Madai ya kukosekana Mochwari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, uongozi wasema fedha imetengwa kujenga jengo hilo

Madai ya kukosekana Mochwari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, uongozi wasema fedha imetengwa kujenga jengo hilo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-05-25 at 22.17.28 (1).jpeg

TAARIFA KWA UMMA​
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi umeona taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu changamoto ya ukosefu wa Mochwari katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Hoja ya Mdau ~ Milioni 100+ zinatumika kununua gari la ‘staff’ Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi wakati hospitali haina mochwari

Hospitali hii bado mpya na inaendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali, bado majengo mengine hayajakamilika. Aidha, changamoto hii tayari Serikali ilishaipa kipaumbele ambapo kwa Bajeti 2026/2027 imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa la kuhifadhia maiti lenye hadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Hata hivyo, Hospitali imetenga chumba maalumu cha kuhifadhia mwili kwa muda wakati taratibu za kusafirisha kwenda Hospitali ya Manispaa ya Mpanda zikiendelea.

Aidha, taratibu zote za kusafirisha mwili zinaratibiwa na kusimamiwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO KWA UMMA
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA KATAVI
25/5/2026
 
Back
Top Bottom