Madaktari wengi ni misukule walio hai

Madaktari wengi ni misukule walio hai

Nikizungumza daktari, kwa muktadha wa kitanganyika, namaanisha watu wote wanaojiita wataalamu wa sayansi ambao kimsingi wala sio wataalamu, wengi wao wana diploma za D mbili kisha wakaunga unga mpaka Kairuki University au Bugandooh kisha wakavaa makoti meupe wakaanza kujiita madaktari na wanasayansi.
Na Sisi wenye Master za Mchongo vipi 🤣🤣🤣
Tuliozipata Canada na Brazil😅😅
 
Jamaa ana pointi kwenye alichoandika lakini si kwa madaktari tu.., ni kada zote tunaishi kama misukule... Elimu inayotolewa na serikali si elimu yetu ni ya wazungu ya kutufanya tuwe watumwa au misukule unayosema. Misukule kwenye nyanja zote, jinsi ya kula, kunywa, kuvaa, tiba, etc etc
 
Nimetumia neno msukule kwa makusudi maalumu. Msukule sio tusi ni nomino, ni jina la mtu aliyetekwa nyara kiroho na kupotezwa kimazingara.

Kwanini madaktari ni misukule? Nitafafanua kwa ufupi na kwa kiwango kinachoeleweka.

Madaktari wengi akili zao zimefungwa minyororo, hawana wazo huru, wala hawana ujuzi huru. Wamebeba furushi la elimu ya kukaririshwa na kumezeshwa kama makinda ya bundi-mwitu.

Nikizungumza daktari, kwa muktadha wa kitanganyika, namaanisha watu wote wanaojiita wataalamu wa sayansi ambao kimsingi wala sio wataalamu, wengi wao wana diploma za D mbili kisha wakaunga unga mpaka Kairuki University au Bugandooh kisha wakavaa makoti meupe wakaanza kujiita madaktari na wanasayansi.

Kiukweli wako mbali sana na sayansi. Hawaijui wala hawaielewi sayansi. Ukimuuliza daktari wa kitanganyika kwanini kansa haina dawa anakwambia kansa haina dawa kwa sababu mabeberu hawajaleta chanjo.

Mfumo mzima wa daktari wa kitanganyika umejengwa katika muhimili wa kukariri na kusubiri maagizo ya mabeberu.

Beberu likiamuru kwamba kansa haina dawa basi ujue daktari wa kitanganyika hapindui meza. Ni mwendo wa kansa haina dawa hadi pale beberu litakapoamua vinginevyo.

Huu ni msukule wa kitanganyika katika mavazi meupe. Akili imefungwa minyororo ya chuma.

Corona ilituaibisha. Wanasayansi wetu wa kitanganyika walijificha uvunguni wakisubiri kuokolewa na mabeberu. Alhamdulillah mabeberu wakatutupia magunia ya chanjo tuyafakamie tupendavyo.

MY TAKE: Madaktari wote wafutiwe leseni zao wakawe wachimbaji wa kawaida wa mitaro ya barabara.

Umesahau misukule mingine ni mifamasia hii mijamaa,inachajua ni kupanga dawa kwenye shelves na kugawa dawa tu,ukiiambia itengneze dawa hata ya kutibu mafua haiwezi,hovyo kabisa.

Daktari pekee angalau ni yule anayefanya upasuaji wengine wote ni misukule.
 
Inaonyesha una dharau sana na taaluma za watu
Lakini inaonyesha taaluma hio unayoizungumzia huijui na wala haikuhusu ndio maana unaropoka ropoka tu
Misukule hutengenezwa kwa mifumo ya mwanga au mchawi ambaye ndio huendesha taratibu zote

Na kama umeona madaktari ni misukule basi wametengenezwa na serikali
Mikakati ya serikali kuboresha mafunzo kwa watoa huduma za Afya Tanzania inaionaje?
Vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu katika kugundua magonjwa na matibabu vipo?

Usiongee upumbavu na kukashifu watoa afya wakati ndugu zako , wewe na familia yako mnawategemea hao hao ambao mnawaona misukule

Watoa afya wanategemea beberu aseme nini ndio wafanye huoni hao ni misukule mtu kati.
 
Masters za kupasua vibofu na viwiko.
Ila ngoja nikusahihishe kidogo kila Daktari na Fani yake kuna wanaodeal na Cancer wanaitwa Oncologists..
Sasa huwezi kumwambia Daktari anayedeal na Wanawake (Gynacologists) au wa Watoto Pediatrician....

Afanye kazi anazofanya Oncologists..

Ndiyo anaweza akafanya kwa sababu amewagi kuwa (GP) General Practi..au MD ila haina maana atafanya kila kitu anachotakiwa kufanya oncologists na ndio maana kuna Rufaa kwa magonjwa mbalimbali
 
Nimetumia neno msukule kwa makusudi maalumu. Msukule sio tusi ni nomino, ni jina la mtu aliyetekwa nyara kiroho na kupotezwa kimazingara.

Kwanini madaktari ni misukule? Nitafafanua kwa ufupi na kwa kiwango kinachoeleweka.

Madaktari wengi akili zao zimefungwa minyororo, hawana wazo huru, wala hawana ujuzi huru. Wamebeba furushi la elimu ya kukaririshwa na kumezeshwa kama makinda ya bundi-mwitu.

Nikizungumza daktari, kwa muktadha wa kitanganyika, namaanisha watu wote wanaojiita wataalamu wa sayansi ambao kimsingi wala sio wataalamu, wengi wao wana diploma za D mbili kisha wakaunga unga mpaka Kairuki University au Bugandooh kisha wakavaa makoti meupe wakaanza kujiita madaktari na wanasayansi.

Kiukweli wako mbali sana na sayansi. Hawaijui wala hawaielewi sayansi. Ukimuuliza daktari wa kitanganyika kwanini kansa haina dawa anakwambia kansa haina dawa kwa sababu mabeberu hawajaleta chanjo.

Mfumo mzima wa daktari wa kitanganyika umejengwa katika muhimili wa kukariri na kusubiri maagizo ya mabeberu.

Beberu likiamuru kwamba kansa haina dawa basi ujue daktari wa kitanganyika hapindui meza. Ni mwendo wa kansa haina dawa hadi pale beberu litakapoamua vinginevyo.

Huu ni msukule wa kitanganyika katika mavazi meupe. Akili imefungwa minyororo ya chuma.

Corona ilituaibisha. Wanasayansi wetu wa kitanganyika walijificha uvunguni wakisubiri kuokolewa na mabeberu. Alhamdulillah mabeberu wakatutupia magunia ya chanjo tuyafakamie tupendavyo.

MY TAKE: Madaktari wote wafutiwe leseni zao wakawe wachimbaji wa kawaida wa mitaro ya barabara.

Kiongozi;
Naomba nikusahihishe kuwa, hakuna kozI yoyote ya Afya inayopelekea kutibu mtu unayoweza kusoma ukiwa na Chini ya pass 4 zikiwemo Chem, Bio, Phy na Maths (na sio pass mbili kama ulivyo andika)
Lakini pia, Nikutoe wasiwasi kuwa, Nimefuatilia data za miaka ya hivi karibuni waliochaguliwa kusoma kozi hizo ngazi ya Diploma ni wale wanye pass za juu sana (Div ONE) na ninauhakika hakuna mwenye Chini ya Div 3 amechaguliwa kwenye chuo chochote hata huko Private.
Kuhusu magonjwa ya Virusi
Wale waliosoma PCB (Form Six) wanaelewa vizuri kwa nini ni vigumu sana kutengeneza dawa ya Ugonjwa unaosababishwa na Virusi, sidhani kama ni suala la udaktari; pengine ni mtu mwenyewe uliye ongea naye
By the way; Sio kIla anayevaa Koti Jeupe ni Dactari (MD) hata hivyo huwezi kufanya Research kwa kuongea na mtu mmoja au wawili halafu uiite research.....
Mwisho: Nikumegee tu kidogo kuwa, virusi vinatabia nyingi za kuonesha kuwa haviko hai na tabia chache za kuonesha kuwa vipo hai. Hivyo hutegemea kwa asilimia zote Cell ya kiumbe hai ili kuishi; sasa mara nyingi kuua kirusi/kutibu kirusi, inabidi uue cell ili kisipate pa kuishi ambapo ni karibia sawa na kuua kiumbe......matokeo yake mathara yanakuwa makubwa kuliko faida....hivyo tafiti mbalimbali bado zinaendelea.....
Mimi sio Dactari ila nilisoma hayo masomo yakanipa uelewa kiasi....
 
Kiongozi;
Naomba nikusahihishe kuwa, hakuna kozI yoyote ya Afya inayopelekea kutibu mtu unayoweza kusoma ukiwa na Chini pass 4 zikiwemo Chem, Bio, Phy na Maths (kwa hiyo ulicho andika sio sahihi)
Lakini pia, Nikutoe wasiwasi kuwa, Nimefuatilia data za miaka ya hivi karibuni waliochaguliwa kusoma kozi hizo ngazi ya Diploma ni wale wanye pass za juu sana (Div ONE) na ninauhakika hakuna mwenye Chini ya Div 3 amechaguliwa kwenye chuo chochote hata huko Private.
Kuhusu magonjwa ya Virusi
Wale waliosoma PCB (Form Six) wanaelewa vizuri kwa nini ni vigumu sana kutengeneza dawa ya Ugonjwa unaosababishwa na Virusi, sidhani hata kama ni suala la udaktari; pengine ni mtu mwenyewe uliye ongea naye
By the way; Sio kIla anayevaa Koti Jeupe ni Dactari (MD) hata hivyo huwezi kufanya Research kwa kuongea na mtu mmoja au wawili halafu uiite research.....
Divisheni one za shule za kata wala hazimaanishi kwamba kweli mtu ana kipaji au akili.

Hizi ni maksi tu za kitanganyika ambazo ni kinyume na uhalisia.

Ndio maana unamkuta daktari ana divisheni one lakini anakwambia kansa haina dawa kwa sababu beberu hajaleta chanjo.

Usiombe ukutane na mwenye D MBILI halafu kavaa STETHOSCOPE!!! Alooooohhhhh
 
Ila ngoja nikusahihishe kidogo kila Daktari na Fani yake kuna wanaodeal na Cancer wanaitwa Oncologists..
Hao oncologists kazi yao ni nini huko mahospitalini mbona kila ukienda wanakwambia kansa haina dawa??

Mimi nilifikiri kazi ya wataalamu ni kutoa suluhisho, kumbe kazi yao ni kukueleza kwamba jambo fulani halina suluhu! Eboo!!

Sasa kama ni hivyo, ni bora waondoke hapo hospitali wakawe vibarua wa mashamba ya alizeti tupate mafuta mengi tuongeze uchumi wa taifa.
 
Divisheni one za shule za kata wala hazimaanishi kwamba kweli mtu ana kipaji au akili.

Hizi ni maksi tu za kitanganyika ambazo ni kinyume na uhalisia.

Ndio maana unamkuta daktari ana divisheni one lakini anakwambia kansa haina dawa kwa sababu beberu hajaleta chanjo.

Usiombe ukutane na mwenye D MBILI halafu kavaa STETHOSCOPE!!! Alooooohhhhh

Kuhusu Cancer hilo ni somo tofauti na linahitaji maarifa kulijadili
kwa kifupi tu; Cancer haisababishwi na wadudu ( Bacteria au Virusi).
Madactari watanisaidia ufafanuzi hapa
 
Misukile hyo hyo ndo inatibu ndugu zako wakapona na wakaamka vitandani hebu heshima hata kidogo jitihada zao kwenye kusaidia jamii na suala la ugunduzi Hilo hata usilaumu mana wengi wao toka wakiwa mwaka wa kwanza wa udaktari Hadi kuwa maprofesa elimu bado n Ile ile na n mfumo kila mtu ameukuta
 
Inaonyesha una dharau sana na taaluma za watu
Lakini inaonyesha taaluma hio unayoizungumzia huijui na wala haikuhusu ndio maana unaropoka ropoka tu
Misukule hutengenezwa kwa mifumo ya mwanga au mchawi ambaye ndio huendesha taratibu zote

Na kama umeona madaktari ni misukule basi wametengenezwa na serikali
Mikakati ya serikali kuboresha mafunzo kwa watoa huduma za Afya Tanzania inaionaje?
Vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu katika kugundua magonjwa na matibabu vipo?

Usiongee upumbavu na kukashifu watoa afya wakati ndugu zako , wewe na familia yako mnawategemea hao hao ambao mnawaona misukule
Mnapenda sana kujidekeza.

Hata mkipewa fedha na vifaa bado mambo yatabaki vile vile.

Shida sio vifaa wala hela, shida bongo zimelala.
 
Back
Top Bottom