Madai kwamba Magufuli alimpiga Ben Saanane risasi pale Ikulu isichukiliwe kihisia; hizi hapa ni sababu za msingi kuamini kwamba ni ukweli

AKIKATAA KUA HAKUTAKA KUBAKWA KABENDERA ATASEMAJE? UNAFIKIRI SSH ANAWEZA KUKUBALI UJINGA KAMA HUO ?KABENDELA DISH LIMEYUMBA
Mimi ninachotaka ni watu wahojiwe mahakamani, kwa kutumia standards za kimahakama, chini ya kiapo.

Akikataa, akikubali, sina tatizo mradi maongezi ya mahakamani yatatupa nafasi ya kusikia maneno kutoka kwenye cross examination.

Kwani wapi nilikwambia Samia lazima atakubali.

Kama Samia ataweza kutuonesha kuwa Kabendera ni muongo, hilo litakuwa jambo zuri, tutajua ukweli.

Na hapo ndipo umuhimu wa kumshitaki Kabendera unapokuja, tutapata kusikia upande tofauti na Kabendera ukitolewa mahakamani.

Bila kumshitaki Kabendera hatutapata mazungumzo hayo.
 
Kwahiyo na soka naye anaweza kuwa kafanyiwa hivyo hivyo😓😓
Ile ya Ben saanane ilikuwa ya Magufuli ya soka atahusika mama maana huko mbele tutapata mwandishi mwingine atatueleza kwa namna gani mama alimpiga risasi soka pale ikulu wakati utaongea maana Kabendela ni chombo cha usalama na kinatoa taarifa.
 
Hopeless kabisa.....ila sio mbaya maana jf ni jukwaa huru hata ukiamua kutoa utumbo unatoa tu.
 
Nawe
Nawe chukua fursa hii kuchunguza na kuandika kitabu Cha Hawa waliopotea 2024

Unafikiri kwa sababu unaandika JF ndio unaweza kuandika kila kitu hata usichokijua wala kukifanyia kazi? Uandishi wa uchunguzi una mambo mengi na ya hatari sana.
Usije kuwa umekunywa zako wanzuki unajipa moyo unaweza kuandika. Ni shughuli pevu sana.
 
Hizi kwamba zimekuwa nyingi, ni kama stori za koridon…… hakuna solid evidence presented. Hizi story zipo hapa JF way back ….. zimebaki kama udaki. Kitabu cha kabebdera pia hakuna solid evidence

Kuamini hizo story kunahitaji Iman na imani ni personal

Tunahitaji solid evidence
 
Kama unaamini kitabu kama kile kilipaswa kuweka evidence basi wewe sio msomi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…