Nafurahi sana kukuelimisha
BICHWA KOMWE -
Sasa Nisikilize..
Katika Kada ya Afya au Katika Matibabu..
Kuna sector Kuu Tatu au kuna Kada kuu tatu..
- Matibabu/Tiba
- Kinga
- Utafiti/Research/Study
Sasa Rafiki ni kwamba Kila sector inategemea nyingine japo zinafanya kazi kwa utofauti sana..
Matibabu/Tiba inahusika na Kuzuia magonjwa kutosababisha madhara zaidi kwenye mwili wa Binadamu (Baada ya mtu akishapatwa nayo) na pia kuzuia kifo na hii mara nyingi ndo watu huiiona kwa sababu iko Mahospitali na Bituo vingi vya afya.
Kinga hii inafanya kazi kwa ukaribu sana na hiyo ya kwanza ambapo Mtu huweza kuzuia Magonjwa kabla hayajatokea kwa Kutoa Dawa kinga kama Prophylaxis na hasa Chanjo (Ambazo najua wengi wanazo)..
Utafiti/Research/Study Hapa tunadeal sana sana na kufanya Reseaech kuhusu Magonjwa yaani Hapa mambo ya Epidemiology na Biostatistics sana kujua magonjwa yanatokeaje magonjwa haya yanapata watu gani na kwanini yawepate na yanaambukizwaje na hawa ndo wenye jukumu la kuingia maabara na kuja na suluhisho la matibabu au kutoa suluhisho la Chanjo kwa ajili ya Ugonjwa..
Sasa, Hivi vitengo haviingiliani japo vinafanya kazi kwa pamoja huwezi kuta Mtu wa chanjo anamwambia Mtu wa matibabu kwanini unatibu wakati mimi natoa chanjo ya huo ugonjwa?
Au mtu wa matibabu anawambia mti wa chanjo kwanini unatoa Chanjo wakati mimi natibu huu ugonjwa??
Kwahyo kitengo cha kinga hakiwezi kumwingilia kitengo cha matibabu japo watu wanaofanya kazi kwenye Kinga wanaweza kufanya kazi kwenye matibabu pia..
Sasa kulingana na Kazi yao hawa hupokea Mrejesho wa kimatibabu na Kikinga kutoka kwenye utafiti na kuufanyia kazi..
Ikumbukwe kwamba wanaofanya utafiti pengine wana elimu sawa na wanaofanya Tiba au kinga ila ni kuachiana majukumu tu..
Japo haiko Limited kwa yoyote anayefanya kazi kwenye Utafiti/tiba/Kinga kutofanya kazi za hao wengine na wengine nao hivyo hivyo likewise..
Wanaofanya kwenye Tiba huwa ni HOSPITALI,VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI..
wanaofanya Kwenye Kinga ni Chanjo,Vituo vya afya Kitengo cha kinga n.k
Wanaofanya Utafiti ni NIMR,na IFAKARA pia wanafanya
Sasa Tunapokosea ni kuchukua Swali la NIMR au IFAKARA kumuuliza Daktari anayefanya kazi Kwenye Kinga au Tiba badala ya kuuliza Daktari anayefanya kazi kwenye Utafiti
Karibu kwa maswali zaidi
BICHWA KOMWE -