Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia

Ni vyema ukaweka mizaha pembeni, kada hii ni muhimu sana kama sio Leo kesho utakutana na daktari, tafuta kuelewa changamoto walizo nazo na uwasaidei kusema Ili waweze kukuza ufanisi wao kesho ukikutana nao waweze kukuhudumia vyema
Nani anaeleta mizaha? Mimi ninayeshauri wasipoteze muda wawahi VETA kusoma coursevwatakayoi mudu? Au wewe unaetaka watu waliofeli waonewe huruma na kupewa ruhusa kwenda kuchezea afya za watu?
 
piga kitabu mzee hata wao walipita huko huko
 
Sasa ndo umpime daktari kwa maswali 100 ya multiple choice??
Huo mfumo ni wa hovyo, hapo unachopima sio uelewa ila ni spidi ya kumaliza maswali 200 ya kuchagua kwa masaa 6.

Kwanini wasipewe mitihani wajieleze tu, hapo dokta anafanya ana anaa doo tu. Wanapima uwezo wa makisio
 

There is sufficient evidence showing relation between new medics including junior doctors and causes of medical error.

Hayo sio maneno yangu kuna ‘research papers’ luluki from various parts of the worlds, with better health systems; just go check on PubMed and MEDLINE.

Moreover hata hospitali zinazo record medical errors, evidence shows a majority are caused by new medics nurses/doctors. Kuna sababu luluki zinazotajwa kama chanzo cha mistake leading to medical errors; chiefly among them is lack of practice experience and fatigue.

Unatakiwa ufundishwe hilo katika masomo yako; sababu za medical errors, how to avoid them and systems in place to reduce them. Kwa sababu hilo ni tatizo kubwa duniani sio Tanzania tu linalopelekea hundred of thousand unnecessary loss of lives each year. Halafu unatuambiwa hawa watu wapewe leseni ya kufanya kazi unsupervised.
 
Haya mabaraza ya wanasheria, madaktari, wajenzi, na pia wafamasia ni ya kipigaji zaidi kuliko usimamiaji wa weledi kwenye fani hizo!! Wamejiandalia mazingira kunyonya pesa kiurahisi!! Haiwezekani baraza la mct au pct kutoa mtihani wa leseni kwa wahitimu ambao hawakuhusika kabisa katika kuwafundisha!! Wanawafelisha ili kuandaa mazingira ya rushwa, na kupiga tena pesa kupitia supplimentary exams!
Haiingi akilini daktari aliyefaulu mitihani yake chuoni na kule internship chini ya usimamizi wa maprofesa na madaktari mabingwa halafu wewe uje useme hawafai kupata leseni.

Kuhusu law school, hii shule ya sheria ndo sifuri kabisa! Badala ya kuwapima wanafunzi wao huko huko field kwa mwaka mzima, ili kufanya mafundisho yawe more practical!! Badala yake wanawapa mitihani ya nadharia tena!! Assesment ingefanyikia huko huko field mahakamani, ofisi za waendendesha mashitaka, ofisi za mawakili wakiwa kwenye uhalisia wa kazi kwa vitendo!1
 
Sasa hili haliwezi kudhibitiwa na mtihani wa theory wa MCT ndio sababu tunataka matatizo haya yatafutiwe njia sahihi ya kuyatatua na sio mtihani wa MCT
Ni mfumo mzima upo corrupt we angalia tu mfano walimu wa zamani na wa sasa, ndo maana wenzetu wanawekeza sana kwenye AI and robotics sababu wanajua wanaweza kumrestrict to a specific tasks; maana binadamu wa sasa wana mambo mengi sana kichwani and majority are irrelevant.
 
Wizara za Afya na Elimu zipo kufanya nini?
 
Kwahiyo mnataka mfanye kazi bila leseni?
 
Kwakweli ukiangalia hili jambo kwa undani utakubaliana nami kwamba hao wanaowafelisha hawa vijana wenyewe walifikia hapo walipo kupitia nguvu za uchawi. Mwenye akili timamu hawezi kabisa kukubaliana na huu utaratibu. Kama siyo uchawi unawasumbua, basi watoke kwenye hizo ofisi zao waende kwenye hivyo vyuo ambamo hawa vijana wamesoma na wakakutane na ma Lecturer wao wakawaeleze wanachokihitaji kwa ajili hawa vijana madaktari wapate vyeti vyao.
 
Mkuu kwenye professional zote Bongo ni majanga. Wahitimu wanamaliza huku hawana utaalam sahihi. Mimi ndhani hiyo mitihani inaakisi kiisi hasa cha shida. Tusiingize siasa kwenye utalaam. Sheria, Udaktari, uinjiania, kote huko asilimia kubwa ya ma-graduate ni vilaza. BTW hii ni barua imeandikwa na watu wenye hadhi ya kuitwa madaktari imekaa kichawa-chawa namna hii? Siamini!
 
Uwezo wao ni mdogo. Chanzo cha matatizo ni vyuo wanavyosoma. Tusiweke siasa kwenye utaalam.
 
Nani anaeleta mizaha? Mimi ninayeshauri wasipoteze muda wawahi VETA kusoma coursevwatakayoi mudu? Au wewe unaetaka watu waliofeli waonewe huruma na kupewa ruhusa kwenda kuchezea afya za watu?
Nina nani kakuambia wamefeli? Wewe unajua Daktari katika mtihani huo wa hujuma anatakiwa afaulu kwa marks ngapi? Na je unaweza kuekeza ni kwanini matokeo ya usiri mkubwa? Na je unaweza kusema ni kwanini Daktari akakata rufaa hawezi kuoneshwa mtihani wake? Kuna hujuma na sio watu kufeli mtihani.
 
Rejaa barua za Madaktari pls kwa kuwa hawapingi mtihani ila wanapinga hujuma zinazofanywa kwao. Ni kuekeze tu Madaktari bingwa ndio wenye kuweza kumthibitisha mtu kuwa daktari na si mtihani wa MCT. Tuwaache madaktari bingwa watusaidie kupata Daktari bora na kumhakiki Daktari na si maswali 200 ya multiple choice.
 
At this point hata sijui unacholalamikia ni kitu gani. Mada inasema madokta wanataka leseni ya kuweza kufungua private practice zao; ambapo MCT imekuwa kikwazo.



Sasa kama unataka kufungua private practice huko vigezo vyake na masharti yake ya kuendesha hizo clinics yanatolewa na MCT, wewe unaleta habari za kufundishwa na daktari bingwa so uachwe. Hata hiyo training unayopewa na huyo daktari bingwa mwongozo wake unatolewa na MCT.

Moreover ‘Medical Councils’, ndio zenye dhamana ya kutunga masharti hayo duniani, sio Tanzania pekee.

Isitoshe huko kwengine duniani kuna taasisi ya kukagua hizo huduma na lazima usajiliwe nao waje kukagua huduma zako mara kwa mara kama zina standards. Kwetu hakuna taasisi kama hiyo mnataka mpewe vibali mkadhuru watu huko bila ya kusimamiwa.
 
Shida yenu ni moja nyie madaktari mkipata kazi mnaanza kuvimba mitaani, mnaanza kufanya sexual harassment kwa wagojwa wenu hasa wa kike.
 
Naam, hapa ndipo nchi yetu ilipo sasa, kizazi cha vijana legevu walalamishi, wasio na spirit ya kufight, hebu kwanza tuelewesheni hao asilimia 50% waliofaulu wamefaulu vipi na nyie mkafeli? taaluma ya afya ni taaluma nyeti inayohitaji umakini kama sheria ilipelekwa hadi bungeni ikapitishwa kwa lengo la kumlinda mwananchi anaekuja kupewa huduma na mitihani ya leseni ni utaratibu common hata nchi zilizoendelea mfano marekani kuna USMLE, Uingereza kuna Cambridge exams nyie mnalia lia nini hapa? tumefika sehem vijana wanataka short cut kwenye kila jambo? kizazi very corrupt kina amini there is a way past every thing, sasa wanatafuta sympathy? alafu waje kutibu wananchi wasababishe madhara taaluma nzima ionekane hovyp? juzi tu tumona mtoa huduma ya afya anaosha vifaa vya hospitali kama vyombo vya kupikia makande na kuanika juani, si ndio watu wa namna hii? mbona nimesikia wanao tunga mitihani hapo MCT ni wasimamizi wa hawa madaktari kutoka hospitali wanakofanya mafunzo?
Hii taaluma sio kama taaluma zisizo na madhara immediate ya uhai wa binadamu, sio kama kupotea kwa dola na kupanda bei ya mafuta wakati tuna wachumi waliotakiwa kuona projections za kupotea dola kabla haijatokea! bahati nzuri hakuna mtu anakufa immediately ukiacha kulala njaa kama daktari akikosea dose au operesheni! mtu anapoyteza maisha au kupata ulemavu wa milele hapo hapo! Nina mshangaa sana waziri wa afya kuintertain hawa madaktari goi goi! unaounda tume ya kufanya nini? tatizo humu kwenye hili group unakuta watoto wa vigogo wenye uwezo mdogo waliopata nafasi za kusoma udaktari bila kuwa na sifa sasa wakifeli sheria zinaanza kupindishwa! Kufaulu mitihani ya chuo na huu utitiri wa vyuo vingine vya nje kama China ambako vigogo wanapeleka watoto wao haiwezi kuwa justification kuwa nyie mmefaulu na grade A msifanye mitihani! Kuna vyuo China wakati wa Corona vilianza kufundisha udaktari online! alafu unapata A ya chuo cha aina hii uantuambia una uwezo wa kutibu mtu?

Acheni kucheza na afya za watu!
 
wewe utakuwa miongoni mwa hao makanjanja!
1. Kupima uwezo si ndio huo mtihani? mtihani umetungwa na wasimamizi wa vituo vya internship hao hao wewe unaodai wamekufaulisha, Sio kwamba huko internship mnafanya mafunzo chini ya usimamizi? mnasema mnatibu watu wanapona? mbona nilienda Mloganzila nikaambiwa daktari wa mafunzo ya vitendo ataniona na kuwasilisha kwa Specialist ili kupata plan ya matibabu? mnatibu wenyewe? basi na huko mtakuwa mnaua watu hzi hospitali nazo zichunguzwe!

2. Kufaulu chuo haikutosha nadhani ndio maana Bunge likapitisha sheria ya kuunify quality, sii juzi tu hapa tumesikia sijui chuo cha Ifakara kimeitisha vyeti vya wahitimu ? sasa wewe utakubali utibiwe na daktari alienyanganywa cheit alichosomea bila kufanya mitihani ya bodi yake ya taaluma kuthibitisha kama kweli ni Doctor? Au wale MaDoctor waliorudi Tanzania toka China ambako hata wagonjwa wa kichina hawakubali kuguswa na mwanafuzni muafrica warudi tu nchini wapewe visu waanze kutuchana wakati huko walikosoma hata kupasua jipu hawajahwahi?

3. Unasema mtihani wa masaa matatu au sita hautoshi kupima uwezo wa mtu? unataka kupewa muda gani kuonyesha uwezo? mtihani wa NECTA huwa ni masaa mangapi? unataka mtihani wa mwezi mzima? eti mtihani wa Practical sasa unaenda kupractice nini kama theory ya hicho kitu hauna?
 
Mbona huongelei asilimia 50% waliofaulu? hao wamekwamishwa kwa vigezo gani? wamefeli mtihani! hizo habari za kutumia hela ya mzazi na ndugu haiwezi kuwa sababu ya kuruhusu daktari asie na uwezo wa kutibu ili akasababishe madhara kwa wagonjwa! Huyu mtu angetumia hizo hela za mzazi kusoma au kufanya vitu anavyoviweza! angefungua banda la mitumba!
 
Hawa madogo, wasituchoshe, wanataka kufaulu kwa sympathy? huku jamii forum tunajadili issues ambazo ni intriguing, au kama wangekuwa wameleta tangble evidences kuwa wameonewa au wamekuwa targetted specifically kuonewa kwaa grounds tofauti na kigezo cha kufaulu mtihani! Hapa kuna asilimia 50% ya wenzao wamefaulu huu mtihani swali ni kuwa hawa wamefaulu kwa upendeleo au halali? kama ni halali hawa waliofeli wana lalamika nini? ni kwamba wajitambue watie bidii warudie mtihani wafaulu waje kututibu wakiwa na ni madaktari Salama! Humu ndani mtu ajitokeze ambaye yuko tayari kwenda theater kufanyiwa Operation na mmoja wa hawa madaktari! maneno ya kwamba wamesomeshwa na hela za mzazi na sasa wako nyumbani hayana mashiko kwamba mzazi kakusomesha kuwa rubani hujakidhi vigezo lakini kwa vile hela ya mzazi ilishatumika tukupe ndege urushe uianghushe ili kumfurahisha mzazi wako? hizi ni tabia za vi "LAST BORN" vilivyo dekezwa kwao! Kazeni mbwa nyie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…