Mada maalumu ya picha za watu maarufu waliowahi kuwepo na waliopo duniani

Mada maalumu ya picha za watu maarufu waliowahi kuwepo na waliopo duniani

Mehmet Ali agca raia wa uturuki Alie kua na kusudia la kumuua kiongozi wa kanisa katoliki dunia pope John 2.
Ingawa Papa aliweza kumsamehe na mahakama pia ilimuachia huru kutoka kifungo Cha maisha, Ila haijajulikana haswa Ni kwa sababu gani alikua na kusudi lile au Ni Nani Alie mtuma!
EY8MgqlXYAEhSjU.jpg
 
Nadhani hakuweza kufariki kwa tukio Hilo Bali alifariki 1919 miaka 8 baadae.
Kwa kipindi hiko na pengine hata Sasa ni rais wa marekani alipata kushika madaraka akiwa na umri mdogo miaka 42.
Kwani Obama aliingia na miaka mingap?
 
Bi condoleezza Rice aliwahi kuwa mwanamke maarufu akiwa kiongozi wa wizara ya nje ya marekani. Akiwa Ni mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Africa kushika wadhifa huo. View attachment 1796689
Code name ya Wali nyumbani hiyo..Leo jioni mwala chakula gani😀😀😀utasikia Condoleesa.Maisha yanaenda kwa kasi.
 
Nipo naangalia series ya Narcos inayohusu maisha ya Pablo Escobar, japo alikua muhalifu ila hua namuAdmire sana. Moja ya kitu alichonifurahisha ni kupiga hii picha mbele ya ikulu ya marekani akiwa na mwanae wakati huo anatafutwa balaa. Hakuishia hapo aliipeleka familia yake kwenye kituo cha Disneyland marekani kula bata
View attachment 1797542

Jamaa alikuwa smart sana
Namkubali sana na documentary zaidi nimeangalia sana
 
Oscar Leonard Carl Pistorius. South African former professional sprinter.
At the 2011 World Championships in Athletics, Pistorius was the first amputee to win a non-disabled world track medal.
At the 2012 Summer Olympic Games, Pistorius was the first double-leg amputee participant.
View attachment 1795549
Hivi huyu jamaa ilikuwaje mpaka akakatwa miguu yote miwili?
 
Fidel Castro. Aliekuwa Rais wa Cuba kwa miaka 49 kuanzia mwaka 1959 mpaka 2008. Katika kipindi hicho chote Marekani ilitawaliwa na Marais 10.

Ni maarufu kwa speech ndefu duniani moja wapo ikiwa ni ile ya zaidi ya masaa 7 mwaka 1986 akihutubia chama cha kikomunisti jijini Havana.
ratio3x2_700.jpg
 
images (7).jpeg
images (5).jpeg

Ernesto Che Guevara, Muargentina alieshiriki katika mapinduzi ya Cuba akiwa na Fidel Castro.

Alikuwa ni daktari, kiongozi wa vita vya misituni (guerrilla wars) waziri wa viwanda Cuba. Aliwawa nchini Bolivia mwaka 1967 na jeshi la nchi hiyo wakishirikiana na CIA baada ya kuhamasisha mapinduzi yaliyoshindikana.


Anachukuliwa kama alama ya mapinduzi popote duniani.
 
images (8).jpeg

Patrice Lumumba ni waziri mkuu wa kwanza wa Jamuhuru ya Kidemokrasia ya Kongo. Inasadikika kuwa alikuwa na misimamo ya kikomunisti/kijamaa na hivyo kuonekana kuwa tishio kwa mataifa ya Magharibi.

Alikuwa waziri mkuu kuanzia mwezi June mpaka Septemba 1960 na kulazimika kukimbilia mafichoni ambapo aliuwawa Januari 17, 1961 akiwa na umri wa miaka 35 tu, na wapinzani wake (Mobutu) wakishirikiana na CIA bamoja na serikali ya Ubelgiji.
 
images (12).jpeg

Edward Moringe Sokoine alikuwa mwanasiasa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili tofauti.

(1) Kuanzia13 Februari 1977 mpaka 7 Novemba 1980
(2) 24 Februari 1983 mpaka 12 Aprili 1984.


Sokoine alifariki dunia Aprili 12, 1984 saa 10 jioni wakati akitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam baada ya gari yake kupata ajali kwa kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na mkimbizi kutoka Afrika Kusini aliyejulikana kwa jina la Dube.
Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Wami Dakawa, sasa Wami Sokoine kilichoko umbali wa kilometa 40 kabla ya kufika Morogoro Mjini.

Inasemekana kwamba, baada ya kikao cha NEC, karibu viongozi wakubwa wa kitaifa waliondoka mjini Dodoma kwa ndege, lakini yeye akasema wazi kuwa ni muumini wa sera ya kilimo ni uti wa mgongo wa taifa, hivyo alipendekeza kusafiri kwa njia ya barabara. Lengo lake lilikuwa ni kujionea mashamba makubwa na maendeleo ya kilimo kwa ujumla wakati akipita barabarani.
 
Back
Top Bottom