Wengine wanasema eti 'entertainment ' ....!
Watanzania tuanze kuamini katika kujitegemea...kujitegemea hakuwezi kuja kirahisi. Lazima tubane matumizi...na ukiona unaumia kwa kubana matumizi ujue wewe ni mtu muhimu katika nchi hii maana unaitengeneza Tanzania ya kwako, ya watoto wako na vizazi vijavyo ambayo itakuwa inajitegemea kiuchumi na kijamii. Hatutahitaji tena misaada yenye masharti ya kutudhalilisha na kututaka tufanye ushetani.
Watanzania tumuunge mkono rais kwa kila hatua anayoifanya kuelekea kutengeneza Tanzania imara, inayojitegemea kiuchumi na kijamii. Tunaweza tusikatishwe tamaa.