Kwa sasa kiuhalisia njia pekee ya kukuza uchumi wa Taifa ni Technology. Taifa kama Taifa linahitaji kuadapt kasi ya ukuaji wa Technology duniani. Kuanzia kwenye Education, Transportation, Communication, Agriculture, Economics na Public Infrastructures in general.
Lakini utahitaji viable, straightforward executable plan itakayotufikisha huko.
Maana yake Serikali itatakiwa kuwekeza kwenye vijana wa sasa hivi wenye uchu na Technology na kuja na long term plan juu yao. (If mtu mwenye akili hiyo angekuwepo.)
Ningesema Serikali iwekeze vyuoni. Lakini sio kweli. Vyuoni kumejaa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wenye ndoto za kujikwamua kimaisha binafsi kwa kupata ajira TCRA ili apate kufaidi vizuri yeye na familia yake. To hell mwananchi wa chini.
Hivyo kuwekeza vyuoni ni idea ya kipuuzi ya kumwagia kuku mchele. Kila mtu atagombania ale kivyake. Pia utekelezajia wa hiyo plan utakuwa ni mgumu, sababu hautoweza kujua kina nani wana akili gani, mawazo gani na nia gani kitaifa. Ni mchanganyiko mkubwa wa watu wenye background tofauti na viwango tofauti vya fikra na utambuzi.
Na watu wanaotakiwa ni wachache sana.
Hivyo basi, solution ni kuja na sehemu maalumu zitakazo kutanisha aina ya watu wanaohitajika. Watu wenye akili zenye udadisi, fikra chanya na mawazo mapya ya kutatua changamoto za aina zote. Watu wenye curiosity watakao discuss, think na ku-tear apart problems, find their nature and solve them. Kutatua changamoto kuanzia kwenye Military, Weaponry, Medicine, Engineering, Energy, Economics, Agriculture, Public infrastructures, Robotics, Software, Hardware na mpaka changamoto za chini kabisa za mwananchi wa kawaida.
Technology Hubs au kiufupi TechHubs. Ni sehemu zitakazokutanisha watu wa aina hiyo. Unaweza sema ni equivalent na Silicon Valley ukienda Marekani. Watu wenye nia kweli na uchu wa udadisi, innovations na inventions watakutana hapo. Sababu hakutakuwa na malipo bali pure passion na hunger ya kuona Taifa lako na akili yako ikitumika ipasavyo na kukutana na watu mnaofanana mitazamo. That's where Technologically Advanced Countries Emerge.
Mataifa makubwa na yanayojitambua mambo haya huwa mandatory ili kutunishiana misuli nani ni mbabe, lakini hapa kwetu tufanye kwa nia ya kujikwamua wenyewe.
Nalipa kodi. Na ni haki yangu kushauri Taifa litumie vipi kodi yangu effectively for the betterment of the entire country and future generations.
Serikali itenge maeneo makubwa na kujenga majengo makubwa yatakayo kutanisha watu wa aina hii. Kila jengo na niche yake. Iwe Engineering, Military, Weaponry, Medicine, Robotics, Public Infrastructures nk Hizi niche zitakuwa zikishirikiana na ku-collaborate kutafuta solutions za mambo mbalimbali.
Na watu watakuwa wanakuja na Ideas, Problems za kila aina constantly na kutafuta solutions na experiments constantly. Na either Serikali au Private Investors wataamua kuwekeza kwenye ideas na solutions kama ni viable na zenye potential kubwa kitaifa. Na vilevile Serikali itakuwa inatoa maagizo na maombi ya solutions juu ya Matatizo, Changamoto mbalimbali au kwa Kiingereza Problems zitakazotakiwa kutafutiwa solutions ASAP au Gradually.
Nitaandika Thread ndefu kiundani kule jukwaa la Intelligence na Siasa tuone kama Nchi yetu ina mtu au watu niliowasema.