Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Nami naomba kuuliza, hivi mtu akakugonga barabarani, ni njia gani nitatumia ya kumuita trafic haraka afike kwenye eneo la tukio?
 
Nami naomba kuuliza, hivi mtu akakugonga barabarani, ni njia gani nitatumia ya kumuita trafic haraka afike kwenye eneo la tukio?

Ukiwa mbali na mji au Karibu na mji? Kwa kawaida kuna police post nyingi tu na askari wa doria pamoja na raia wema ambao wanaweza kukusaidia
 
Ukiwa mbali na mji au Karibu na mji? Kwa kawaida kuna police post nyingi tu na askari wa doria pamoja na raia wema ambao wanaweza kukusaidia

Nashukuru kunijibu mshana jr, ila nataka pia kujua kama ukiwa karbu na mjini na huoni askari yeyote karbu na tukio, kuna namba maalum za kuwapigia hawa askari?
 
Nashukuru kunijibu mshana jr, ila nataka pia kujua kama ukiwa karbu na mjini na huoni askari yeyote karbu na tukio, kuna namba maalum za kuwapigia hawa askari?

Sanasana ni namba za dharura sidhani kama wana namba maalum
 
Utakua umebadili ukubwa wa tairi mfano labda ilikua 185 we ukaweka 195 au vise versa

Mi tairi zangu ni 205/65R15 ambazo original yake. Ila naomba elimu zaidi kuhusu uhusiano uliopo kati ya size ya tairi na odometer reading.
 
Mi tairi zangu ni 205/65R15 ambazo original yake. Ila naomba elimu zaidi kuhusu uhusiano uliopo kati ya size ya tairi na odometer reading.

Kuna snapshot nimeweka ukiangalia kwa makini utaona tairi mbili za 195na185*jinsi zinavyotofautisha usomaji kwa elimu zaidi download software ya tire expert ipo play store
 
Ikiwa tairi yako ni mpya, na ni original size iliyopendekezwa na mtengenezaji wa gari na upepo umejaza kulingana na ujazo uliopendekezwa kwa uzito ulio nao hakuna mabadiliko katika odometer na umbali halisi.Ikiwa tairi imelika madhalani millimita mbili basi kipenyo kitapungua kwa milimita nne, katika hali hii odometer yako itasoma zaidi ya mwendo halisi.
Kwa tairi 205/65R16 in maana 205 ni upana wa tairi ikiwa na upepo sawia. 65 ni asilimia ya ya tofauti ya kipenyo kila upande(profile ratio) na 16 ni kipenyo cha rim yaani 16"
Kupata kipenyo(k) cha tairi ktk mm fanya 16" ni 16*25.4 (mm406.4 kipenyo cha rim)+(205*65%*2)=672.9mm
Hivyo Mzingo(circumfrence) wa tairi size 205/65R16 ni k*PI = 672.9*3.14=mm2112.906= 2.112906m.
Katika kilomita moja ni mita1000 unapata mizunguko 1000/2.112906 = 473.28 ambapo odometer itasoma pia 1km kwa tairi yenye vigezo vya hapo juu. Ikiwa tairi imelika madhalani 2mm kwa uwiano basi itakuwa imelika 2*2=4mm hivyo kipenyo inakua 672.9-4=668.9mm na mzingo ni 668.9*3.14= 2.100346mtrs. Kwa mizunguko 473.28*2.100346 utasafiri mita 994.05175488 pungufu ya mita 5.9 ulizosafiri lakini odomita inasoma 1km(mita1000).
Naamini utanielewa ukienda taratibu.
 
Kwa kawaida kwa tairi zote size eg 205/65r16 inafuatiwa na namba na herufi eg100H. 100 ina maana ya uzito wa tairi(load index) na H ni speed rating. Hizi ni muhimu sana kukuongoza uzito unaoweka na mwando unaokwena. Hapa 100 husimama kama kilo 800 kwa tairi na H ni 240km/h katika standard provision. Kadiri unavyoongeza mzigo ndivyo speed itakavyopungua. Load index ya magari ya abiria na magari magari madogo(light trucks) huwa ni kati ya 70-110.
Hili ni somo muhimu sana ambalo kwa kweli mara nyingi wengi hatuzingatii mahitaji ya tairi zetu na kujifunza ili kufuata masharti. Tairi ni mojawapo ya sehemu sana ya gari ya kujalu sana kabla hujawasha gari na kuondoka.
 
Habari zenu wadau. Mwenzenu nahitaji kununua gari, Na nimependa hizi gari Nissan sasa wadau kwa uzoefu wenu ni ipi gari nzuri kwa maana ya Uzuri kwa maana ya muonekano, Uhimili wa misukosuko na hasa kwa kuzingatia ubovu wa barabara zetu lakini pia na ulaji wa mafuta. Naomba kuwasilisha ninunue gari gani kati ya Nissan FUGA na Nissan TEANA Asanteni wadau nasubiri ushauri wenu.
 
kama kuna MTU anaweza ni shauri pia kuhusu ubora na udhaifu wa Nissan Tiida anapomjibu Mr. Bean nitashukuru pia
 
Kiasili make nyingi za Nissan ni magari imara sana lakini pia gari nyingi za kisasa body zake zimekuwa nyanya sana
Tiida Teane Duga zote ni nzuri japo zinatofautiana ulaji wa mafuta kulingana na ukubwa wa engine
 
heshima kwenu,
nina swali kwenu,hv je ktk hii nchi yetu tanzania,kulingana na sheria zetug,je. kama mtu anataka kupata kadi ya gar au pikipk,pale tu unapokuwa na chombo kisichokuwa na kadi je unafanya nini?
nawakarisha majibu kwa msaada kwa wengne.
 
Mwenye uzoefu NA kuifahamu gari hii TOYOTA AQUA ubora wake ulaji mafuta NA upatikanaji WA spare zake
 
Back
Top Bottom