"Made in China 2025" Mpango wa China wa kujitegemea kiteknolojia wafikia asilimia 88

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
'Made in China 2025' ukipenda iite MIC25

Huu ni mpango kabambe wa serikali ya China wa miaka 10 (2015-2025). Ambapo China imepanga kufikia 2025 ijitegemee kabisa katika teknolojia za hali ya juu (high tech) na innovation.

Lengo ni kufikia the 4th industrial revolution (the integration of intelligent digital technologies into manufacturing and industrial processes)

Haikuwa kazi rahisi, ndani ya miaka 10 wanasayansi, engineers na programmers wa China wamepambana sana kutumia elimu na ujuzi wao kwa kufanya research ili wafikie innovation katika high tech licha ya vita vya kiuchumi na kiteknolojia kutoka Marekani.

Hii inaturudisha nyuma hadi mwaka 2015 ambapo raisi wa China Xi Jinping akiwa na miaka 2 tu tangu aingie madarakani, yeye na viongozi wengine wa CPC walipokuja na huu mpango.

MIC25 iligusa maeneo 260 ambayo yaligawanywa katika makundi 10 makuu:


1. The new generation of IT
2. High end numerical control machine tools and robotics
3. Aviation and aerospace equipment
4. Maritime equipment andhigh tech shipping
5. Advanced rail transportation equipment
6. Energy saving vehicles and NEVs
7. Power equipment
8. Agricultural machinery equipment
9. Medicine and medical devices
10. New materials

Ikiwa imebaki miezi 6 tayari China imefikia 88% ya malengo hayo. Hebu tuangazie kwa kifupi.

1. THE NEW GENERATION OF INFORMATION TECH (IT)

(a)5G tech
●Kwa upande wa 5G HUAWEI ndiyo ilikuwa kampuni ya kwanza kutumia 5G commercial chip mwaka 2019. Kwa sasa wameanza kuelekea kwenye 6G
●China is the world's largest 5G network
●Makampuni ya China HUAWEI na ZTE yameshikilia 60% ya kandarasi na uuzaji wa vifaa vya 5G sehemu mbalimbali duniani.


(b)Operating system

●Wakati simu nyingi zikitunia Android OS na Apple wakitumia IOS, HUAWEI walifanya mapinduzi wakati wa vita vya kiteknolojia na wakaja na Operating System yao iitwayo Harmony OS mwaka 2022.


(c)Semiconductors na integrated circuits [IC]

● China ikiwa mzalishaji mkubwa wa vifaa vya umeme duniani inahitaji sana chips na IC. Hivyo ili kuepuka kutegemea sana chips na IC kutoka nje, MIC25 plan imeweza kuifanya kampuni ya kutengeneza chips na IC ya SMIC kuwa ya tatu kwa ukubwa duniani kwa utengenezaji wa chips na IC na ya tatu kimapato nyuma ya Samsung na TSMC ya Taiwan.

Kwa sasa wanafanya mass production ya chips za 7nm na wameanza kuunda chips za 5nm wakishirikiama na kampuni tanzu ya HUAWEI iitwayo HiSilicon. Now they are working on 3nm chips.


(f)Industrial software, and smart manufacturing
●Badala ya kutegemea software za kutoka nje hasa nchi za Magharibi, MIC25 imewezesha kampuni za ndani kutengeneza software. Kwa sasa software zilizotengenezwa China zimeshika 70% ya soko la ndani.

Kufikia 2022, kuna zaidi ya makampuni 35,000 ya software.

Notable Companies in the Software Development in China industry:
1. Huawei Technologies Ltd,
2. Alibaba Group Holding Limited,
3. Neusoft Corporation
4. Haier group,
5. leit system Co.
6. Hangzhou Hikvision Digital Tech Co. Ltd


(g) Servers, desktop CPUs, solid-state drives, high-speed fiber optics, industrial operating systems and big data systems
●China ilizuia matumizi ya processor, database software na operating system za makampuni ya Marekani kama Intel, AMD na Microsoft Windows kwa matumizi ya serikali na mashirika makubwa ya mawasiliano ya China.

Lengo ni kuacha utegemezi wa kiteknolojia na kuzipa nafasi kampuni za ndani katika teknolojia ya hardware na software.

Notable domestic companies for computer processor:
1. Loongson
2. Zhaoxin

Notable domestic companies approved for desktop and server operating systems:
1. The Galaxy Kirin Linux
2. The Tongxin OS
3. Fangde OS

Notable domestic companies for database:
1. Alibaba Cloud's PolarDB
2. Tencent’s TDSQL



2. AVIATION AND AEROSPACE EQUIPMENT
(a)Aerospace
●Tiangong Space Station (TSS).
Hivi sasa kuna vituo viwili tu vya anga vinavyofanya kazi kikamilifu. Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) na Kituo cha Anga cha Tiangong cha China (TSS) kilichozinduliwa 2021.



●The global BeiDou satellite navigation system


Mfumo wa Satellite wa BeiDou wa China (BDS) ulizinduliwa rasmi 2022. Umetambuliwa kuwa wa kiwango kinachohitajika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO), na kuufanya mfumo huu kukubalika ulimwenguni kote kwa usafiri wa anga.

Una satellite 56 katika orbit, una ukubwa mara mbili wa mfumo wa GPS pia una zaidi ya monitoring stations 10.

BeiDou ni mojawapo ya mifumo ya satellite minne ya kimataifa, pamoja na GPS ya Marekani, GLONASS ya Urusi na Galileo ya Umoja wa Ulaya.


●Zhurong rover
Mwaka 2021 kifaa kiitwacho Zhurong kilitua sayari ya Mars kwa ajili ya exploration.



Chang'e - 6
In 2024 China lands probe Chang'e-6 on far side of the Moon, 1st country to reach there and collect rock samples there.



(b)Aviation
Mwaka 2023 COMAC walizindua ndege ya kwanza ya abiria kutengenezwa China, C919.



3. MARITIME EQUIPMENT AND HIGH TECH SHIPS
China inaongoza duniani ikifuatiwa na South Korea na Japan.

(a)China inaunda container ships, oil tankers ships, LNG ships na Ro-Ro ships





(b)Aircraft carriers
Kwa sababu ya advacement katika ship building China imeweza kuboresha jeshi lake la Navy kwa kutengeneza aircraft carriers na aina nyingine za meli vita bora kama type 055 destroyer.


China's first domestically aircraft carrier Shandong ilizinduliwa mwaka 2017


Fujian aircraft carrier imezinduliwa mwaka huu 2024. The largest carrier ever built outside of the United States


China's Type 055 destroyer best surface combatant in the world. (Ina new hypersonic missile YJ-21, area air defence HHQ-9, anti-ship YJ-18, anti-submarine YU-8)




(c)Super cruise ship
Mwaka 2023 China ikazindua cruise ship ya kwanza Adora Magic City na mwaka huu nyingine kubwa zaidi ya Adora iko dock, Shanghai ikiundwa.


4. ENERGY SAVING VEHICLES AND NEVs
●Made in China 2025 plan (MIC25) imeifanya China ishike nafasi ya kwanza duniani katika utengenezaji na uuzaji wa magari ya umeme (EVs)


Mwaka 2023 BYD iliizidi TESLA na kuwa kinara si tu katika uuzaji wa magari ya umeme bali pia teknolojia ya energy saving.




Ukiacha BYD China ina EVs auto manufacturers nyingine zinazofanya vizuri kama Chery, Nio, Li, SAIC, Geely, Xiaomi, Xpeng n.k



5. POWER EQUIPMENT TECHNOLOGY

(a)Photovoltaic na solar panel techs
●China account for over 80% of global solar panel market share.

The largest solar panel manufacturers in China include Tongwei Solar, JA Solar, Aiko Solar, and LONGi Solar, all of which are also the top global solar PV manufacturers.

In general, Chinese companies dominate the top 10 list for solar panel manufacturers
.

Installed solar power in China larger than the next 3 countrues combined




(b)Wind turbines
China ndio wazalishaji wakubwa duniani wa wind turbines na vifaa vyake on global market. Goldwind kampuni ya China is a world leader in wind turbine.

China controls EVERY major wind turbine supply chain segment:


Gearboxes (80%)


Generators (65%)


Blades (60%)





(c)EVs batteries
CATL ndiyo kampuni namba 1 duniani kwa utengenezaji wa battery za magari ya umeme inafuatiwa na BYD. Kwa ujumla 50% ya soko la EVs batteries limetawaliwa na hizi brands mbili za Kichina.




(d)Nuclear power technology
China imeweza kujenga nuclear power reactors kwa kutumia teknolojia iliyobuniwa na wanasayansi wa China iitwayo Hualong One technology badala ya kutegemea teknolojia kutoka nchi za Magharibi.


Kinu cha kuzalisha umeme wa nyuklia kinachotumia Hualong One tech, Southeast China's Fujian province.




6. ADVANCED RAIL TRANSPORTATION EQUIPMENT
🇨🇳 China high-speed rail lines
2000: 0 kilometers

2022: 42,000 kilometers




China imeanza kupata kandarasi za kujenga high speed railways nje ya China


The Jakarta-Bandung High Railway in Indonesia built by China's CRRC running with a top speed of 350km/hr


China built high speed rail btw Belgrade and Novi Sad in Serbia Eastern Europe with a top speed 200km/hr.



7. MEDICINE AND MEDICAL DEVICES
Kwa miaka mingi mashine za MRI na CT scan zimekuwa zikitengenezwa na makampuni ya nchi za Magharibi kama SIEMENS, GE na PHILIPS.

Hatimaye China kupitia mpango wake wa Made in China 2025 imewezesha kampuni ya Kichina ya Shanghai United Imaging Healthcare Co., Ltd. kuunda na kuanza mass production ya mashine hizo.



8. ROBOTICS


9. AGRICULTURAL MACHINERY EQUIPMENT
The government of China has been supporting the agricultural equipment manufacturing companies to a great extent. The central government provided 120 billion of subsidies to the industry. China’s agricultural machinery manufacturing industry mainly produced equipment used for the treatment of soil, fertilization, gardening, plant harvesting, crop farming, etc.

According to statistics, China has an annual output value of more than 500 billion US$.

The list of biggest manufacturers of agricultural machinery in China
1. YTO Group Corporation
2. Shandong Foton Heavy Industry International
3. Hubei Fotma Machinery Company
4. Weifang CP Machinery Company Limited
5.
Jiangsu Yueda Intelligent Agricultural Equipment Company





Ukweli utabaki kuwa China kupitia chama cha CPC is very skilled at making long-plans and achieving them accurately.

Lakini Marekani haikupendezwa na mpango wa Made in China 2025 ku-break dependence on foreign technologies.

Ndio maana vita vya kiuchumi na kiteknolojia dhidi ya China vilianza hasa 2018 Trump akiwa raisi wa Marekani na vinaendelea mpaka sasa chini ya Biden.

Afrika tuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa China on how to set plans and goals and achieve them.
 
Hongera sana kwa uchambuzi,I wako mzuri .. Tanzania ni Nchi isiyokuwa na maono haya tumekubali kuongozwa na wafu wenye uwezo mdogo na wasiojua Dunia inataka nini naisikitikia Tanzania Yangu uliojaa rushwa na isiona umuhimu wa kuwapa nguvu wananchi katika kukuza teknolojia na uzalishaji huku nchi ikiwa na rasilimali zote . Ila inaona umuhimu kuongeza masomo ya Dini
 
Unafikiri nini kifanyike ili Afrika hasa Tanzania tusogee kiteknolojia na uzalishaji?
 
Siku Watanzania tukiondokana na ujinga, ndio tuanze kufikiria kuyafanya haya mambo
Sio ujinga. Matter of fact, hakuna kitu kinachoitwa "general ignorance" ndani ya nchi. Sio Tanzania tu, bali kila sehemu duniani. Siku zote kutakuwepo na balance kwenye kila kitu, ikiwemo ujinga na akili. Ni maamuzi ya mtu mmoja kutambua na kuamua atumie upande gani.

China imefikia hii hatua sio sababu Nchi nzima ni Ma-genious. Sio kweli, bali mtu mmoja au kundi la watu wachache lenye maono na utambuzi, kuamua waende njia ipi kama Taifa. Na wote watafuata.

Ni kama ubongo ndani ya kichwa unavyoamua na kuongoza mwili ufanye nini. Na sio kwamba kila kiungo kinafanya kazi kinavyopenda, No. Bali maamuzi na uongozi wa ubongo ndio utadetermine fate ya mwili. Kama utakuwa wenye afya na balance au zombie huku kila kiungo kikienda kitakavyo.

Vivo hivyo kitaifa. Wananchi ni waongozwaji, wanahitaji kuongozwa na kuonyeshwa njia. Watakuwa wajinga au wenye akili hicho kiungo kikuu kikiamua.

Taifa linahitaji kiungo kimoja tu (Literally). Uongozi wenye maono na uwezo wa kutambua njia ipi Taifa lipite kufikia matokeo bora.

Kiuongo ambacho kwa sasa Tanzania hatuna.
 
Wana spirit flani ya kutokushindwa. Haijalishi wanapitia vikwazo gani, hua inawapa morali ya kufanya vizuri zaidi. Kuna documentary moja niliwahi kuiona kuhusu TBM zao.

Baada ya mataifa ya magharibi kuyazuia makampuni yao ku supply hizi machine kwa Wachina, serikali ilibidi i team up na vyuo vikuu vya teknolojia na makampuni ya ujenzi wakatengeneza TBM yao ya kwanza miaka ya 60 na ikaja kuwa tested miaka ya 70.

So hawa jamaa hawakubali kuwa wanyonge. Ukiwawekea vikwazo unawa boost kufanya vizuri zaidi.
 
Nini kifanyike kuondoa ujinga?
Pesa itolewe kwenye siasa ili watu waone kuwa mwanasiasa ni passion tu na siyo ajira. Watu wafanye kazi zenye kuleta tija katika jamii.
Siyo upuuzi inayofanywa na jamii yetu kwa sasa, mtu akitaka kufanya jambo lenye manufaa kwa nchi anaulizwa kama ana kadi ya chama au ni mwenzetu?
Tofauti na hapo tutaendelea kusikilizia tu maendeleo kwenye bomba.
 
China imefikia hii hatua sio sababu Nchi nzima ni Ma-genious. Sio kweli, bali mtu mmoja au kundi la watu wachache lenye maono na utambuzi, kuamua waende njia ipi kama Taifa. Na wote watafuata.
Hapo uliposema mtu mmoja au kundi la watu ukanikumbusha China

Kuna watu kama:
●Chairman Mao na
●Comrade Deng Xiaoping (Architect of Modern China)

Watakumbukwa sana kwa mapinduzi makubwa sana waliyofanya China

Na inapohusu kundi la watu China ipo hapo ilipofikia kwa sababu ya maono ya wanachama wa chama cha CPC na maraisi wa China kama akina Jiang Zemin, Hu Jintao na Xi Jinping
 
Akili nyingi hapa kwetu hao wasom kiutwa ila akili bado zipo kwny makalio hamna cha maana , msomi wa bongo ndoto yake kujua kingereza na kuajiriwa NGO's za kimataifa ila kufanya mapinduzi makubwa hamna kitu .

Eti leo hii mtu kaunganisha Satelitte kafany assembling basi ndio habari kubwa mjini , wanatucheka kweli ni utoto huo .
 
Watu wafanye kazi zenye kuleta tija katika jamii.
Umesema vyema

Mfano China mpaka uone mtu amekuwa raisi basi ujue CPC walimchunguza tangu grassroot yaani level ya chini kabisa ya uongozi alifanya vitu gani vya maendeleo

Ndio maana China kuna ushindani mkubwa wa viongozi wa provinces kuzinyanyua provinces zao kiuchumi, kiteknolojia, na GDP ili wapate nafasi za juu katika serikali

CV ya uongozi nchini China haiko kwenye makaratasi ila umefanya nini field.

Kwa mfano kwa Tanzania kiongozi mkuu au wa serikali kuu kama waziri aanze kuchunguzwa tangu akiwa kiongozi kwenye serikali ya kijiji alikiletea tija gani kijiji hicho
 
TUKITAKA TUFIKE SISI WA AFRIKA CHA KWANZA TUACHE KUZARAULIANA KILA JAMBO NA KUHESHIMU KILA MTAKACHO PEWA.
WACHINA WALIJIFANYA WAJINGA KWA UJIRA MDOGO HUKU WAKIJIFUNZA KWENYE VIWANDA VILIVYO WEKEZWA HAPO KWAO.

LEO HAPA MNAJAZA UJINGA WACCM ETI CCM CHIPUKIZI,UVCCM ,CHAWA WA KUSIFU UNATEGMEA HATA KIJIKO TANZANIA TUTAWEZA KUZALISHA
 
Sote tuliumbwa na Mungu . Tuliumbwa kwa sura na mfano wa Mungu . Mungu ni tajiri . Hivyo tuliumbwa ili tufanikiwe na tuwe matajiri . Kama Afrika hatujatajirika basi kuna kikwazo kimesimama njiani kutuzuia . Lakini mzungu na mwafrika wote wana macho mawili , wote wana masikio mawili na wote wana ubongo. .


Usalama wa Taifa uachane na ujinga wa kulinda wanasiasa uchwara wasio na maono . Nchi iache kuendekeza siasa . Uelekeo wa dunia ya sasa ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia . Pia nchi na raia kwanza katika kufanya mipango ya rasilimali za nchi ndio kipaumbele kwa mataifa yanayojielewa .

Nchi iandae majasusi wenye uwezo wa kuipeleka Tanzania kwenye mapinduzi ya kiteknolojia sio kumuwinda Tundu Lissu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…