Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Uwezo wa kutoa msamaha Sheria ya 1984 Na.15 ib.9 45.-

(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:- (a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria; (b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum; (c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu; (d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________ 36 aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka utaratibu utakaofuatwa na Rais katika utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa ibara hii.

(3) Masharti ya ibara hii yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Zanzibar na kwa adhabu zilizotolewa Tanzania Zanzibar kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge inayotumika Tanzania Zanzibar, hali kadhalika, masharti hayo yatatumika kwa watu waliohukumiwa na kuadhibiwa Tanzania Bara kwa mujibu wa sheria.
 
  1. Kwanini hata katiba inamlinda asikosolewe?
  2. Kwanini chama chake cha CCM kinasimamia itikadi ya kumuadhibu vikali yeyote anayemkosoa rais?
  3. Kwanini vyombo vya dola huwashughulikia vikali wakosoaji wa rais? Akumbukwe Stan Katabalo, Ben Saanane na wengine....
  4. Neno lake ni sheria, maana yake akitoa maagizo ni sheria kamili
Kwa haya yanayoendelea ni dhahiri shahiri kuwa Rais wa Tanzania anamilikiwa na nafsi yake na walio kwenye taasisi ya urais. Tujiulize Watanzania, ni lini tutampata Rais wetu ambaye atakubali kukosolewa, kupingwa hata kuwajibishwa anapokuwa madarakani?

Ujinga wetu ndo mauti yetu
 
Uzuzu huu hata akiwekwa kangaroo pale magogoni atatawala nchi ya wasadikika
 
Mwenyekiti wa Chadema ni nani?

Sumu haionjwi!
Huyo mwenyekiti wa chadema si alishtakiwa na mwenyekiti wa CCM? Ana ubavu gani kwenye nchi hii?

Na alipoona kesi inaiacha uchi serikali akaona afute kesi....
 
Katiba ya sasa haikatazi kukosoa

Katiba mpya si mua40


Katiba Mpya ina redefine nchi. Kama Kenya walivyofanya, Sasa hivi usikii fujo baada ya uchaguzi. Baada ya kuamua Kuwa na Mahakama ya kilele ambayo itasikiliza kesi za uchaguzi Tena kwa uharaka.
 
Back
Top Bottom