Hakika huyu mzee atakumbukwa kwa mengi haswa kwenye utumishi wa umma alio hudumu kwa kipindi chote.
Kila alipokua kwenye nafasi fulani huko aliacha alama ya mfano, mtu mwenye udhubutu na maono ya mbali asie kubali kushindwa katika kile alichoona kinawezekana.
Ni bahati mbaya kidogo katika nafasi ya urais alipata doa ! Labda kwa vile hio kazi ya urais sio ndogo na inajumuisha mambo mengi hivyo mengine yalimwangusha Kama yalivyotokea kwa wengine.
Au labda alidhani namna ya kuongoza katika nafasi fulani Kama wizara Ni sawa na kuongoza katika urais hii ikapelekea kupata matokeo hafifu.
Sio wote walioweza kuona mwenendo wake ule wa uongozi kwamba ulikua unaelekea kubaya, Bali wengi waliona yupo sawa na no Bora kuliko wengi!
Mpaka anafariki ukweli ulikua unabaki kwamba angetuacha vibaya Kama taifa kipindi ambacho angetoka madarakani, lakini inabaki kua alikua Ni rais mwenye mema yake mengi Sana lakini katika mema mengi yale kulikuako na mwambato wa ubaya, kuliko pelekea kuonekana Ni mbaya moja kwa moja kwa walio wengi.
Mungu amjalie kuupata uzima wa milele.
Sent using
Jamii Forums mobile app