Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia

Mheshimiwa Rais,
Amani iwe nawe daima.

Mheshimiwa Rais, Awali ya yote tunakupa pole kwa kazi zako za kila siku za kuhudumia Watanzania, huku tukiamini Mwenyezi Mungu anaendelea kukujalia afya tele na tunatambua pia una majukumu mengi kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, hii ni sauti ya Umoja wa Madaktari wahitimu watarajali ambao tunaleta kwako waraka huu kwa lengo la kukufikishia ujumbe kutokana na vikwazo vinavyotukabili ambavyo vimetufanya kugeuka ombaomba mtaani licha kwamba sisi ni wasomi madaktari ambao tumeshindwa kujiajiri, kuajirika kutokana na kizingiti kinachoitwa leseni.
Mheshimiwa Rais, tumeamua kuleta waraka huu kwako baada ya juhudi zetu za kupeleka changamoto zetu na hata kuonana na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya kugonga mwamba.

Mheshimiwa Rais, Tumekuwa kwenye mazoezi ya vitendo (internship) katika hospitali kubwa za rufaa nchini, huko kazi zote na za aina zote tumekuwa tukizifanya sisi na kusimamiwa na madaktari bingwa nchini.Huko tumeokoa maisha ya Watanzania wenzetu wengi, tumejipatia umahiri wa kuhudumia wagonjwa kwa uwezo wa elimu tuliyonayo.

Mheshimiwa Rais, Sisi madaktari wa utarajali tunashangazwa na kuumizwa na utaratibu wa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) pamoja na Wizara ya Afya, kwa kadhia kubwa wanayotusababishia.
Sisi madaktari watarajali tunaamini Serikali ilikuwa na nia njema ilipoamua kutunga Sheria No.11 ya Mwaka 2017 ambayo ilipitishwa na Bunge letu Tukufu ikitaka kila Mhitimu wa fani ya Udaktari sharti apewe leseni baada ya kufanya mtihani wa MCT.
Mbali na nia hiyo njema ya Serikali, bahati mbaya chombo hiki hakijaweza kujua kifanye kazi ipi na kwa wakati upi ili kiweze kulisaidia taifa lipate madaktari bora na sio bora madaktari.

Mheshimiwa Rais, hatuipingi sheria hiyo isipokuwa utaratibu au kanuni zinazotumika, hususan kuanzishwa kwa mtihani wa ‘pre na post internship. Baraza hili (MCT) limekuwa likiendesha mitihani hiyo kwa hasara, uonevu, ukatili na hujuma kwa madaktari watarajali.
Ikumbukwe kwamba sisi madaktari Watarajali hatupingi kuwapo kwa mitihani hiyo ikizingatiwa tumemaliza vyuo pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo (internship) na kupata ufaulu usiotiliwa shaka.

Tunachokipinga na ambacho kimetufanya kuandika waraka huu kwako Mheshimwa Rais ni haya yafuatayo:

1. Mtihani wa baada ya utarajali (post internship) uliofanyika 22/03/2023 kumekuwa na massive failure kiasi ambacho hadi imesababisha Baraza kutokutoa takwim za waliofeli na waliofaulu ingawa mpaka sasa tupo madaktari zaidi ya 300 ambao matokeo hayakutoka vizuri hivyo kushindwa kupatiwa leseni, hivyo tunaomba mtihani huu usahihishwe upya na matokeo yafanyiwe standardization, na usahihishwe na wasimamizi wa nje ya MCT (external examiners) ili kuondoa hii massive failure kama ilivyotokea matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 mitihani ilisahihishwa upya na ufaulu ukapatikana
2. MCT kutokuzingatia uhalisia wa namna ya kumpata daktari bora
3. MCT kutumia mtihani kwa lengo la kuondosha changamoto za ulevi uliopitiliza kwa baadhi ya madaktari, kuchelewa kazini au kutokufika kazini pamoja na uzembe kazini
4.MCT kutokuzingatia muda wa daktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kwenda kufanya kazi ili kulihudumia taifa.
5. MCT kutokuzingatia namna sahihi ya kumpima daktari kulingana na huduma zinazotolewa katika hospitali tunazofanyia internship

6. MCT kutokujali na kuheshimu muda jambo linalopelekea daktari kutaka hatari ya kupoteza taaluma yake kwa kusubiri mtihani kwa muda mrefu wakati mwingine kwa miezi takribani 10.
7. MCT kutokuwa wawazi juu ya alama (marks) za ufaulu na uendeshaji mzima wa mtihani na matokeo utakaomfanya mtu ajue amefeli idara ipi hata baada ya kukata rufaa.
8. MCT kutokuheshimu na kuzingatia muda tunaopaswa kumaliza taaluma ya udaktari.

Ushauri na mapendekezo yetu.

1. Yafanyike marekebishio ya sheria ili iweze kuakisi upatiakanaji wa madaktari bora.
2. Wizara ifuatilie mapungufu yaliyopo MCT na itumie dhamana yake kuwawezesha madaktari wapate leseni ili washiriki ujenzi wa taifa lao.

3. Wizara itoe leseni baada ya madaktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kufaulu vizuri kwa kuzingatia taarifa ya hospitali ambayo daktari amefanya mazoezi kwa vitendo (internship).
4. Tunashauri kusiwepo na mtihani wa leseni, kuwepo na mtihani wa kumpima mwanafunzi kama ana uwezo wa kuwa daktari bora baada ya kumaliza mitihani ya chuo na kabla ya kuapa au kwenda mazoezi kwa vitendo (internship). Hii itapelekea ufaulu mzuri kwa sababu ya mtu kuwa na muda wa kutosha kujiandaa na watakaotakiwa kurudia mtihani warudie kila baada ya miezi miwili katika kituo kimoja ili kuepuka gharama kubwa. Hii itapelekea milango ya hujuma, rushwa, uzalilishaji na uonevu anaoupata daktari wakati wa kusubiri mtihani kutoweka.
5. Mtihani wa kumpima mwanafunzi ili aweze kuwa daktari utungwe kama inavyofanyika vyuoni, mtihami wa kuchagua (multiple choice) wa maswali 100 au 200 pekee hauwezi kuwa kielelezo cha kumpata daktari bora kama ilivyo sasa.
6. Kuwepo na muda rafiki wa kukata rufaa walau kuanzia mwezi mmoja.
7. Kwakuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC), hivyo tunapendekeza itumie mifumo inayotumiwa pia na nchi wanachama ambapo wahitimu wa udaktari wanapewa mtihani online na kwa muda wowote. Nchi zote wanachama wa EAC zenye utaratibu wa kufanya mitihani ya leseni, mtihani na alama (marks) zake zinajulikana na zipo kwenye website zao isipokuwa Tanzania tu ndiyo alama za ufaulu hazijulikani.

Mheshimiwa Rais, sisi madaktari watarajali tumesoma kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu na kumalizia mwaka mmoja wa mafunzo ya vitendo (internship) na tumefaulu vizuri sana hadi kufikia ngazi ya utabibu, ni nani leo anaweza kusema sisi sio wasomi? Ni nani anayeweza kusema kuwa sisi sio madaktari ili hali tumetibu wagonjwa mwaka mzima na kutunukiwa vyeti vya ufaulu wa alama A ?

Mheshimiwa Rais, ni ukweli kwamba Taifa letu linahitaji madaktari bora, lakini je madaktari bora wanaweza kupatika kupitia maswali 200 ya mtihani wa kuchagua kwa muda wa saa tatu mpaka sita pekee?

Mheshimiwa Rais, kutokana na kadhia ya namna hii huenda Wizara yenye dhamana na afya haiviamini vyuo vyake vilivyopo nchini, hivyo wanaona suluhisho pekee la kupata madaktari bora ni huo mtihani wa saa 3 mpaka sita ambao utaratibu wake umekuwa kikwazo kwa daktari ambaye tayari alikwisha kula kiapo kujiajiri au kuajiriwa katika sekta zote, yaani umma na binafsi.

Mheshimiwa Rais, swali la kujiuliza na lipo kwa Watanzania wengi kama ambavyo walivyoaminishwa na MCT ni hili, Je ni kweli sisi madaktari ni waoga wa mtihani na hatutaki kufanya mtihani wa kujipima wa MCT? Jibu ni hapana!
MCT wanapaswa watoe leseni kwa kila daktari aliyefaulu mazoezi kwa vitendo kwakuwa moja kwa moja ana sifa za kuwa na leseni kwa sababu amekutana na wagonjwa, amewatibu, wamepona na amefanikiwa kuokoa maisha ya watu.

Mheshimiwa Rais, tunasisitiza hatupingi mtihani wa kupata leseni, tunashauri uwepo isipokuwa uende sambamba na mitihani ya kumaliza vyuo na si unaompima daktari baada ya mazoezi kwa vitendo. Utaratibu wa sasa ujulikane ni batili, hivo tunaomba standardization ifanyike na tupatiwe leseni

Mheshimiwa Rais, tunashauri Serikali ipitie upya Sheria ya mitihani ya mwaka 2017 ili kuwepo na utaratibu mzuri usio na malalamiko mengi na kuwepo uwazi wa kutosha.

Aidha tunashauri vyuo vya udakitari viwe chini ya Wizara ya Afya na sio Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili waweze kuvisimamia vizuri viweze kutoa wataalam wazuri wa afya.

Tunakushukuru sana.
Kupitia kwako ni matumaini yetu maombi yetu yatapata ufumbuzi wako wewe Rais wetu na Mama yetu mpendwa.
Na mnavyojidai nyie half cooked ngedere nyie, fani ya hovyo sana mnabuni tu huko mahospitalini, hamna huruma kama hamtakufa vile.

Na mkome nyie ngedere
 
Hakuna anaetaka mtihani ufutwe, mtihani uendelee kuwepo lakini uwepo kwa wakati sahihi, mwanafunzi kabla hajawa Daktari apatiwe mtihani huo baada tu ya kamaliza chuo. Apewe mtihani na akifauku ndio aapishwe kuwa daktari hii itafanya wanafunzi wahakikishe wanajiandaa vizuri kuwa madaktari. Na mtu akiwa amesomea nje ya nchi basi Ili aweze kufanya internship ni mpaka awe amefanya mtihani utakaompa sifa ya kuwa daktari kwa kufaulu na kuapa.

Na kwa kuwa daktari huongezeka ubora wake kwa kufanya clinical au kwa kupractice, Daktari aendelee kupractice wakati wote hasa baada tu ya kumaliza internship lakini hili la Sasa hivi la kusubiri mtihani huko ni kupoteza ufanisi wa Daktari kwa kuwa alazimika asubiri mtihani huku akitafuta pesa ya chakula na pango kwa kufanya ujasiriamali.
Hapo kuna sentensi imeomba kufutwa kwa mtihani watu wamalizapo internship wapewe leseni kama hapo awali
Pakua hizi
Hiyo barua yenu mbona ina typographical errors kibao hadi inatia shaka hata mnachokipigania wataona kama nyie ndio mna tatizo je hamkuwa na mtu wa kufanya proofreading before hamjasubmit?
 
Mnafaulu wengi sana, inabidi wawakazie kama Law School. Intake moja wafaulu watu 22 au 25 tu kati ya hao 600.
 
Kwanini hao wengine wamefaulu nyie mmefeli?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Wamefaulu kwa sababu waliokuwa na nafasi ya kujisomea, Ili uweze kufaulu mtihani wao basi ni lazima upuuze practice. Kama ukiamua kuacha kuasaidia wagonjwa wakati wa internship, ukiamua kukwepa kufanya clinical rotations wakati wa internship na kutokuzingatia kukutana na wagonjwa na kuwawekea maana na nguvu zako ukaziamishia kwenye kujisomea utafaulu. Elewa hivi, wakati wa internship ndio wakati pekee wa daktari kukuza uwezo wake wa kutibu. Kwa Daktari mwenye upendo na taaluma yake atalazimika ajikitete kweli kweli kwenye kuhudumia wagonjwa akiwa na jopo la madaktari Ili aweze kuwa bora ndio sababu utasikia kunamadaktari wanalala hospitalini, hao ni internship wanaopemda kujua kutibu. Wakati wa internship ni wakati wa kujifunza kupractice nasio wakati wa kujisomea Ili ukimaliza tu in internship ukafanye mtihani. Ni vyema ukaelewa hoja ya madaktari sio kukataa kufanya mtihani ila mtihani ufanyike kwa wakati sahihi sio wakati wa practical uletewe theory Ili hali ulikuwa ukipractice. Kwa upande wa taaluma ya udaktari huwa kuna shuke ya Clinical/practical na ya theory, Sasa uhuni wa MCT ni kuleta mtihani wa Theory wakati watu wametika kupractice. Sasa Ili ufaulu theory yao utalizimika usiwe Bora katika kujua kutibu maana ukijikita kujifunza kutibu na kuisaidia wagonjwa basi utakosa muda wa kujisomea na ukimaliza tu mtihani wao huu hapa na hivyo huts weza kufaulu kwa sababu ulikuwa busy kujifunza na kusadia kutibu wagonjwa. Watu wanaofaulu ni wale wanaopata muda wa kujisomea, wengine wanabahatika wakimakiza internship wanapata muda wa miezi miwili kujisomea wengine hapatati kabisa na wengine wanajikuta wanafanya ujasiriamali kwa miezi 8 ndipo mtihani unamfikia na ukimfikia anajikuta kichwani aubobezi wa ujasiriamali kwa sababu hakupewa nafasi ya kuendeleza ufanisi wa taaluma yake
 
Tusilete siasa kwenye mambo ya msingi. Restructuring ya MCT inatakiwa Yes, lakini na wao wanafunzi wasome kwa bidii wafaulu hio mitihani.
 
Hao waliofaulu pepa walikuwa wanakaa 8hrs hospital? Pepa za leseni nmepitia vzr most of questions ni vile vitu unavyopractice ukiwa internship.
Nachoweza kusema labda ni MCT wafanye kusimamia vyuo ili vitoe elimu yenye standard bas. Ila hoja ya kufuta license examinations siungi mkono.
Hatuungi wala hatusemi mtihani ufutwe, mtihani ujue nyakati na mtihani ufanyike baada ya mtu kumaliza chuo na si vinginevyo. Muda sahihi kwa mtihani wa MCT ni baada tu ya mitihani ya chuo na kabla mtu ajaapa kuwa dakatari
 
Mheshimiwa Rais,
Amani iwe nawe daima.

Mheshimiwa Rais, Awali ya yote tunakupa pole kwa kazi zako za kila siku za kuhudumia Watanzania, huku tukiamini Mwenyezi Mungu anaendelea kukujalia afya tele na tunatambua pia una majukumu mengi kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Rais, hii ni sauti ya Umoja wa Madaktari wahitimu watarajali ambao tunaleta kwako waraka huu kwa lengo la kukufikishia ujumbe kutokana na vikwazo vinavyotukabili ambavyo vimetufanya kugeuka ombaomba mtaani licha kwamba sisi ni wasomi madaktari ambao tumeshindwa kujiajiri, kuajirika kutokana na kizingiti kinachoitwa leseni.
Mheshimiwa Rais, tumeamua kuleta waraka huu kwako baada ya juhudi zetu za kupeleka changamoto zetu na hata kuonana na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya kugonga mwamba.

Mheshimiwa Rais, Tumekuwa kwenye mazoezi ya vitendo (internship) katika hospitali kubwa za rufaa nchini, huko kazi zote na za aina zote tumekuwa tukizifanya sisi na kusimamiwa na madaktari bingwa nchini.Huko tumeokoa maisha ya Watanzania wenzetu wengi, tumejipatia umahiri wa kuhudumia wagonjwa kwa uwezo wa elimu tuliyonayo.

Mheshimiwa Rais, Sisi madaktari wa utarajali tunashangazwa na kuumizwa na utaratibu wa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) pamoja na Wizara ya Afya, kwa kadhia kubwa wanayotusababishia.
Sisi madaktari watarajali tunaamini Serikali ilikuwa na nia njema ilipoamua kutunga Sheria No.11 ya Mwaka 2017 ambayo ilipitishwa na Bunge letu Tukufu ikitaka kila Mhitimu wa fani ya Udaktari sharti apewe leseni baada ya kufanya mtihani wa MCT.
Mbali na nia hiyo njema ya Serikali, bahati mbaya chombo hiki hakijaweza kujua kifanye kazi ipi na kwa wakati upi ili kiweze kulisaidia taifa lipate madaktari bora na sio bora madaktari.

Mheshimiwa Rais, hatuipingi sheria hiyo isipokuwa utaratibu au kanuni zinazotumika, hususan kuanzishwa kwa mtihani wa ‘pre na post internship. Baraza hili (MCT) limekuwa likiendesha mitihani hiyo kwa hasara, uonevu, ukatili na hujuma kwa madaktari watarajali.
Ikumbukwe kwamba sisi madaktari Watarajali hatupingi kuwapo kwa mitihani hiyo ikizingatiwa tumemaliza vyuo pamoja na kufanya mazoezi kwa vitendo (internship) na kupata ufaulu usiotiliwa shaka.

Tunachokipinga na ambacho kimetufanya kuandika waraka huu kwako Mheshimwa Rais ni haya yafuatayo:

1. Mtihani wa baada ya utarajali (post internship) uliofanyika 22/03/2023 kumekuwa na massive failure kiasi ambacho hadi imesababisha Baraza kutokutoa takwim za waliofeli na waliofaulu ingawa mpaka sasa tupo madaktari zaidi ya 300 ambao matokeo hayakutoka vizuri hivyo kushindwa kupatiwa leseni, hivyo tunaomba mtihani huu usahihishwe upya na matokeo yafanyiwe standardization, na usahihishwe na wasimamizi wa nje ya MCT (external examiners) ili kuondoa hii massive failure kama ilivyotokea matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 mitihani ilisahihishwa upya na ufaulu ukapatikana
2. MCT kutokuzingatia uhalisia wa namna ya kumpata daktari bora
3. MCT kutumia mtihani kwa lengo la kuondosha changamoto za ulevi uliopitiliza kwa baadhi ya madaktari, kuchelewa kazini au kutokufika kazini pamoja na uzembe kazini
4.MCT kutokuzingatia muda wa daktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kwenda kufanya kazi ili kulihudumia taifa.
5. MCT kutokuzingatia namna sahihi ya kumpima daktari kulingana na huduma zinazotolewa katika hospitali tunazofanyia internship

6. MCT kutokujali na kuheshimu muda jambo linalopelekea daktari kutaka hatari ya kupoteza taaluma yake kwa kusubiri mtihani kwa muda mrefu wakati mwingine kwa miezi takribani 10.
7. MCT kutokuwa wawazi juu ya alama (marks) za ufaulu na uendeshaji mzima wa mtihani na matokeo utakaomfanya mtu ajue amefeli idara ipi hata baada ya kukata rufaa.
8. MCT kutokuheshimu na kuzingatia muda tunaopaswa kumaliza taaluma ya udaktari.

Ushauri na mapendekezo yetu.

1. Yafanyike marekebishio ya sheria ili iweze kuakisi upatiakanaji wa madaktari bora.
2. Wizara ifuatilie mapungufu yaliyopo MCT na itumie dhamana yake kuwawezesha madaktari wapate leseni ili washiriki ujenzi wa taifa lao.

3. Wizara itoe leseni baada ya madaktari kumaliza mazoezi kwa vitendo (internship) na kufaulu vizuri kwa kuzingatia taarifa ya hospitali ambayo daktari amefanya mazoezi kwa vitendo (internship).
4. Tunashauri kusiwepo na mtihani wa leseni, kuwepo na mtihani wa kumpima mwanafunzi kama ana uwezo wa kuwa daktari bora baada ya kumaliza mitihani ya chuo na kabla ya kuapa au kwenda mazoezi kwa vitendo (internship). Hii itapelekea ufaulu mzuri kwa sababu ya mtu kuwa na muda wa kutosha kujiandaa na watakaotakiwa kurudia mtihani warudie kila baada ya miezi miwili katika kituo kimoja ili kuepuka gharama kubwa. Hii itapelekea milango ya hujuma, rushwa, uzalilishaji na uonevu anaoupata daktari wakati wa kusubiri mtihani kutoweka.
5. Mtihani wa kumpima mwanafunzi ili aweze kuwa daktari utungwe kama inavyofanyika vyuoni, mtihami wa kuchagua (multiple choice) wa maswali 100 au 200 pekee hauwezi kuwa kielelezo cha kumpata daktari bora kama ilivyo sasa.
6. Kuwepo na muda rafiki wa kukata rufaa walau kuanzia mwezi mmoja.
7. Kwakuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC), hivyo tunapendekeza itumie mifumo inayotumiwa pia na nchi wanachama ambapo wahitimu wa udaktari wanapewa mtihani online na kwa muda wowote. Nchi zote wanachama wa EAC zenye utaratibu wa kufanya mitihani ya leseni, mtihani na alama (marks) zake zinajulikana na zipo kwenye website zao isipokuwa Tanzania tu ndiyo alama za ufaulu hazijulikani.

Mheshimiwa Rais, sisi madaktari watarajali tumesoma kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu na kumalizia mwaka mmoja wa mafunzo ya vitendo (internship) na tumefaulu vizuri sana hadi kufikia ngazi ya utabibu, ni nani leo anaweza kusema sisi sio wasomi? Ni nani anayeweza kusema kuwa sisi sio madaktari ili hali tumetibu wagonjwa mwaka mzima na kutunukiwa vyeti vya ufaulu wa alama A ?

Mheshimiwa Rais, ni ukweli kwamba Taifa letu linahitaji madaktari bora, lakini je madaktari bora wanaweza kupatika kupitia maswali 200 ya mtihani wa kuchagua kwa muda wa saa tatu mpaka sita pekee?

Mheshimiwa Rais, kutokana na kadhia ya namna hii huenda Wizara yenye dhamana na afya haiviamini vyuo vyake vilivyopo nchini, hivyo wanaona suluhisho pekee la kupata madaktari bora ni huo mtihani wa saa 3 mpaka sita ambao utaratibu wake umekuwa kikwazo kwa daktari ambaye tayari alikwisha kula kiapo kujiajiri au kuajiriwa katika sekta zote, yaani umma na binafsi.

Mheshimiwa Rais, swali la kujiuliza na lipo kwa Watanzania wengi kama ambavyo walivyoaminishwa na MCT ni hili, Je ni kweli sisi madaktari ni waoga wa mtihani na hatutaki kufanya mtihani wa kujipima wa MCT? Jibu ni hapana!
MCT wanapaswa watoe leseni kwa kila daktari aliyefaulu mazoezi kwa vitendo kwakuwa moja kwa moja ana sifa za kuwa na leseni kwa sababu amekutana na wagonjwa, amewatibu, wamepona na amefanikiwa kuokoa maisha ya watu.

Mheshimiwa Rais, tunasisitiza hatupingi mtihani wa kupata leseni, tunashauri uwepo isipokuwa uende sambamba na mitihani ya kumaliza vyuo na si unaompima daktari baada ya mazoezi kwa vitendo. Utaratibu wa sasa ujulikane ni batili, hivo tunaomba standardization ifanyike na tupatiwe leseni

Mheshimiwa Rais, tunashauri Serikali ipitie upya Sheria ya mitihani ya mwaka 2017 ili kuwepo na utaratibu mzuri usio na malalamiko mengi na kuwepo uwazi wa kutosha.

Aidha tunashauri vyuo vya udakitari viwe chini ya Wizara ya Afya na sio Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ili waweze kuvisimamia vizuri viweze kutoa wataalam wazuri wa afya.

Tunakushukuru sana.
Kupitia kwako ni matumaini yetu maombi yetu yatapata ufumbuzi wako wewe Rais wetu na Mama yetu mpendwa.
Mtihani unaokuwa na massive failure kwa watu wanaofanya kazi kama interns wa udaktari unamaanisha failure ipo kwenye watoa mtihani.

Kati ya watu 300 kuna watu wa kila aina, kwa nini kuna massive failure?

Nchi yetu ina tatizo kubwa sana la kukosa madaktari, kwa mujibu wa World Health Organisation, kiwango cha uwiano wa daktari mmoja kwa idadi ya watu anaowahudumia ni 1:8000, kwa Tanzania, uwiano huu ni 1:20,000 , karibu mara tatu zaidi ya kiwango kinachotakiwa, tunahitaji madaktari mara tatu zaidi ya tulionao, kwa nini wanabaniwa hivi? Maana mimi naona hii ni kuwabania tu. Hawa watu wamesoma Utabibu mpaka kufika hapo si vilaza. Kwa nini kuna massive failure?

Au ndio ule utamaduni wetu wa "wakifeli wengi ndiyo elimu inakuwa nzuri"?
 
Hatuungi wala hatusemi mtihani ufutwe, mtihani ujue nyakati na mtihani ufanyike baada ya mtu kumaliza chuo na si vinginevyo. Muda sahihi kwa mtihani wa MCT ni baada tu ya mitihani ya chuo na kabla mtu ajaapa kuwa dakatari
Una point mkuu, ikiwa mtihani unatolewa hivyo, basi unaelekea kudhalilisha kada ya udaktari.

Unatibiwa na mtu, halafu unaambiwa huyu kashindwa MCT, hutataka kumuona tena!

Matokeo yake unaenda kwa mganga wa kienyeji sasa.
 
Mkarudie mitihani na msome ,kama wanafaulu 300 kwenye 600 nawashauri wakaze zaidi hiyo idadi ni kubwa ,Law school wanafaulu 30,Afya zetu ni muhimu wakaze kweli kweli.
Rejea comments zote utajifunza kitu.
Kwanza ni vyema ujue huo mtihani hauna uwazi ukifaulu na ukifanyiwa hujuma huta jua. Dr Mzava anasema ukifeli umefeli na ukifaulu vizuri umefeli, Sasa Je huoni wanaofeli ni wale walio na uwezo mkubwa ila wamefeli kwa sababu ya uwezo wao mkubwa? Wewe unaachaje kuamini kuwa mtu akifeli mara ya kwanza, mara ya pili atajiandas kwa usongo na hivyo atafaulu vizuri na akifaulu vizuri kwa mujibu wa Dr Mzafa atafelishwa kwa mtihani kwa sababu watakuwa namashaka nae kwa nini amefaulu vizuri? Tena ukikata rufaa huta jua ni kwa nini umefeli...

Wengu wamefaulu kwa sababu waliokuwa na nafasi ya kujisomea, Ili uweze kufaulu mtihani wao basi ni lazima upuuze practice. Kama ukiamua kuacha kuasaidia wagonjwa wakati wa internship, ukiamua kukwepa kufanya clinical rotations wakati wa internship na kutokuzingatia kukutana na wagonjwa na kuwawekea maana na nguvu zako ukaziamishia kwenye kujisomea utafaulu. Elewa hivi, wakati wa internship ndio wakati pekee wa daktari kukuza uwezo wake wa kutibu. Kwa Daktari mwenye upendo na taaluma yake atalazimika ajikitete kweli kweli kwenye kuhudumia wagonjwa akiwa na jopo la madaktari Ili aweze kuwa bora ndio sababu utasikia kunamadaktari wanalala hospitalini, hao ni internship wanaopemda kujua kutibu. Wakati wa internship ni wakati wa kujifunza kupractice nasio wakati wa kujisomea Ili ukimaliza tu in internship ukafanye mtihani. Ni vyema ukaelewa hoja ya madaktari sio kukataa kufanya mtihani ila mtihani ufanyike kwa wakati sahihi sio wakati wa practical uletewe theory Ili hali ulikuwa ukipractice. Kwa upande wa taaluma ya udaktari huwa kuna shuke ya Clinical/practical na ya theory, Sasa uhuni wa MCT ni kuleta mtihani wa Theory wakati watu wametika kupractice. Sasa Ili ufaulu theory yao utalizimika usiwe Bora katika kujua kutibu maana ukijikita kujifunza kutibu na kuisaidia wagonjwa basi utakosa muda wa kujisomea na ukimaliza tu mtihani wao huu hapa na hivyo huts weza kufaulu kwa sababu ulikuwa busy kujifunza na kusadia kutibu wagonjwa. Watu wanaofaulu ni wale wanaopata muda wa kujisomea, wengine wanabahatika wakimakiza internship wanapata muda wa miezi miwili kujisomea wengine hapatati kabisa na wengine wanajikuta wanafanya ujasiriamali kwa miezi 8 ndipo mtihani unamfikia na ukimfikia anajikuta kichwani aubobezi wa ujasiriamali kwa sababu hakupewa nafasi ya kuendeleza ufanisi wa taaluma yake
 
Wamefaulu kwa sababu waliokuwa na nafasi ya kujisomea, Ili uweze kufaulu mtihani wao basi ni lazima upuuze practice. Kama ukiamua kuacha kuasaidia wagonjwa wakati wa internship, ukiamua kukwepa kufanya clinical rotations wakati wa internship na kutokuzingatia kukutana na wagonjwa na kuwawekea maana na nguvu zako ukaziamishia kwenye kujisomea utafaulu. Elewa hivi, wakati wa internship ndio wakati pekee wa daktari kukuza uwezo wake wa kutibu. Kwa Daktari mwenye upendo na taaluma yake atalazimika ajikitete kweli kweli kwenye kuhudumia wagonjwa akiwa na jopo la madaktari Ili aweze kuwa bora ndio sababu utasikia kunamadaktari wanalala hospitalini, hao ni internship wanaopemda kujua kutibu. Wakati wa internship ni wakati wa kujifunza kupractice nasio wakati wa kujisomea Ili ukimaliza tu in internship ukafanye mtihani. Ni vyema ukaelewa hoja ya madaktari sio kukataa kufanya mtihani ila mtihani ufanyike kwa wakati sahihi sio wakati wa practical uletewe theory Ili hali ulikuwa ukipractice. Kwa upande wa taaluma ya udaktari huwa kuna shuke ya Clinical/practical na ya theory, Sasa uhuni wa MCT ni kuleta mtihani wa Theory wakati watu wametika kupractice. Sasa Ili ufaulu theory yao utalizimika usiwe Bora katika kujua kutibu maana ukijikita kujifunza kutibu na kuisaidia wagonjwa basi utakosa muda wa kujisomea na ukimaliza tu mtihani wao huu hapa na hivyo huts weza kufaulu kwa sababu ulikuwa busy kujifunza na kusadia kutibu wagonjwa. Watu wanaofaulu ni wale wanaopata muda wa kujisomea, wengine wanabahatika wakimakiza internship wanapata muda wa miezi miwili kujisomea wengine hapatati kabisa na wengine wanajikuta wanafanya ujasiriamali kwa miezi 8 ndipo mtihani unamfikia na ukimfikia anajikuta kichwani aubobezi wa ujasiriamali kwa sababu hakupewa nafasi ya kuendeleza ufanisi wa taaluma yake
Maelezo mengi ya nini?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Utitiri wa vyuo vikuu binafsi unatuzalishia madaktari vilaza na hatari kwa maisha yetu. Wao lengo lao ni kutengeneza pesa, ada sh 10m kwa mwaka etc. Hivyo mitihani ya kitaifa kupitia MCT ni muhimu na ni bora vikawa kila mwaka wa masomo huko vyuoni, written and practical/ clinical
 
Una point mkuu, ikiwa mtihani unatolewa hivyo, basi unaelekea kudhalilisha kada ya udaktari.

Unatibiwa na mtu, halafu unaambiwa huyu kashindwa MCT, hutataka kumuona tena!

Matokeo yake unaenda kwa mganga wa kienyeji sasa.
Kinachoendeka leo nchini ni udhalilishaji mkubwa wa madaktari, tatizo watanzania wengi hawajui kada hii ya udaktari ndio sababu tunamuomba rais aingilie kati na atume nafasi tueleze mambo mengi ya ajabu ambayo ni aibu kuyaainisha hapa.

MCT wanadhakikisha madaktari na waadhalilisha Madaktari Bingwa wa hapa nchini kwetu. Ili mtu awe Daktari ni lazima aidhinishwe na madaktari Bingwa wasiopungu 50. Hawa ndio wanaompima dakatari anapokuwa internship na hawa ndio wanaosema huyu Daktari amefaulu vizuri idara yetu ya upasuaji na Sasa aende idara ya watoto, Daktari hata weza kwenda idara ya watoto kama idara ya upasuaji hakufanya vizuri, madaktari bingwa kila idara ndio wanaomfundisha, kumsaidia na kuuona uwezo wa Daktari katika idara na hao ndio wanaweza kumuongezea siku Daktari za kubakia katika idara yao baana ya kutambua kuwa bado hajawa na ufanisi Bora katika upasuaji. Mwisho wa kuzunguka idara zote na kufanya vizuri Madaktari bingwa ndio wanakutunuku cheti cha ufauruji wako wakithibitisha kwa Dunia yote kuwa wewe daktari Sasa unaweza kutibu, ajabu ni pale MCT anatunga mtihani bila kujua autoe lini harafu anasema huyu hawezi kutibu wakati alipokuwa ok internship ameokoa maisha ya watu wengu. Huko ni kuwadhalilisha madaktari na madaktari bingwa wa Tanzania yetu pendwa
 
Mkarudie mitihani na msome ,kama wanafaulu 300 kwenye 600 nawashauri wakaze zaidi hiyo idadi ni kubwa ,Law school wanafaulu 30,Afya zetu ni muhimu wakaze kweli kweli.
Huelewi, tafuta kuelewa na usilinganishe mafuta na maji eti kwa sababu vyote ni vimiminika. Ogopa sana kama hujuma itatawala kwa madaktari. Sikikiza na uelewe hoja za Madaktari kisha Pinga hujuma za MCT
 
Hawa ndio wafaulu wa D, yaani junior Dokta apewe leseni ya kufanya kazi bila ya kusimamiwa wakati research zinaonyesha asilimia kubwa ya ‘medical errors’ chanzo chake ni new medics.

Huko ni sawa na kutoa kibali cha kwenda kudhuru watu huko mitaani au sijui wapi wanapotaka kwenda.

Given the amount of public outcry on negligence sina shaka ukienda Muhimbili hawana utaratibu wa ku record medical errors zilizosababisha madhara na pengine kupoteza maisha ya watu unnecessary ili waboreshe intervention zao na kupunguza hizo risks.

Huko madongo poromoko kwengineko vifo vya uzazi or during minor operations ni kawaida kabisa and they don’t see that as a problem huko wizarani; bado unaongelea medical error in drug prescriptions ambalo ndio kubwa zaidi leo ukawape vibali interns wakajifanyie practice wenyewe.

Akili zao zinawatosha wenyewe hao vijana walioandika hiyo barua.
Reja hoja za Madaktari na Rejea barua zote ninazokuwekea hapa, Mtihani wa MCT hauna ufumbuzi wa hayo unayoyasema. Mtihani wao ni hujuma. Ni hujuma kwa sababu madaktari wametibu watu na kuisaidia kurejesha afya za watu . Hawa madaktari tunaowaongelea hawata hizo changamoto ulizoziainisha na changamoto hizi hawahusiki nazo na zingewahusi wasingekuwa hapo wangekuwa wamerudia Clinical rotations na wengine wanngeshitakiwa. Changamoto ulizozianisha zinatokana na uzembe na uzembe hauwezi kutatukiwa na mtihani wa MCT. Rejea comments zingine. Soma hizo nilizo zi attach. Soma zote bila uvivu.
 
Attachments

Hao waliofaulu pepa walikuwa wanakaa 8hrs hospital? Pepa za leseni nmepitia vzr most of questions ni vile vitu unavyopractice ukiwa internship.
Nachoweza kusema labda ni MCT wafanye kusimamia vyuo ili vitoe elimu yenye standard bas. Ila hoja ya kufuta license examinations siungi mkono.
Unaongea Yale Yale na unatakiwa kujua hizo 8hrs ni kwa hospital ipi? Hospital zote za Rufaa kasoro MOI wanawategemea internship kila kitu na kila wakati. Mtingo wa internship ni zaidi ya sounds watu wanatinga masaa 20 harafu wewe unasema 8. Harafu hakuna Daktari anaeweza kuwa bora kwa hospital zetu kwa kutinga masaa 8 wakati wa internship. Hii ndio sababu wanaofanyia MOI wanazingua ila kwenye mitihani ya theory wanaweza sana kwa sababu wana muda sana wa kuhisomea
 
Ila madaktari wa siku hizi wanafikirisha sana, mtu unamwelezea matatizo yako ye yuko bize na memes
Sasa hili haliwezi kudhibitiwa na mtihani wa theory wa MCT ndio sababu tunataka matatizo haya yatafutiwe njia sahihi ya kuyatatua na sio mtihani wa MCT
 
Hao wasipoteze muda, wawahi nafasi za masomo VETA.
Ni vyema ukaweka mizaha pembeni, kada hii ni muhimu sana kama sio Leo kesho utakutana na daktari, tafuta kuelewa changamoto walizo nazo na uwasaidei kusema Ili waweze kukuza ufanisi wao kesho ukikutana nao waweze kukuhudumia vyema
 
Wazee wengi wana asili ya uchawi, hawataki kada zao ziwe na watu wengi ili waendelee kujiona special. Kada zinazoumia zaidi kwa wazee wachawi ni hizi

1.) Architecture (kada yangu) - Miaka mitano degree

2.) Udaktari - Miaka mitano degree

3.) Sheria - Miaka mitano hadi Law school
Haiwezekani huyu mtu kahitimu degree baada ya kusota miaka mitano, kafanya internship mwaka mzima bado hutaki kumthibitisha kufanya kazi za udaktari kwa kumwekea kamtihani kamoja ka mtego, hii ni kuwahujumu hawa vijana na kuwapotezea uwelekeo wa maisha bila sababu za msingi.

Sina hakika kama kwa sasa madaktari wanatosha nchi hii na Kwa mambo kama haya vijana watakwepa kusomea udaktari na kuongeza tatizo la ukosefu wa madaktari kuwa kubwa zaidi.​
 
Nimesoma kuanzia juu hadi nilipofikia hapo uliposema mitihani isahihishwe upya halafu ifanyike standardization nikaacha.

Afya ya mtu haina standardization. Tatizo vyuo vya afya siku hizi vimekuwa vingi.

Matangazo kibao ya vyuo vya afya.Utasikia chuo kipo ghorofa ya sita jengo fulani...... Kweli?
Endelea kusoma, lakini pia MCT wana usiri mkubwa na hawana Marks za kueleweke. Emu soma na pita hizi attachment chini. Kinachotafuta na madaktari ni walau wapate leseni maana kama uweza wa kutibu wanao mkubwa Sasa hizo zingine zinaitwa ombaomba
 
Attachments

Back
Top Bottom