MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Je hapo unapoishi kuna watoto wengine? ikiwa hakuna watoto wengine waweza kuwa sababu .....
 
Dah! Najua unakosa raha na kujisikia mnyonge pole sana. Mi ka kwangu ka kike miaka miwili lakini kanacharaza maneno hatari ila nami nilikosa raha kipindi kalipochelewa kutembea.
 
Pole Mpwa wangu, wangu ana 2.9yrs bado hajanyoosha maneno japo yeye anaelewa kila kitu, nadhani ni muda tu
 
Thanks @Honey Faith, ni kweli, mtoto wangu pia mara nyingi alikuwa anapenda sana kucheza peke yake, hata ukimchanganya na wenzake bado anapenda kuwa na michezo yake tofauti. Siku hizi kidogo kidogo ameanza kujichanganya na watoto wenzie lakini bado haijasaidia.
Hivi ndivyo alivyokua mwanangu, naye alichelewa kuongea tena alikua hajichanganyi na watoto wengine. Hata ukimuweka kwenye kundi la watoto baada ya muda alikua anajitenga.

Sasa hivi yuko std 5 anaongea lakini bado ana tabia za pekee. Hebu jaribu kumuangalia ulimi wake yaani chini ya ulimi kukoje. Wakati mwingine waweza kuta ulimi umeshikiliwa na kinyama/ sijui kinaitwa tongue tie .
 
Poleni sana, hakikisheni anakuwa muda mrefu na watoto wenzie na hata kama mnaweza kuwaomba hao watoto muda mwingi wajaribu kumuongelesha labda inaweza kusaidia naye akaanza kuongea. Hakikisheni pia hana matatizo ya ukiziwi. Kila la heri.
 
Rafiki hebu fafanua hapo kwenye rangi. Hiki kinyama kinaweza kuondolewa na Wataalamu? Maana kucheza na ulimi si kitu kidogo kama kutakuwa na makosa.

Hivi ndivyo alivyokua mwanangu nae alichelewa kuongea tena alikua hajichanganyi na watoto wengine hata ukimuweka kwenye kundi la watoto baada ya muda alikua anajitenga. Sasa hivi yuko std 5 anaongea lkn bado ana tabia za pekee. Hebu jaribu kumuangalia ulimi wake yaani chini ya ulimi kukoje. Wakati mwingine waweza kuta ulimi umeshikiliwa na kinyama/sijui kinaitwa tongue tie .
 
Kwa dalili unazosema, anaweza kuwa na social and communication difficulty, possibly Autism. Autism iko katika aina tofauti, check na pediatrician (doctor wa watoto) anaweza kukushauri nini cha kufanya. The earlier the better.
 
Kama alivyochangia hapo Ablessed mtimzame vizuri hususan akilia ulimi ananyanyua kwa chini au haunyanyuki? Ukiona haunyanyuki na kuna ki nyuzi basi niutata (tongue-tie)
 
Last edited by a moderator:
Pia nimewah skia kahawa inawafanya watoto kuongea haraka yaani una mnywesha kidogo ila sikushauri lakini labda wataalamu waje watuthibitishie
 
Muache mtto acheze na wenzake mkuu
 
Rafiki hebu fafanua hapo kwenye rangi. Hiki kinyama kinaweza kuondolewa na Wataalamu? Maana kucheza na ulimi si kitu kidogo kama kutakuwa na makosa.
Ndio hicho kingozi wataalamu wanakiondoa . Hapo ninaposema ana tabia za pekee namaanisha bado si mtu wa kujichanganya sana na wataalamu waliniambia kuna watoto wako hivyo so nisiwe na wasi wasi. Wataalam namaanisha madaktari usije ukafikiri nazungumzia waganga wa kienyeji (just kidding lol)
 
Ahsante sana rafiki, lol!!! hahahahaha wala sikudhani wataalamu unaozungumzia ni hao wa ndumba na ngaye lol!!!

Back
Top Bottom