N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
DONDOO YA LEO KUHUSU TAIRI:
»»»»Hakikisha kiwango cha upepo kwenye matairi yako hakiwi cha juu kabisa "yaani kile cha mwisho"
KWANINI:
1-Hatari ya kupasuka huwa kubwa zaidi.
2-Uwezo wa tairi kunasa vema barabara unapungua
3-Mara nyingi tairi huchakaa katikati kwa sababu ukijaza sana upepo kuna umbile la karai dome shape hujitengeneza eneo la katikati hivyo kona za tairi hugusa chini kidogo na kusababisha uchakavu katikati.
3-Udhibiti wa kona na breki hususani za haraka hupungua gari huweza kuserereka na hata kusababisha ajali.
Asanteni...psi recommended ni Kati ya psi 30-35 hata hivyo rejea operational manual yako Hakikisha unazingatia hilo usijaze upepo bila kujua kiwango cha upepo uliomo ktk gari.
.....Usipime upepo tairi zikiwa za moto Subiri zipoe au pima na kujaza upepo wakati ukiiamsha gari asubuhi.
MUHIMU: Tairi la gari yako ni kiungo kikubwa sana cha usalama wako...zaidi waone MAKANIKA WATAALAMU wa matairi wakupe ushauri stahiki.
MWISHO: Usisubiri kubadili tairi likiwa chakavu kabisa na wakati wote sisitiza tairi orijinali achana na bandia au mkono wa pili ni hatari.