Tetesi: Madai kuhusu Commodity Import Task Force iliyoundwa kukusanya fedha za Serikali ya Japan na vigogo wanaohusishwa ni ya kweli?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kuna taarifa inasambaa mitandaoni tangu jana kuhusu hiyo task force inayodaiwa kuundwa kwa lengo la kukusanya fedha za serikali ya Japan zinazohusiana na Commodity Import Support.

Mtoa taarifa, mbali na kutaja watu anaowatuhumu, ameweka mpaka demand notice jambo linalonifanya nijuilize maswali mengi zaidi kwani inaleta picha/hisia kuwa hizo document huenda amepewa na wahanga wa hili jambo au watu wengine wasiopendezwa na mambo haya.

Kwakuwa sijui ukweli wa madai haya yaliyotolewa na yule whistleblower maarufu, sitaeleze tuhuma husika wala kutaja wanaotuhumiwa, ila natarajia wenye dhamana au watuhumiwa kujitokeza hadharani ama kukanusha au kutoa ufafanuzi.

Vile vile nasubiri neno kutoka kwa wamiliki wa akaunti zilizotajwa na pia mabenki husika kutoa ufafanuzi wa hizo akaunti.

Kama tuhuma hizi na zingineni zinazoibuka hivi sasa na kuandikwa mitandaoni na huyu whistleblower ni za kweli, basi naanza kupata wasiwasi na mashaka kama Mama yetu ataiweza vita aliyoianza au itabidi afunike kombe kunusuru baadhi ya watu.

Time will tell.
 
Kuna taarifa inasambaa mitandaoni tangu jana kuhusu hiyo task force inayodaiwa kuundwa kwa lengo la kukusanya fedha za serikali ya Japan zinazohusiana na Commodity Import Support.

Kwakuwa sijui ukweli wa madai haya yaliyotolewa na yule whistleblower maarufu, sitaeleze tuhuma husika wala kutaja wanaotuhumiwa, ila natarajia wenye dhamana au watuhumiwa kujitokeza hadharani ama kukanusha au kutoa ufafanuzi.

Vile vile nasubiri neno kutoka kwa wamiliki wa akaunti zilizotajwa na pia mabenki husika kutoa ufafanuzi wa hizo akaunti.

Kama tuhuma hizi na zingineni zinazoibuka hivi sasa na kuandikwa mitandaoni na huyu whistleblower ni za kweli, basi naanza kupata wasiwasi na mashaka kama Mama yetu ataiweza vita aliyoianza au itabidi afunike kombe kunusuru baadhi ya watu.

Time will tell.
Tumwagie taarifa iliyoshiba ili nasi tujuwe mbivu mbichi.
 
Nasubiri ukweli ndio nitie neno mkuu. Kwa jambo nisilolijua mimi huwa sikurupuki kama wewe
Na kuabudu anaabudiwa Mungu sio mtu
Sawa eee?
Mama d mama yangu dada yangu mdogo wngu nchi hii upigaji unakwenda kwa awamu
Kila awamu ikingia lazima kuna watu watafaidika nayo watabebwa,na kuna wengine wataliaaa
Weka akili mwako hiyoo

Ova
 
Tulishuhudia wakati wa Mkapa waliokua na Mwinyi wakilia
Tukashuhudia wakati wa JK wa mkapa wakilia
Wakati JPM wa JK walilia
Na sasa kwa SSH tutashuhudia wa JPM wakilia

Kibaya wanaokua kwenye hizo nafasi huwa hawawazi huu mwisho😅😅
 
Back
Top Bottom