Madaraka Nyerere: Kiongozi anamsifia Nyerere lakini hapokei simu zetu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa hayati Mwalimu Julius Nyerere amesema anasikitishwa na baadhi ya viongozi wanaokwenda kutembelea mji wa Baba wa Taifa na kutoa kauli mbalimbali za kumsifu mwalimu, lakini wakiondoka hawapokei tena simu zake.

Madaraka amesema si kila simu anayopiga ni simu ya kulia shida, bali kuna wakati anapiga simu kwa ajili ya mipango ya kuendelea kuyasema mazuri ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
 
#Repost azamtvtz
——

Habari | Augustine Mgendi
Mhariri | John Mbalamwezi
 
Kuna wakati sio lazima kupokea/kupiga simu,ndio maana kuna sms haijalishi ni nani au yupi.
Binadamu tumeumbwa tofaut itofauti ni vizuri tukavumiliana na sio lazima kuwaambia watu madhaifu ya wengine.
 
Hasa viongozi kwa nini hawapokei simu za madaraka, viongozi mshike simu mmeambiwa huko
Mudathiri Yahaya alishawapigia viongozi wa Azam wakawa hawataki kupokea simu, sasa shangilia yake ni kupokea simu maana sio Madaraka peke yake hio ipo kwa watu wengi sana sana sana wanapuuza hata Jambo linaloweza kuwasaidia wenyewe wanapuuza kupokea simu
 
Kuna wakati sio lazima kupokea/kupiga simu,ndio maana kuna sms haijalishi ni nani au yupi.
Binadamu tumeumbwa tofaut itofauti ni vizuri tukavumiliana na sio lazima kuwaambia watu madhaifu ya wengine.
Pokea simu wewe usipuuze unapopigiwa simu labda nyumba yako inaungua watu wanataka kukupa taarifa unapuuza ukifika nyumba imegeuka mkaa
 
Ni kweli kabisa,kwa upande wangu ni lazima nipokee simu.
Tatizo lipo kwa wenye daraja fulani la maisha kudhani kuwa kupokea simu sio lazima au kuwa na tabia za kubagua simu za watu wengine.
 
Hapo umesema vyema Mimi hata km namba ngeni ikipiga nikiwa mbali nikikuta missed call nafsi inanisuta lazima nimtafute nimalizane nae
 
Back
Top Bottom