agudev
Member
- Apr 5, 2016
- 80
- 128
Hili swali nimekuwa nikijiuliza bila kuelewa, nimekuwa nikisikia majibu kama chumvi mbichi na chumvi iliyoiva, sielewi ni namna gani chumvi inaitwa imeiva wakati yenyewe ni kemikali.
Tuchukulie mifano hii:
Je, kuna tofauti gani kati ya mapishi haya mawili ikiwa kiasi sawa cha chumvi kimewekwa kote na kimesabaa kwa uwiano sawia?
Tuchukulie mifano hii:
- Nimepika maharage kilo moja bila kutia chumvi halafu nikaja kuongeza vijiko vitatu vya chumvi baada ya maharage kuiva na kuiacha kwa muda ili chumvi iyeyuke na kuenea kwenye maharage
- Nimepika maharage kilo moja na kuongeza chumvi vijiko vitatu nikaacha viive kwa pamoja
Je, kuna tofauti gani kati ya mapishi haya mawili ikiwa kiasi sawa cha chumvi kimewekwa kote na kimesabaa kwa uwiano sawia?