mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Bob Marley tangu afariki imepita miaka zaidi ya 40 lakini familia yake bado wanakula bata kupitia loyarities na JIna la baba yao. Michael Jackson family, Tupac family, Kennedy family pia ni miongoni mwa wanufaika wa jina.
Tukija hapa nchini, Karume, Kikwete, Mwinyi. Hawa familia zao vizazi na vizazi hawatajua shida ni nini.
Babu yake Kikwete alikuwa ni Akida au Liwali wa Serikali ya kikoloni, Baba yake Kikwete alikuwa DC enzi za mwalimu, Jakaya mwenyewe sina haja ya kumuelezea, kijana wake tayari ni waziri si ajabu huko mbeleni akawa mtu mkubwa nchi hii.
Mchungaji Getrude Rwakatale alikomalia hilo jina la Rwakatare, Japo yeye ni mpogolo aliona aendelee na hilo jina la kihaya kwa sababu alijua wahaya wanapenda elimu na yeye akikuwa anawekeza kwenye shule, ilimsaidia sana, wahaya wengi wakipeleka watoto St. marys kwa imani ya kumuungisha biashara muhaya mwenzao, walikuja kugundua ni mpogolo too late.
Maisha ya familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere yako wazi sana, ni familia inayoishi maisha ya kawaida sana. Baba yao alikuwa muadilifu sana hakuwa mwizi
Si ajabu Makongoro kupewa cheo cha u RC akiwa na miaka 60+ huku wenzake wenye umri huo wakistaafishwa kwa cheo hicho hicho.
Lengo ilikuwa kuclear njaa ndogo ndogo kwenye familia na familia kuwa na mwakilishi serikalini.
Unaweza kudhani watoto wa Nyerere wamesusa kupambana na maisha ila kuna stori mitaani kuwa hawabebeki,wanaamka saa nne.
Wameshindwa kutumia jina la baba yao kuleta ushawishi.
Hiawa chawa wetu wakizazi hiki wangebahatika kuzaliwa kwenye hiyo familia tungekoma,wangekuwa mabilionea.
waamke usingizini wafungue hata mgahawa wauite Butiama au Nyerere hapo Dodoma ,Makongoro akae reception waone kutakavyojaa
au wabuni mradi wowote wa familia,sisi tuko tayari kuwachangia
kila mtu anajua kuwa wana njaa,baba yao hakuibia Taifa
Mungu fundi Mama Maria kuishi kwake miaka mingi ni faida kwa watoto,siombei ila ikitokea siku hayupo basi biashara imeisha,hakuna simu itapigwa au kupokelewa.