Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

povu la nini idara nyingine wakiwa field wanalipwa?? tena bora mmepewa chakula na malazi
Nimegundua kuna watu mnachangia hii mada ila either hamuelewi tofauti ya field na intern au mnafikiria kwa kutumia makalio, nahisi hata hao wakubwa zenu waliotoa wazo hili hawaelewi maana ya intern doctor.
 
Sikujua km kujitegemea ni kuwaumiza watu wa hali ya chini kwa kuwanyima mahitaj yao ya msingi huku wengine wakiendelea kuogelea kweny ukwasi. Wakuu wa wilaya wamekuw retained licha ya kuonekan ni vyeo visivyo na umuhim mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Wanatembelea ma vx v8 kwa kodi hiyo hiyo tunayosema tunataka kubana matumizi. Unataka kumnyang'anya intern anayefanya kazi kama punda kile kidogo anachokipata kwa kisingizio cha kubana matumizi ili kumtengenezea msongo wa mawazo anyway nyinyi na familia zenu mkiugua hamtibiwi hospital za umma ndio maana unaongea ukitawaliwa na wivu.
Kama ni kweli mi inaniuma sana aisee hata sielewe tunakoelekea Ila tumwachie MUNGU maana sasa unafiki umetamalaki[emoji34]
 
Soon watu watakuwa wanakufa taratibu tu kumbe mmewaudhi Madaktari. Mtachomwa sindano za sumu bure, kila siku mnashughulika na Madaktari tu hakuna watumishi wengine?
 
Kama mihimili ya dola haidhibitiani,haya ndio matokeo yake
 
Kwani walimu wanafunzi wakiwa field huwa wanalipwa 80% ya mshahara? If no why to doctors? Ifike mahala pasitokee watu kujifanya wao ni peculiar kuliko wengine.

Posho zote Magufuli afute hata za Maaskari kuondoa matabaka na minong'ono kwa watumishi wengine wa umma,
Nina mashaka na Wewe kama ata shule ulienda walimu wote wanapoenda field kila mwisho wa mwaka wa masomo hupewa pesa kiasi cha 620000/= kila mmoja. Hivyo hivyo kwa madaktari wanapokua chuo wanapoenda field hupewa pesa kiasi hicho hicho na hii ni kwa kozi zote kwa mtu ambae amepewa mkopo na loans board hupewa hiyo pesa kila mwisho wa mwaka wa masomo kwa madaktari wao huanza kupewa hiyo pesa ya field mwaka wa tatu.
Lakini tunapokuja kwenye swala la internship ni tofauti kabisa na field maana yake ni mafunzo kazini kimsingi unakua ushamaliza chuo na unatakiwa kuajiliwa na ktk kada ya udaktari huwez kuajiriwa bila kupitia intern kwa sheria za udaktari huwez ruhusiwa kufanya kazi bila kuwa na leseni kutoka bodi ya madaktari ambayo hutoa leseni mpaka utakapo maliza intern. Hii ni tofauti kabisa na ualimu unaoulinganisha na udaktari.

Naruhusu kurekebishwa
 
Natamani MaDaktari wawe wanaajiriwa kwenye NGOs kwa kibali maalum toka kwa katibu mkuu kiongozi and ofcourse ndiyo mapendekezo tuliyoyapeleka.
Zoezi hill liende sambamba na kuhakiki wale waliopo kwenye hizo NGOs.
Inabidi Madaktari wasambazwe had I ngazi vituo vya afya na ikibidi kwenye zahanati ambazo ni high volumes.
Unakuta MD mzima yupo kukusanya data tu kwenye hizo NGOs na kuwapa wengine wakazisome na Ku evaluate n.k.
Ficha upumbavu wako,yani mtu asome miaka mi5 bado umpangie sehem ya kufanya kazi? Tumia akil yako kufikiri.
 
Wengine wanasema eti 'entertainment ' ....!

Watanzania tuanze kuamini katika kujitegemea...kujitegemea hakuwezi kuja kirahisi. Lazima tubane matumizi...na ukiona unaumia kwa kubana matumizi ujue wewe ni mtu muhimu katika nchi hii maana unaitengeneza Tanzania ya kwako, ya watoto wako na vizazi vijavyo ambayo itakuwa inajitegemea kiuchumi na kijamii. Hatutahitaji tena misaada yenye masharti ya kutudhalilisha na kututaka tufanye ushetani.

Watanzania tumuunge mkono rais kwa kila hatua anayoifanya kuelekea kutengeneza Tanzania imara, inayojitegemea kiuchumi na kijamii. Tunaweza tusikatishwe tamaa.
Ahahaha nani amekuambia kuna nchi inayojitegemea bila kukopa? Yani mtu asome miaka mitano halafu afanye kazi bila ya kupewa posho? Acha utani na maisha ya watu.
 
Eeee "wasilipwe tu maana "hatuwataki"" sisi tunataka kazi tu....
 
Kuna tetesi kuwa serikali imekusudia kufuta posho za madaktari wa mazoezi (Interns) kuanzia madaktari wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu. Katika utaratibu huo mpya madaktari wa mazoezi watapewa nyumba na chakula katika hospitali watakazoenda kufanyia kazi (Internship) lakini hawatakua na posho yoyote ya kujikimu.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kuwalipa madaktari hao, ambazo hazilipiwi kodi.!
Hii ni taarifa ngumu kwa jamii ya Tanzania wengi wana kumbuka maafa yanayotokana na madai ya stahiki za hawa jamaa!
Labda mtoa mada ulete source ya habari hii tusije kutokwa na povu la mdomo kumbe ni tetesi tu!
 
Ila hizi ni tetesi,kwanini GT tuko busy kujadili tetesi
 
Acha ujinga wewe ndorobo.hivi huyu intern doc anayefanyia mafunzo mbeya wakati yeye ni wa kigoma akimaliza mafunzo arudije kwao???akiugua na si madawa yote yanapatikana hosp za serikali nani atanunua hzo dawa,na pesa ya vocha ya kuwasiliana na seniors wake pindi ahitajipo msaada wa kiutendaji nani ampe acha kutumia kiuno kufikiria kaka
Kuhusu kuugua; Serikali inaweza kuwadhamini kujiunga na NHIF; kuhusu vocha serikali inaweza kuwaruhusu kutumia simu za ofisi ama za majumbani watakapokuwa wanakaa kwa utaratibu maalum..kumbuka internship haina likizo..;....: Wewe majibu hayo yanakutosha ingawa unajitahidi sana kutumia lugha ya kuudhi.
Sikujua km kujitegemea ni kuwaumiza watu wa hali ya chini kwa kuwanyima mahitaj yao ya msingi huku wengine wakiendelea kuogelea kweny ukwasi. Wakuu wa wilaya wamekuw retained licha ya kuonekan ni vyeo visivyo na umuhim mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Wanatembelea ma vx v8 kwa kodi hiyo hiyo tunayosema tunataka kubana matumizi. Unataka kumnyang'anya intern anayefanya kazi kama punda kile kidogo anachokipata kwa kisingizio cha kubana matumizi ili kumtengenezea msongo wa mawazo anyway nyinyi na familia zenu mkiugua hamtibiwi hospital za umma ndio maana unaongea ukitawaliwa na wivu.
Hawa wakuu wa wilaya wapo kisheria/kikatiba. Lazima ubadili hivi vitu ndiyo utaweza kuondoa nafasi hizi. Tumia utaratibu uliowekwa kurekebisha hili ndipo VX v8 za wakuu wa wilaya zitapotea. Ni makosa kusema intern anafanya kazi kama punda, pale anakuwa kwenye mafunzo ya kusaka uzoefu. Hilo ndilo hasa lengo la internship ndio maana kunakuwa na seniors kumuelekeza. Kwa maneno mengine anakuwa bado mwanafunzi. Au unataka serikali impe na mkopo wa kufanya interns? Sikuelewi ujue!?
mkuu hatuna sheria za kulinda haya, leo hii tuna sacrifice anakuja mwengine kesho anaanza mengine upya.
Hiki hasa ndicho cha kufanyia kazi...watu badala kuhimiza jambo la kuhakikisha mfumo unaimarishwa wao wako kwenye kutumia lugha chafu, kujadili wateuliwa, wanakimbia sehemu muhimu za kufanya maamuzi n.k
Kwanini walikuwa wanapewa boom walipokuwa Muhas il-hali kulikuwa na hostels? Mahitaji ya mtu mzima si accomodation na chakula tu. Madaktari interns wa kike hospitali zitakuwa zinawapa pedi na pesa za kusuka nywele?
Haya yote yanazungumzika tena kwa lugha ya staha...ni kiasi cha kujenga hoja. Serikali ina nia njema na watanzania.
 
Nimegundua kuna watu mnachangia hii mada ila either hamuelewi tofauti ya field na intern au mnafikiria kwa kutumia makalio, nahisi hata hao wakubwa zenu waliotoa wazo hili hawaelewi maana ya intern doctor.

we hutumii makalio utawalipa endapo itakaatwa
 
Huyu jamaa bana no wonder sikumpigia kura and never will I,ndo nini hiki
 
Ahahaha nani amekuambia kuna nchi inayojitegemea bila kukopa? Yani mtu asome miaka mitano halafu afanye kazi bila ya kupewa posho? Acha utani na maisha ya watu.
intern wanachokifanya kinaelekea kuwa na kile cha graduate wa sheria, au engineers wanaotaka 'uprofessional'. Kudhibitisha kuwa umeiva katika fani...! Ni kweli unakuwa unafanyakazi lakini katika usimamizi ...!!
 
Mbona madactar wameandamwa sana kwani secta zingine hazipo? Mbona hatusikii wakasema wanajeshi?
Wanajeshi hawana kazi hata kwny usafiri wa umma wanatembea bure ila hawaguswi,udaktari ni very sensitive aisee, tutatibiwa na nani
 
intern wanachokifanya kinaelekea kuwa na kile cha graduate wa sheria, au engineers wanaotaka 'uprofessional'. Kudhibitisha kuwa umeiva katika fani...! Ni kweli unakuwa unafanyakazi lakini katika usimamizi ...!!
Kwahiyo wasipewe posho?
 
Back
Top Bottom