Jimmy Santadio
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 466
- 134
Injinia,tunamhurumia mtu kwa matatizo ya kujitakia,awe anatoa au anaingiza,biashara hii haifai,na kuhusu kuchafuliwa,ni kadhia ambazo watz wanatoa ushuhuda wa kukumbana nazo kwenye viwanja vya ndege huko ughaibuni,pindi waoneshapo Pass za TANZANIA
Mkuu, kama umewahi kuishi ughaibuni utagundua kwamba Tanzania ni nchi ambayo duniani haijulikani kabisa, achilia mbali pasipoti ya Tanzania. Ughaibuni mtu yoyote anayesafiri na pasipoti ya nchi isiyojulikana au nchi za Afrika, husimamishwa na kuulizwa maswali ambayo wazungu hawaulizwi. Hili halitokei kwa Watanzania peke yake. Hata Wamalawi wanakutwa na kadhia hii.
Kitu kingine ambacho nimejifunza ughaibuni, Ingawa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, lakini Zanzibar inajulikana kuliko Tanzania. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Tanzania haijulikani. Wapo watakaobisha katika hili kwa sababu ukweli una tabia ya kuchoma choma na ndiyo maana haupendwi. Wazungu wengi watakuelewa upesi unatoka wapi kama ukisema unatoka Zanzibar kuliko ukisema unatoka Tanzania.
Mimi Mwenyeji wa Kunduchi Beach Dar-es-salaam, mara nyingi sana nimesema natoka Zanzibar ingawa sijawahi kwenda Zanzibar. Inaondoa maswali kibao,. Ukisema unatoka Tanzania, swali linalofuata ni "where the heck is that"?
Kwa hiyo usiwe na wasi kuhusu pasipoti ya Tanzania, haijulikani na mtu yoyote.