Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia

MCT washikilie hapohapo.wakikubali kuingiza siasa tutakuwa na madaktari wa mchongo kama wanasheria wamchongo waliopo serikalini wanaotetea mkataba wa kihuni kati ya Tanganyika na dp world.
Ndugu yako aliyesoma miaka mitano kwa garama kubwa kutoka kwa mama/baba masikini akikwamishwa kupata Leseni ajiajiri/aajiriwe ndo utakuja kujua uchungu wake,maumivu wanayoyapitia hawa madogo ni maumivu makali sana,ni Bora kukaa kimya kuliko kuwakatisha tamaa,Dunia duara.
 
MCT washikilie hapohapo.wakikubali kuingiza siasa tutakuwa na madaktari wa mchongo kama wanasheria wamchongo waliopo serikalini wanaotetea mkataba wa kihuni kati ya Tanganyika na dp world.
Yule Feleshi sio kwamba hana akili kichwani au haelewi kuhusu huo mkataba, tatizo keshakula pesa ya mwarabu, hivyo inabidi aweke pembeni all reasoning na kuwa kama taahira hivi
 
Kwanza poleni kwa changamoto.

Pili siungi mkono kwenye wazo lako la kufuta huo mtihani kabisa kama ulivyodai , maana ninavyofahamu medical student yoyote ni lifelong learner ndio maana kunakuwepo na CPD.

Ushauri wangu ni uwepo utaratibu mzuri kuanzia setters , moderators , markers , final verifiers kila ngazi wawepo watu tofauti mtu asijirudie kwa huo mtihani kuondoa hizo rafu ambazo kweli zinaweza kuwa za kibinadamu au kwa makusudi.

Mitihani iko kwa kada zote za medical duniani wakishindwa waje wajifunze kwa wenzetu huku wa USMLE ambao una step 1 hadi 3 ambayo iko vizuri na ukipass umepass kweli na inafanyika online katika centers zinazotambulika.
 
Mtu mmoja, nafikiri ni Hitler, alipoulizwa kitu anachokiogopa maishani, alisema HAOGOPI CHOCHOTE ISIPOKUWA MITIHANI.

Mitihani si kigezo pekee cha kubaini uwezo wa mtu kitaaluma kwa sababu zifuatazo:
1. Mtahiniwa anaweza akapanick siku ya mitihani hivyo kupelekea kujibu ndicho sicho.

2. Kama watungaji na wasahihishaji wa mitihani ni watu wenye "roho zenye kutu", wanaweza kuwafelisha baadhi ya wanafunzi kwa makusudi. Inasemekana miaka ya nyuma, baadhi ya wahadhiri wa Vyuo Vikuu Tanzania, hasa UDSM, walikuwa wakiona fahari pale wanafunzi wengi wanapofeli masomo wanayoyafundisha.

Kwa hiyo basi, Mitihani inapaswa kuwa njia mojawapo tu ya kumtahini mwanafunzi, tena iwe ni njia ya ziada.
 
"Our aim is not to train Angeles but to minimize mistakes"
Quote ya Professor Makene (R.I.P)akiwa Dean wa faculty of medicine UDSM ..(sasa MUHAS)wakati wa orientation week 1985.
 
Ila madaktari wa siku hizi wanafikirisha sana, mtu unamwelezea matatizo yako ye yuko bize na memes
 
Kwanza walifeli Sana Wanasheria pale Law School

Sasa tunasikia Madaktari nao Wamefeli Sana

Nakumbuka zamani pale NBAA ilikuwaga Hivi Hivi ikagundulika baadae hawakutaka CPA ziwe nyingi mitaani Eti thamani itashuka😂😂

Prof Mkumbo fanya mambo utengeneze Ajjra badala ya sapo

Mungu wa mbinguni atubariki!
 
Badala ya kuomba mpaka Warusi waje kuwekeza bora wakatuma vijana hata 10,000 duniani wakajifunze kutengeneza vitu kutokana na rasilimali zetu

Dunia inasonga na nchi nyingi zinafaidika kwa rasilimali zao kwa kuzibadili kuwa hela

Sisi sijui tunawaza nini
 
13 Yyy 3r45tt
 
5
 
56
 
Wanapofanya intern wanakuwa chini ya madaktari bingwa,wananolewa na kufanyiwa assessment kila idara na wakimaliza ndo wanapewa cheti Cha intern,why wafanye Tena msqs200 za theory wakati wametoka kupractice na wamepitishwa na madaktari bingwa wanaowasimamia??
 
Hapo kwenye standardization umeharibu mzee.
 
Nimesoma kuanzia juu hadi nilipofikia hapo uliposema mitihani isahihishwe upya halafu ifanyike standardization nikaacha.

Afya ya mtu haina standardization. Tatizo vyuo vya afya siku hizi vimekuwa vingi.

Matangazo kibao ya vyuo vya afya.Utasikia chuo kipo ghorofa ya sita jengo fulani...... Kweli?
 
Kuna uhusiano mkubwa sana katika ufaulu wa Form 4 na Form 6 tena masomo ya sayansi na kuja kusomea udaktari chuoni.Udaktari aubatishwi lazima ufaulu vizuri ndio upewe cheti uthibitishe na baraza la Madaktari Tanzania.Kuwa daktari sio kubatisha.
 
Sasa kama uwezo wao ni mdogo ilikuwa wakafaulu na kupewa hizo degree?
Swali chonganishi: Ni nini hasa kilichoisukuma wizara au MCT kuanzisha mtihani huo? Kuna kitu walikihisi kuwa hakipo sawa katka fani hiyo?
Maana Magu alivifungia vyuo vingi ikiwa ni pamoja baadhi vya Udaktari kwa kuwa na viwango hafifu. Pengine Mama hataki kuvifungia ila mkajipime wenyewe kabla ya kuingia kazini.
Swali la pili chonganishi: Kati ya hao waliofeli MUHAS ni wangapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…