamiiForums1429151115.176574.jpgImageUploadedByJamiiForums1429151150.115751.jpg

Hiyo kwangu ni ya zamani 2006 model ni m30-35 unapata
 
mshana jr
My dear nimefurahishwa sana na ujuzi pamoja
ushauri unaotoa.

Binafsi ningeomba kuuliza je ni gari lipi
Kununua ajili ya safari za mara kwa mara
Kutoka Dar mpaka Manyara .na mara nyingi kwenda kijijini ambapo hamna lami na mvua ikinyesha ndio balaaa zaidi. nataka gari ambalo naweza kutembela mjini na kupiga nalo safari ndefu pia. Any suggestions ?

Asante sana.
 
Last edited by a moderator:

afrodenzi nafikiri kwa uzoefu wangu Kwa vyovyote unahitaji gari yenye four wheel drive, sasa katika range ya magari unayopendelea kipe kipaumbele kigezo cha 4WD
 
Last edited by a moderator:
mshana jr
My dear nimefurahishwa sana na ujuzi pamoja
ushauri unaotoa.

Binafsi ningeomba kuuliza je ni gari lipi
Kununua ajili ya safari za mara kwa mara
Kutoka Dar mpaka Manyara .na mara nyingi kwenda kijijini ambapo hamna lami na mvua ikinyesha ndio balaaa zaidi. nataka gari ambalo naweza kutembela mjini na kupiga nalo safari ndefu pia. Any suggestions ?

Asante sana.

Tafuta Sports Utility Vehicle (suv) mfano Suzuki, harrier, rav 5, etc hada zenye 4wd. Mostly zina cc 2000 na kuendelea
 
Last edited by a moderator:
Wadau....suzuki kei vip ....kwa safari za mjini mjini....wenye uzoefu na aina hii ya gari tafadhali....hasa ubora wa injini yake...
 
Wadau heshima kwenu, jamani kuna tofauti gani kati ya RAV 4 hizo hapo juu? Kwenye swala la quality, efficiency, economical in fuel consumption, durability etc ipi nzuri zaidi?
He hizi ndo zinaitwa Rav 4 Kill time mtaani?
Asanteni kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom