Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Habari wana jamvi ,

Nina toyota crown nimekuwa nikiitumia kwa mda mrefu ,

Leo katika kuwasha gari asubuhi ,ghafla nakuta gauge /mshare wa mafuta haufanyi kazi vizuri ,yaani unashuka na kupanda mafuta yapo robo tatu tanki.

Vile vile odometer yaani kilometa za gari hazitembei kabisa ,yaani namba hazisogei kabisa zimebaki pale pale .

Msaada wa mawazo nijue ABC ya tatizo kabla sijaenda kwa fundi.

Natanguliza shukrani.
Tafadhali pata fundi mwenye mashine ya diagnosis kuepuka kubahatisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
b8d1f3c193782902cc65def3ea59a608.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni msaada. Nimenunua Voxy first generation engine ya 1az fse wengine wanaiita D4.
Inakula mafuta balaa. 1 litre kwa 3km.
Na kwenye mlima haina nguvu kabisa hasa ukiwa na watu. labda uwashushe ndio uendelee na ni mwinuko mdogo tu.

Nimejaribu kuuliza mafundi mbalimbali sijapata jibu. Naombeni msaada wenye uzoefu na hizi engine.
Hapo lazima ukonde mzee wangu.
 
Habari wana jamvi ,

Nina toyota crown nimekuwa nikiitumia kwa mda mrefu ,

Leo katika kuwasha gari asubuhi ,ghafla nakuta gauge /mshare wa mafuta haufanyi kazi vizuri ,yaani unashuka na kupanda mafuta yapo robo tatu tanki.

Vile vile odometer yaani kilometa za gari hazitembei kabisa ,yaani namba hazisogei kabisa zimebaki pale pale .

Msaada wa mawazo nijue ABC ya tatizo kabla sijaenda kwa fundi.

Natanguliza shukrani.
Ulinunua bei gani, kama una mpango wa kuliuza mwisho wa mwaka utanicheki pm mkuu.
 
Hakuna anayebisha kwamba kitendo cha kukutana na namba E zikiwa nyingi mtaani kinatosha kutupa ishara kwamba idadi ya magari yanayonunuliwa na kuingizwa Tanzania inazidi kuongezeka mara dufu siku hadi siku na wengi wetu tunafahamu kwamba Japan ndiko magari 'used' yanakonunuliwa kwa wingi kwenye minada.

Kwa kuwa idadi kubwa ya magari yanayonunuliwa na Watanzania ni yale yaliyokwisha tumika (used), haya ni mambo matano ambayo tunatakiwa tuyazingatie sana kwenye karatasi hii maalum ya ukaguzi (auction sheet) kabla ya kununua gari iwe unalinunulia hapahapa Tanzania au umeliagiza Japan ambapo karatasi hii itakusaidia kufahamu umenunua gari likiwa katika hali gani.

1. Jambo la kwanza ni kwamba karatasi hii ( auction sheet) ina madaraja au auction grade kuanzia 0 hadi 5 zikiwa ni alama zinazokuonesha gari hilo liko vizuri kiasi gani ambapo 5 ndio alama ya juu zaidi ya ubora.

2. Kitu cha pili karatasi hii pia inaonesha grade au madaraja ya ukaguzi kuonesha hali ya ndani ya gari na hali ya nje ya gari hivyo kukupa mwanga kama utatakiwa kupita kwa Fundi rangi au Fundi wa interior.

3. Jambo la tatu ni ukaguzi wa mileage unaoonesha gari limetembea kilometa ngapi, hiki ni kipengele kingine muhimu sana unapaswa kukizingatia ili kuepuka baadhi ya Wafanyabiashara wasio waaminifu ambao huzichezea kilometa kwa kuzishusha ili kulifanya gari lionekane jipya zaidi na kumtaka Mteja alipe pesa nyingi zaidi.

4. Kipengele cha nne kinaonesha chassis number, ukubwa wa injini na kama iliwahi kubadilishwa rangi ya gari pamoja na maelezo maalum kutoka kwa Muuzaji kufafanua kama aliwahi kufanya modifications au mambo mengine.

5. kipengele cha tano ni Repair History, maelezo yanayoonesha kama gari limewahi kurekebishwa popote au kufanyiwa ukarabati bila kusahau kipengele cha Diagram, mchoro wa gari ukiwa na alama zinazoonesha sehemu zilizoharibiwa au zilizowahi kukarabatiwa ili upate mwanga.

Swali kwako uliyewahi kununua gari 'used', Je ulipewa hii karatasi na kuisoma kabla ya kulinunua ndinga lako ? YES au NO ?
FB_IMG_1709873869596.jpg
 
Swali kwako uliyewahi kununua gari 'used', Je ulipewa hii karatasi na kuisoma kabla ya kulinunua ndinga lako ? YES au NO ?View attachment 2927785
 
Sina uzoefu na magari, Ila naomba nielimishwe kuhusu gari hii Toyota Porte na Mazda Verisa. Moja wapo hasa Porte naipenda zaidi na hesabu zangu zikienda Vizuri,natarajia kuinunua. Je,Kwa Tanzania niandae bei gani mpaka inifikie mikononi,vile vile Kwa kuagiza Japan itakua bei gani.
Mawazo yenu ni muhimu sana kwangu.
 
Kwa Porte achana nayo labda kama huna mizunguko mingi
 
Back
Top Bottom