Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

Hongera mkuu wa Kaya kwa maamuzi sahihi,hawa madaktari wanafunzi wanapewa fedha zisizo na idadi na wanazifuja kwa wanawake na starehe zisizo na tija kwa taifa
 
Lazima mtu anywe uji wa mgonjwa hapo...
 
Hongera mkuu wa Kaya kwa maamuzi sahihi,hawa madaktari wanafunzi wanapewa fedha zisizo na idadi na wanazifuja kwa wanawake na starehe zisizo na tija kwa taifa
We mburura Wewe unafikiri kusoma medicine ni kama kusoma human resource , lazima serikali iweke motivation watu wasome hizo kozi nakuhakikishia watu watasoma na madegree yao watakaa na vyeti Gheto alaff watafte ajira mbadala
 
Kuna kabila ni maarufu kwa ubahiri. Mtu hulala na njaa ukimsachi ana fedha kibao. Unabana matumizi ili hizo hela ufanyie nn. Mie nilidhani matumizi yenyewe ndio hayo
Napendekeza Rais ateuwe wakinga kwenye wizara ya fedha.
 
Mahitaji ni chakula na mahali pa kulala?
Wengine wanasema eti 'entertainment ' ....!

Watanzania tuanze kuamini katika kujitegemea...kujitegemea hakuwezi kuja kirahisi. Lazima tubane matumizi...na ukiona unaumia kwa kubana matumizi ujue wewe ni mtu muhimu katika nchi hii maana unaitengeneza Tanzania ya kwako, ya watoto wako na vizazi vijavyo ambayo itakuwa inajitegemea kiuchumi na kijamii. Hatutahitaji tena misaada yenye masharti ya kutudhalilisha na kututaka tufanye ushetani.

Watanzania tumuunge mkono rais kwa kila hatua anayoifanya kuelekea kutengeneza Tanzania imara, inayojitegemea kiuchumi na kijamii. Tunaweza tusikatishwe tamaa.
 
Hili naliona likija kwa serikali hii...mana product inayotoka vyuoni sasa hvi ni kubwa mno
Tofauti na zamani, na tuko kwenye sera ya kubana matumizi hakyani watakiona nasema
 
Mimi siamini kama anajua kuwa Kuna Mkurugenzi kateuliwa akiwa amefukuzwa chuo cha TIA kwa sababu ya uzembe na kukosa maadili. Huyo Bwana aligombea ubunge Kwa Kangi Lugora na amepangiwa kuwa mkurugenzi Wa Wilaya ya Hai.
Pia kuna wakurugenzi wa zamani ambao wamebakizwa ambao utendaji wao ni wa mashaka kuliko hata baadhi ya walioachwa.
Rais amesema anachagua watu kumsaidia kutengeneza Tanzania anayoitaka yeye .......... probably haitakuwa ile tunayoitaka sisi!! Kwa hiyo pale unapofikiri amekosea inawezekama kabisa hakukosea!!
 
Lazima uwe chizi ama kuamini hili au kufanya hili.
 
Sijaelewa,watakuwa wanapikiwa au? Kwa hiyo wao watakula chakula cha Hospitalini. Hahahhaa!

Kwani hizo posho zilikuwa za kazi gani kama siyo kwa ajili ya chakula na gharama zingine zikiwepo kulipia kodi kwa kipindi wawapo internship?
Labda wataalisha chakula cha wagonjwa...au watawaruhusu wawe wanaomba CCD
 
Kuna tetesi kuwa serikali imekusudia kufuta posho za madaktari wa mazoezi (Interns) kuanzia madaktari wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu. Katika utaratibu huo mpya madaktari wa mazoezi watapewa nyumba na chakula katika hospitali watakazoenda kufanyia kazi (Internship) lakini hawatakua na posho yoyote ya kujikimu.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kuwalipa madaktari hao, ambazo hazilipiwi kodi.!
watanzania wana miliki viwanda vya kutengeneza uongo- Jk
 
Huyu Jamaa Sasa Nahisi Anataka Kuleta Migomo Isiyo na Maana
 
Demand ya mamedical personels mtaani ni kubwa sasa huo utaratibu wa kupitia kwa katibu mkuu huoni utachelewesha watu kuanza kazi na vp mtu akinyimwa hivyo vibali?
Ikitokea amenyimwa kibali atapangiwa hospital au kituo cha afya kwa kadili ya mapengo yaliyopo au ataendelea kubaki alipo.
Unajua mkuu, nimekubaliana na rais kwamba hii nchi inahitaji kupelekwa ki 'kwatakwata' tu.
 
Unabana posho za intern halafu unalipa wabunge sitting allowances!!

Ni heri wangewapatia na amount Fulani pamoja na hiyo nyumba na chakula sababu mahitaji ni zaidi ya hayo.
 
Kuna tetesi kuwa serikali imekusudia kufuta posho za madaktari wa mazoezi (Interns) kuanzia madaktari wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu. Katika utaratibu huo mpya madaktari wa mazoezi watapewa nyumba na chakula katika hospitali watakazoenda kufanyia kazi (Internship) lakini hawatakua na posho yoyote ya kujikimu.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kuwalipa madaktari hao, ambazo hazilipiwi kodi.!
Hao madakitari watapata wapi dawa ya mswaki, sabuni na usafiri wa dart?
 
Hivi hawa jamaa wanafikiri maisha ni nyumba na chakula tu..!? waandae mortuary za kutosha
 
Back
Top Bottom