View attachment 1798723View attachment 1798724
Julius Caesar maarufu kama Kaisari alikuwa ni mtawala wa kisiasa na kijeshi enzi za Warumi.
Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo.
Baadhi ya mafanikio hayo ni:
1.Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa na lugha nyingi kama Kireno, Kihispanyola n.k (kwa ujumla wake huitwa Romace languages) ni lugha zenye ukaribu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale.
2.Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu.
Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani).
3. Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai.
4.Katika historia ya Roma yee ndie aliepelekea kufa kwa Jamhuri ya Roma (Roman Republic) na kuzaliwa Dola la Roma (Roman Empire) aliloliwekea misingi na lililotawala sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Asia kwa miongo mingi.
Moja ya misemo (quotes) maarufu ya Kaisari ni pamoja na "Veni, Vidi, Vici" kwa Kiingereza "I came, I saw, I concured" kiswahili "Nilikuja, Nikaona, Nikashinda" huu msemo aliutumia katika ripoti yake ya vita baada ya kushinda vita iliyomchukua muda mfupi dhidi ya Pharnaces II wa Pontus.