Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia

Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia

Ni vyema ukaweka mizaha pembeni, kada hii ni muhimu sana kama sio Leo kesho utakutana na daktari, tafuta kuelewa changamoto walizo nazo na uwasaidei kusema Ili waweze kukuza ufanisi wao kesho ukikutana nao waweze kukuhudumia vyema
Nani anaeleta mizaha? Mimi ninayeshauri wasipoteze muda wawahi VETA kusoma coursevwatakayoi mudu? Au wewe unaetaka watu waliofeli waonewe huruma na kupewa ruhusa kwenda kuchezea afya za watu?
 
piga kitabu mzee hata wao walipita huko huko
 
Kwenye afya za watu tusiweke siasa.

Mfano ukisoma Namba 3 wanataka standardization ili wafaulu.

Watu wengi wanaenda vyuo kwa siasa ila uwezo wao mdogo.

Na huko chuo wanafaulishwa wanakamatwa kwenye mitihani.

Ni sawa na walimu wanavyokataa mitihani maana wanajua kabisa lazima watafeli

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Sasa ndo umpime daktari kwa maswali 100 ya multiple choice??
Huo mfumo ni wa hovyo, hapo unachopima sio uelewa ila ni spidi ya kumaliza maswali 200 ya kuchagua kwa masaa 6.

Kwanini wasipewe mitihani wajieleze tu, hapo dokta anafanya ana anaa doo tu. Wanapima uwezo wa makisio
 
Reja hoja za Madaktari na Rejea barua zote ninazokuwekea hapa, Mtihani wa MCT hauna ufumbuzi wa hayo unayoyasema. Mtihani wao ni hujuma. Ni hujuma kwa sababu madaktari wametibu watu na kuisaidia kurejesha afya za watu . Hawa madaktari tunaowaongelea hawata hizo changamoto ulizoziainisha na changamoto hizi hawahusiki nazo na zingewahusi wasingekuwa hapo wangekuwa wamerudia Clinical rotations na wengine wanngeshitakiwa. Changamoto ulizozianisha zinatokana na uzembe na uzembe hauwezi kutatukiwa na mtihani wa MCT. Rejea comments zingine. Soma hizo nilizo zi attach. Soma zote bila uvivu.

There is sufficient evidence showing relation between new medics including junior doctors and causes of medical error.

Hayo sio maneno yangu kuna ‘research papers’ luluki from various parts of the worlds, with better health systems; just go check on PubMed and MEDLINE.

Moreover hata hospitali zinazo record medical errors, evidence shows a majority are caused by new medics nurses/doctors. Kuna sababu luluki zinazotajwa kama chanzo cha mistake leading to medical errors; chiefly among them is lack of practice experience and fatigue.

Unatakiwa ufundishwe hilo katika masomo yako; sababu za medical errors, how to avoid them and systems in place to reduce them. Kwa sababu hilo ni tatizo kubwa duniani sio Tanzania tu linalopelekea hundred of thousand unnecessary loss of lives each year. Halafu unatuambiwa hawa watu wapewe leseni ya kufanya kazi unsupervised.
 
Haya mabaraza ya wanasheria, madaktari, wajenzi, na pia wafamasia ni ya kipigaji zaidi kuliko usimamiaji wa weledi kwenye fani hizo!! Wamejiandalia mazingira kunyonya pesa kiurahisi!! Haiwezekani baraza la mct au pct kutoa mtihani wa leseni kwa wahitimu ambao hawakuhusika kabisa katika kuwafundisha!! Wanawafelisha ili kuandaa mazingira ya rushwa, na kupiga tena pesa kupitia supplimentary exams!
Haiingi akilini daktari aliyefaulu mitihani yake chuoni na kule internship chini ya usimamizi wa maprofesa na madaktari mabingwa halafu wewe uje useme hawafai kupata leseni.

Kuhusu law school, hii shule ya sheria ndo sifuri kabisa! Badala ya kuwapima wanafunzi wao huko huko field kwa mwaka mzima, ili kufanya mafundisho yawe more practical!! Badala yake wanawapa mitihani ya nadharia tena!! Assesment ingefanyikia huko huko field mahakamani, ofisi za waendendesha mashitaka, ofisi za mawakili wakiwa kwenye uhalisia wa kazi kwa vitendo!1
 
Sasa hili haliwezi kudhibitiwa na mtihani wa theory wa MCT ndio sababu tunataka matatizo haya yatafutiwe njia sahihi ya kuyatatua na sio mtihani wa MCT
Ni mfumo mzima upo corrupt we angalia tu mfano walimu wa zamani na wa sasa, ndo maana wenzetu wanawekeza sana kwenye AI and robotics sababu wanajua wanaweza kumrestrict to a specific tasks; maana binadamu wa sasa wana mambo mengi sana kichwani and majority are irrelevant.
 
Kwenye afya za watu tusiweke siasa.

Mfano ukisoma Namba 3 wanataka standardization ili wafaulu.

Watu wengi wanaenda vyuo kwa siasa ila uwezo wao mdogo.

Na huko chuo wanafaulishwa wanakamatwa kwenye mitihani.

Ni sawa na walimu wanavyokataa mitihani maana wanajua kabisa lazima watafeli

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Wizara za Afya na Elimu zipo kufanya nini?
 
Kwahiyo mnataka mfanye kazi bila leseni?
 
Kwakweli ukiangalia hili jambo kwa undani utakubaliana nami kwamba hao wanaowafelisha hawa vijana wenyewe walifikia hapo walipo kupitia nguvu za uchawi. Mwenye akili timamu hawezi kabisa kukubaliana na huu utaratibu. Kama siyo uchawi unawasumbua, basi watoke kwenye hizo ofisi zao waende kwenye hivyo vyuo ambamo hawa vijana wamesoma na wakakutane na ma Lecturer wao wakawaeleze wanachokihitaji kwa ajili hawa vijana madaktari wapate vyeti vyao.
 
Wazee wengi wana asili ya uchawi, hawataki kada zao ziwe na watu wengi ili waendelee kujiona special. Kada zinazoumia zaidi kwa wazee wachawi ni hizi

1.) Architecture (kada yangu) - Miaka mitano degree

2.) Udaktari - Miaka mitano degree

3.) Sheria - Miaka mitano hadi Law school
Mkuu kwenye professional zote Bongo ni majanga. Wahitimu wanamaliza huku hawana utaalam sahihi. Mimi ndhani hiyo mitihani inaakisi kiisi hasa cha shida. Tusiingize siasa kwenye utalaam. Sheria, Udaktari, uinjiania, kote huko asilimia kubwa ya ma-graduate ni vilaza. BTW hii ni barua imeandikwa na watu wenye hadhi ya kuitwa madaktari imekaa kichawa-chawa namna hii? Siamini!
 
Uwezo wao mdogo darasani?
Hoja ni je huo uwezo unaupimaje?
Chuo amefauluje?
Intern amefauluje?
Wagonjwa intern amewatibuje?
Kama uwezo wake ni mdgo
Vyuo vinavyofundisha basi havifai maaana vinapitisha tu
, madaktari bingwa wanaosimamia intern basi hawafai wanawapitisha tu,
Akae nyumbni aje baada ya mwaka 1 arudie mtihan huo uwezo nyumbni anauongezaje?? Wakati amezungukwa na watu wanaomdai na familia inamtegemea na hamna mtu wa kumfundisha,
Je uwezo wa mtu aliefaulu miaka 19 utaupima kwa siku 1 kwa mda wa masaa 6 qns 200? Za multiple choice?
The ans is no
Basi kuna haja kubwa ya huu mtihan kurudishwa vyuoni ambako ndo madarasa yalipo kama alivyosema msajili ili waendelee kujisomea na kufundishwa darasani uwezo wao uongezeke
Uwezo wao ni mdogo. Chanzo cha matatizo ni vyuo wanavyosoma. Tusiweke siasa kwenye utaalam.
 
Nani anaeleta mizaha? Mimi ninayeshauri wasipoteze muda wawahi VETA kusoma coursevwatakayoi mudu? Au wewe unaetaka watu waliofeli waonewe huruma na kupewa ruhusa kwenda kuchezea afya za watu?
Nina nani kakuambia wamefeli? Wewe unajua Daktari katika mtihani huo wa hujuma anatakiwa afaulu kwa marks ngapi? Na je unaweza kuekeza ni kwanini matokeo ya usiri mkubwa? Na je unaweza kusema ni kwanini Daktari akakata rufaa hawezi kuoneshwa mtihani wake? Kuna hujuma na sio watu kufeli mtihani.
 

There is sufficient evidence showing relation between new medics including junior doctors and causes of medical error.

Hayo sio maneno yangu kuna ‘research papers’ luluki from various parts of the worlds, with better health systems; just go check on PubMed and MEDLINE.

Moreover hata hospitali zinazo record medical errors, evidence shows a majority are caused by new medics nurses/doctors. Kuna sababu luluki zinazotajwa kama chanzo cha mistake leading to medical errors; chiefly among them is lack of practice experience and fatigue.

Unatakiwa ufundishwe hilo katika masomo yako; sababu za medical errors, how to avoid them and systems in place to reduce them. Kwa sababu hilo ni tatizo kubwa duniani sio Tanzania tu linalopelekea hundred of thousand unnecessary loss of lives each year. Halafu unatuambiwa hawa watu wapewe leseni ya kufanya kazi unsupervised.
Rejaa barua za Madaktari pls kwa kuwa hawapingi mtihani ila wanapinga hujuma zinazofanywa kwao. Ni kuekeze tu Madaktari bingwa ndio wenye kuweza kumthibitisha mtu kuwa daktari na si mtihani wa MCT. Tuwaache madaktari bingwa watusaidie kupata Daktari bora na kumhakiki Daktari na si maswali 200 ya multiple choice.
 
Rejaa barua za Madaktari pls kwa kuwa hawapingi mtihani ila wanapinga hujuma zinazofanywa kwao. Ni kuekeze tu Madaktari bingwa ndio wenye kuweza kumthibitisha mtu kuwa daktari na si mtihani wa MCT. Tuwaache madaktari bingwa watusaidie kupata Daktari bora na kumhakiki Daktari na si maswali 200 ya multiple choice.
At this point hata sijui unacholalamikia ni kitu gani. Mada inasema madokta wanataka leseni ya kuweza kufungua private practice zao; ambapo MCT imekuwa kikwazo.


AAAA5145-2C01-49E7-927D-08C62B516BF5.jpeg

Sasa kama unataka kufungua private practice huko vigezo vyake na masharti yake ya kuendesha hizo clinics yanatolewa na MCT, wewe unaleta habari za kufundishwa na daktari bingwa so uachwe. Hata hiyo training unayopewa na huyo daktari bingwa mwongozo wake unatolewa na MCT.

Moreover ‘Medical Councils’, ndio zenye dhamana ya kutunga masharti hayo duniani, sio Tanzania pekee.

Isitoshe huko kwengine duniani kuna taasisi ya kukagua hizo huduma na lazima usajiliwe nao waje kukagua huduma zako mara kwa mara kama zina standards. Kwetu hakuna taasisi kama hiyo mnataka mpewe vibali mkadhuru watu huko bila ya kusimamiwa.
 
Shida yenu ni moja nyie madaktari mkipata kazi mnaanza kuvimba mitaani, mnaanza kufanya sexual harassment kwa wagojwa wenu hasa wa kike.
 
Mheshimiwa Rais,
Amani iwe nawe daima.

Mheshimiwa Rais, Awali ya yote tunakupa pole kwa kazi zako za kila siku za kuhudumia Watanzania, huku tukiamini Mwenyezi Mungu anaendelea kukujalia afya tele na tunatambua pia una majukumu mengi kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, hii ni sauti ya Umoja wa Madaktari wahitimu watarajali ambao tunaleta kwako waraka huu kwa lengo la kukufikishia ujumbe kutokana na vikwazo vinavyotukabili ambavyo vimetufanya kugeuka ombaomba mtaani licha kwamba sisi ni wasomi madaktari ambao tumeshindwa kujiajiri, kuajirika kutokana na kizingiti kinachoitwa leseni.
Mheshimiwa Rais, tumeamua kuleta waraka huu kwako baada ya juhudi zetu za kupeleka changamoto zetu na hata kuonana na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya kugonga mwamba.

Mheshimiwa Rais, Tumekuwa kwenye mazoezi ya vitendo (internship) katika hospitali kubwa za rufaa nchini, huko kazi zote na za aina zote tumekuwa tukizifanya sisi na kusimamiwa na madaktari bingwa nchini.Huko tumeokoa maisha ya Watanzania wenzetu wengi, tumejipatia umahiri wa kuhudumia wagonjwa kwa uwezo wa elimu tuliyonayo.

Mheshimiwa Rais, Sisi madaktari wa utarajali tunashangazwa na kuumizwa na utaratibu wa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) pamoja na Wizara ya Afya, kwa kadhia kubwa wanayotusababishia.
Sisi madaktari watarajali tunaamini Serikali ilikuwa na nia njema ilipoamua kutunga Sheria No.11 ya Mwaka 2017 ambayo ilipitishwa na Bunge letu Tukufu ikitaka kila Mhitimu wa fani ya Udaktari sharti apewe leseni baada ya kufanya mtihani wa MCT.
Mbali na nia hiyo njema ya Serikali, bahati mbaya chombo hiki hakijaweza kujua kifanye kazi ipi na kwa wakati upi ili kiweze kulisaidia taifa lipate madaktari bora na sio bora madaktari.

Mheshimiwa Rais, hatuipingi sheria hiyo isipokuwa utaratibu au kanuni zinazotumika, hususan kuanzishwa kwa mtihani wa ‘pre na post internship. Baraza hili (MCT) limekuwa likiendesha mitihani hiyo kwa hasara, uonevu, ukatili na hujuma kwa madaktari watarajali.
Ikumbukwe kwamba sisi madaktari Watarajali hatupingi kuwapo kwa mitihani hiyo ikizingatiwa tumemaliza vyuo pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo (internship) na kupata ufaulu usiotiliwa shaka.

Tunachokipinga na ambacho kimetufanya kuandika waraka huu kwako Mheshimwa Rais ni haya yafuatayo:

1. Mtihani wa baada ya utarajali (post internship) uliofanyika 22/03/2023 kumekuwa na massive failure kiasi ambacho hadi imesababisha Baraza kutokutoa takwim za waliofeli na waliofaulu ingawa mpaka sasa tupo madaktari zaidi ya 300 ambao matokeo hayakutoka vizuri hivyo kushindwa kupatiwa leseni, hivyo tunaomba mtihani huu usahihishwe upya na matokeo yafanyiwe standardization, na usahihishwe na wasimamizi wa nje ya MCT (external examiners) ili kuondoa hii massive failure kama ilivyotokea matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 mitihani ilisahihishwa upya na ufaulu ukapatikana
2. MCT kutokuzingatia uhalisia wa namna ya kumpata daktari bora
3. MCT kutumia mtihani kwa lengo la kuondosha changamoto za ulevi uliopitiliza kwa baadhi ya madaktari, kuchelewa kazini au kutokufika kazini pamoja na uzembe kazini
4.MCT kutokuzingatia muda wa daktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kwenda kufanya kazi ili kulihudumia taifa.
5. MCT kutokuzingatia namna sahihi ya kumpima daktari kulingana na huduma zinazotolewa katika hospitali tunazofanyia internship

6. MCT kutokujali na kuheshimu muda jambo linalopelekea daktari kutaka hatari ya kupoteza taaluma yake kwa kusubiri mtihani kwa muda mrefu wakati mwingine kwa miezi takribani 10.
7. MCT kutokuwa wawazi juu ya alama (marks) za ufaulu na uendeshaji mzima wa mtihani na matokeo utakaomfanya mtu ajue amefeli idara ipi hata baada ya kukata rufaa.
8. MCT kutokuheshimu na kuzingatia muda tunaopaswa kumaliza taaluma ya udaktari.

Ushauri na mapendekezo yetu.

1. Yafanyike marekebishio ya sheria ili iweze kuakisi upatiakanaji wa madaktari bora.
2. Wizara ifuatilie mapungufu yaliyopo MCT na itumie dhamana yake kuwawezesha madaktari wapate leseni ili washiriki ujenzi wa taifa lao.

3. Wizara itoe leseni baada ya madaktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kufaulu vizuri kwa kuzingatia taarifa ya hospitali ambayo daktari amefanya mazoezi kwa vitendo (internship).
4. Tunashauri kusiwepo na mtihani wa leseni, kuwepo na mtihani wa kumpima mwanafunzi kama ana uwezo wa kuwa daktari bora baada ya kumaliza mitihani ya chuo na kabla ya kuapa au kwenda mazoezi kwa vitendo (internship). Hii itapelekea ufaulu mzuri kwa sababu ya mtu kuwa na muda wa kutosha kujiandaa na watakaotakiwa kurudia mtihani warudie kila baada ya miezi miwili katika kituo kimoja ili kuepuka gharama kubwa. Hii itapelekea milango ya hujuma, rushwa, uzalilishaji na uonevu anaoupata daktari wakati wa kusubiri mtihani kutoweka.
5. Mtihani wa kumpima mwanafunzi ili aweze kuwa daktari utungwe kama inavyofanyika vyuoni, mtihami wa kuchagua (multiple choice) wa maswali 100 au 200 pekee hauwezi kuwa kielelezo cha kumpata daktari bora kama ilivyo sasa.
6. Kuwepo na muda rafiki wa kukata rufaa walau kuanzia mwezi mmoja.
7. Kwakuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC), hivyo tunapendekeza itumie mifumo inayotumiwa pia na nchi wanachama ambapo wahitimu wa udaktari wanapewa mtihani online na kwa muda wowote. Nchi zote wanachama wa EAC zenye utaratibu wa kufanya mitihani ya leseni, mtihani na alama (marks) zake zinajulikana na zipo kwenye website zao isipokuwa Tanzania tu ndiyo alama za ufaulu hazijulikani.

Mheshimiwa Rais, sisi madaktari watarajali tumesoma kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu na kumalizia mwaka mmoja wa mafunzo ya vitendo (internship) na tumefaulu vizuri sana hadi kufikia ngazi ya utabibu, ni nani leo anaweza kusema sisi sio wasomi? Ni nani anayeweza kusema kuwa sisi sio madaktari ili hali tumetibu wagonjwa mwaka mzima na kutunukiwa vyeti vya ufaulu wa alama A ?

Mheshimiwa Rais, ni ukweli kwamba Taifa letu linahitaji madaktari bora, lakini je madaktari bora wanaweza kupatika kupitia maswali 200 ya mtihani wa kuchagua kwa muda wa saa tatu mpaka sita pekee?

Mheshimiwa Rais, kutokana na kadhia ya namna hii huenda Wizara yenye dhamana na afya haiviamini vyuo vyake vilivyopo nchini, hivyo wanaona suluhisho pekee la kupata madaktari bora ni huo mtihani wa saa 3 mpaka sita ambao utaratibu wake umekuwa kikwazo kwa daktari ambaye tayari alikwisha kula kiapo kujiajiri au kuajiriwa katika sekta zote, yaani umma na binafsi.

Mheshimiwa Rais, swali la kujiuliza na lipo kwa Watanzania wengi kama ambavyo walivyoaminishwa na MCT ni hili, Je ni kweli sisi madaktari ni waoga wa mtihani na hatutaki kufanya mtihani wa kujipima wa MCT? Jibu ni hapana!
MCT wanapaswa watoe leseni kwa kila daktari aliyefaulu mazoezi kwa vitendo kwakuwa moja kwa moja ana sifa za kuwa na leseni kwa sababu amekutana na wagonjwa, amewatibu, wamepona na amefanikiwa kuokoa maisha ya watu.

Mheshimiwa Rais, tunasisitiza hatupingi mtihani wa kupata leseni, tunashauri uwepo isipokuwa uende sambamba na mitihani ya kumaliza vyuo na si unaompima daktari baada ya mazoezi kwa vitendo. Utaratibu wa sasa ujulikane ni batili, hivo tunaomba standardization ifanyike na tupatiwe leseni

Mheshimiwa Rais, tunashauri Serikali ipitie upya Sheria ya mitihani ya mwaka 2017 ili kuwepo na utaratibu mzuri usio na malalamiko mengi na kuwepo uwazi wa kutosha.

Aidha tunashauri vyuo vya udakitari viwe chini ya Wizara ya Afya na sio Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili waweze kuvisimamia vizuri viweze kutoa wataalam wazuri wa afya.

Tunakushukuru sana.
Kupitia kwako ni matumaini yetu maombi yetu yatapata ufumbuzi wako wewe Rais wetu na Mama yetu mpendwa.
Naam, hapa ndipo nchi yetu ilipo sasa, kizazi cha vijana legevu walalamishi, wasio na spirit ya kufight, hebu kwanza tuelewesheni hao asilimia 50% waliofaulu wamefaulu vipi na nyie mkafeli? taaluma ya afya ni taaluma nyeti inayohitaji umakini kama sheria ilipelekwa hadi bungeni ikapitishwa kwa lengo la kumlinda mwananchi anaekuja kupewa huduma na mitihani ya leseni ni utaratibu common hata nchi zilizoendelea mfano marekani kuna USMLE, Uingereza kuna Cambridge exams nyie mnalia lia nini hapa? tumefika sehem vijana wanataka short cut kwenye kila jambo? kizazi very corrupt kina amini there is a way past every thing, sasa wanatafuta sympathy? alafu waje kutibu wananchi wasababishe madhara taaluma nzima ionekane hovyp? juzi tu tumona mtoa huduma ya afya anaosha vifaa vya hospitali kama vyombo vya kupikia makande na kuanika juani, si ndio watu wa namna hii? mbona nimesikia wanao tunga mitihani hapo MCT ni wasimamizi wa hawa madaktari kutoka hospitali wanakofanya mafunzo?
Hii taaluma sio kama taaluma zisizo na madhara immediate ya uhai wa binadamu, sio kama kupotea kwa dola na kupanda bei ya mafuta wakati tuna wachumi waliotakiwa kuona projections za kupotea dola kabla haijatokea! bahati nzuri hakuna mtu anakufa immediately ukiacha kulala njaa kama daktari akikosea dose au operesheni! mtu anapoyteza maisha au kupata ulemavu wa milele hapo hapo! Nina mshangaa sana waziri wa afya kuintertain hawa madaktari goi goi! unaounda tume ya kufanya nini? tatizo humu kwenye hili group unakuta watoto wa vigogo wenye uwezo mdogo waliopata nafasi za kusoma udaktari bila kuwa na sifa sasa wakifeli sheria zinaanza kupindishwa! Kufaulu mitihani ya chuo na huu utitiri wa vyuo vingine vya nje kama China ambako vigogo wanapeleka watoto wao haiwezi kuwa justification kuwa nyie mmefaulu na grade A msifanye mitihani! Kuna vyuo China wakati wa Corona vilianza kufundisha udaktari online! alafu unapata A ya chuo cha aina hii uantuambia una uwezo wa kutibu mtu?

Acheni kucheza na afya za watu!
 
Uwezo wao mdogo darasani?
Hoja ni je huo uwezo unaupimaje?
Chuo amefauluje?
Intern amefauluje?
Wagonjwa intern amewatibuje?
Kama uwezo wake ni mdgo
Vyuo vinavyofundisha basi havifai maaana vinapitisha tu
, madaktari bingwa wanaosimamia intern basi hawafai wanawapitisha tu,
Akae nyumbni aje baada ya mwaka 1 arudie mtihan huo uwezo nyumbni anauongezaje?? Wakati amezungukwa na watu wanaomdai na familia inamtegemea na hamna mtu wa kumfundisha,
Je uwezo wa mtu aliefaulu miaka 19 utaupima kwa siku 1 kwa mda wa masaa 6 qns 200? Za multiple choice?
The ans is no
Basi kuna haja kubwa ya huu mtihan kurudishwa vyuoni ambako ndo madarasa yalipo kama alivyosema msajili ili waendelee kujisomea na kufundishwa darasani uwezo wao uongezeke
wewe utakuwa miongoni mwa hao makanjanja!
1. Kupima uwezo si ndio huo mtihani? mtihani umetungwa na wasimamizi wa vituo vya internship hao hao wewe unaodai wamekufaulisha, Sio kwamba huko internship mnafanya mafunzo chini ya usimamizi? mnasema mnatibu watu wanapona? mbona nilienda Mloganzila nikaambiwa daktari wa mafunzo ya vitendo ataniona na kuwasilisha kwa Specialist ili kupata plan ya matibabu? mnatibu wenyewe? basi na huko mtakuwa mnaua watu hzi hospitali nazo zichunguzwe!

2. Kufaulu chuo haikutosha nadhani ndio maana Bunge likapitisha sheria ya kuunify quality, sii juzi tu hapa tumesikia sijui chuo cha Ifakara kimeitisha vyeti vya wahitimu ? sasa wewe utakubali utibiwe na daktari alienyanganywa cheit alichosomea bila kufanya mitihani ya bodi yake ya taaluma kuthibitisha kama kweli ni Doctor? Au wale MaDoctor waliorudi Tanzania toka China ambako hata wagonjwa wa kichina hawakubali kuguswa na mwanafuzni muafrica warudi tu nchini wapewe visu waanze kutuchana wakati huko walikosoma hata kupasua jipu hawajahwahi?

3. Unasema mtihani wa masaa matatu au sita hautoshi kupima uwezo wa mtu? unataka kupewa muda gani kuonyesha uwezo? mtihani wa NECTA huwa ni masaa mangapi? unataka mtihani wa mwezi mzima? eti mtihani wa Practical sasa unaenda kupractice nini kama theory ya hicho kitu hauna?
 
Ndugu yako aliyesoma miaka mitano kwa garama kubwa kutoka kwa mama/baba masikini akikwamishwa kupata Leseni ajiajiri/aajiriwe ndo utakuja kujua uchungu wake,maumivu wanayoyapitia hawa madogo ni maumivu makali sana,ni Bora kukaa kimya kuliko kuwakatisha tamaa,Dunia duara.
Mbona huongelei asilimia 50% waliofaulu? hao wamekwamishwa kwa vigezo gani? wamefeli mtihani! hizo habari za kutumia hela ya mzazi na ndugu haiwezi kuwa sababu ya kuruhusu daktari asie na uwezo wa kutibu ili akasababishe madhara kwa wagonjwa! Huyu mtu angetumia hizo hela za mzazi kusoma au kufanya vitu anavyoviweza! angefungua banda la mitumba!
 
Kwanza poleni kwa chanhamoto.

Pili siungi mkono kwenye wazo lako la kufuta huo mtihani kabisa kama ulivyodai , maana ninavyofahamu medical student yoyote ni lifelong learner ndio maana kunakuwepo na CPD.

Ushauri wangu ni uwepo utaratibu mzuri kuanzia setters , moderators , markers , final verifiers kila ngazi wawepo watu tofauti mtu asijirudie kwa huo mtihani kuondoa hizo rafu ambazo kweli zinaweza kuwa za kibinadamu au kwa makusudi.

Mitihani iko kwa kada zote za medical duniani wakishindwa waje wajifunze kwa wenzetu huku wa USMLE ambao una step 1 hadi 3 ambayo iko vizuri na ukipass umepass kweli na inafanyika online katika centers zinazotambulika.
Hawa madogo, wasituchoshe, wanataka kufaulu kwa sympathy? huku jamii forum tunajadili issues ambazo ni intriguing, au kama wangekuwa wameleta tangble evidences kuwa wameonewa au wamekuwa targetted specifically kuonewa kwaa grounds tofauti na kigezo cha kufaulu mtihani! Hapa kuna asilimia 50% ya wenzao wamefaulu huu mtihani swali ni kuwa hawa wamefaulu kwa upendeleo au halali? kama ni halali hawa waliofeli wana lalamika nini? ni kwamba wajitambue watie bidii warudie mtihani wafaulu waje kututibu wakiwa na ni madaktari Salama! Humu ndani mtu ajitokeze ambaye yuko tayari kwenda theater kufanyiwa Operation na mmoja wa hawa madaktari! maneno ya kwamba wamesomeshwa na hela za mzazi na sasa wako nyumbani hayana mashiko kwamba mzazi kakusomesha kuwa rubani hujakidhi vigezo lakini kwa vile hela ya mzazi ilishatumika tukupe ndege urushe uianghushe ili kumfurahisha mzazi wako? hizi ni tabia za vi "LAST BORN" vilivyo dekezwa kwao! Kazeni mbwa nyie!
 
Back
Top Bottom