Mtoa hoja alitaka kueleza jambo la ndani zaidi, ambalo watu wengi hatulioni.
Anae angalia mambo kwa nje, bila kuingia kwa ndani, ataona kuwa mtoa hoja, hana heshima, na shukurani.
Lakini yeye, amejaribu kuona mambo kwa ndani, na kuona makosa ya elimu yetu. Neno "makosa" hapa linamanisha kuwa, elimu haitakiwi kuwa hivi ilivyo.
Elimu yetu yote: sio tu, kwenye afya bali maeneo yote: ni elimu huduma. Inatuandaa kuwa "Watumiaji" badala ya "Waumbaji". Asili ya mtu, ni Muumbaji, na maana ya mtu, ni Muumbaji.
Makosa ya elimu yetu:
Mtu anasoma kwa ajili ya kuwa "Mtumiaji". Yaani mtu unasoma kwa ajili ya ujira, mshahara.
Angalia watu wetu wanaosoma: wale wanajiendeleza au kusomea zaidi, kwa maana ya obobevu katika taaluma fulani; au wale wanaojibidiisha kwenye kazi au ajira zao. Je, wanalenga nini? Ni nini wanatafuta katika hayo? Kusema ukweli, wanatafuta: Vyeo, na kupanda madaraja au mshahara.
Kwa hiyo, kilichomo ndani ya mtu ni kitu gani, yaani mtu anasoma kwa lengo gani? Elimu yetu inatufundisha kuwa kitu gani? Elimu yetu inatufundisha kuwa sisi au mimi ni nani?
Unakwenda kusomea ualimu au udakitari au uchungaji au upadiri, kwa sababu gani?
Tuna amini nini?
I think this is what the writer is trying to address.