Nyumba hajawahi jengwa kirahisi hivyo labda kama unajenga kibanda
Wasiokunywa kabisa wanaitwa 'Tea-totaller' (yaani chai tu), lakini inatamkwa 'teetotaller' .
Hebu waulize hao wagidaji wanapata faida gani mbali na kujisikia 'kuchangamka' halafu kulewa, halafu kupata 'ajali' (ya 'kugonga' demu mwenye virusi bila kinga shauri ya ulevi) au kugonga gari (kwa ajali inayosababishwa na ulevi}?
Hebu nikuulize wewe mlevi:- Je, umewahi kupiga hesabu ya kiasi cha pombe unachokunywa kwa mwezi mmoa tu? Nakuhakikishia, ukiwa unaandika idadi ya bia unazokunywa kila siku, ukatafuta idadi na gharama yake kwa mwezi, utashituka. Gharama inaongezeka sana kama utakuwa unachukua demu kwenda ku-enjoy nae. Ukipiga hesabu, utatambua kwamba ndani ya miezi sita ungekuwa na hela ya kununua kiwanja. Miezi sita ingine, ungeweka msingi. Mwaka unaofuata ungepandisha mpaka lenta na kupaua. Mwaka unaofuata ungemalizia na kuhamia.