"Made in China 2025" Mpango wa China wa kujitegemea kiteknolojia wafikia asilimia 88

SEMA SIJUI WACHINA WANAKULIPA KIASI GANI CHA HII PROPAGANDA?
 
SEMA SIJUI WACHINA WANAKULIPA KIASI GANI CHA HII PROPAGANDA?badala ya propaganda. Ukifika china ukaona walichokifanya, na tukajilinganisha nao, pamoja na rasilimali tulizonazo,, tuna haki ya kujitukana sisi ni mabwege, wanyama au tusi lolote baya.

SEMA SIJUI WACHINA WANAKULIPA KIASI GANI CHA HII PROPAGANDA?
Hii sio propaganda ndiyo ukweli halisi. Bahati mbaya hatutaki kukosolewa au kujifunza. Tembelea China uone maendeleo yao.,, halafu tulijinganishe nao kwa rasilimali tulizonazo, tuna haki ya kujitukana sisi ni mabwege,, wanyama au tusi lolote baya. Na hiatatokea tuwafikie hata robo.
 
Hivi, viongozi wetu nao huaga wanasoma nyuzi kama hizi? Hawajisikiagi WIVU? Ni upumbavu kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa including ccm halafu hupeleki pesa kwa watafiti; vyuo kama UDSM, Muhimbili, Sokoine, Saint Joseph, Bugando, KCMC nk (nimetaja vyuo vya masomo ya Sayansi tu) vingekua ni vitalu vya kuipeleka nchi yetu mbele huko, wagunduzi nchi za Kiafrica wala huaga hawapewi kipaumbele, sijui nani alituloga sisi. Magufuli aliwahi kujaribu kuwapa heshima baadhi ya wagunduzi ila ndio akafa mapema. Miaka ya nyuma kuna watu walitengenezaga bunduki, mamlaka zikawafunga. PUMBAVU kabisa, ilishindikana nini wale kuwaendeleza ili penhine huko mbele na sisi tungewapata kina AK47 wetu? Unamfunga mtu aliyegundua kutengeneza bunduki halafu the same you kesho unakwenda kununua bunduki nje ya nchi, kuna kitu hakipo sawa kwenye ubongo wetu
 
The US is the world’s sole military superpower. It spends more on its military than the ten next highest spending countries combined. China is now the world’s sole manufacturing superpower. Its production exceeds that of the nine next largest manufacturers combined.
OECD TiVA database 2023
 
Wako kutunisha matumbo yao kwanza
 
🚄 China opened 2,300 km of new high-speed rail lines in 2024 alone. For comparison, Japan's total HSR system stands at 3000km.

🇨🇳 China's total High Speed Rail now stands at over 47,000km, over 2/3rds of the global total. It intends to reach 70,000 km of HSR by 2035.

 
Kufikia hii level ya Mchina, kama taifa hatuna budi kuufanyia mageuzi mfumo wetu wa elimu. Kama tulivyoweza kuanzisha sekondari za kata, sasa ni wakati wa kuanzisha technical schools zenye kutilia mkazo masomo ya sayansi pamoja na maabara za kisasa zaidi kwa wanafunzi kujifunzia kwa vitendo kile wakisomacho darasani. Hizi technical schools tulizoachiwa na wakoloni nyingi hazina utofauti na sekondari za kata kwani zinatumia mfumo uleule utumikao kwenye sekondari za kawaida.

Mkazo uwekwe kwenye masomo ya hesabu, fizikia, kemia, uandisi, ufundi, kilimo, kompyuta n.k. Vilevile ziajiri walimu kutoka kwenye mataifa yaliyoendelea. Kwa uanzishwaji wa shule hizi, naamini tutaweza kuzalisha watu ambao watakuwa wabunifu katika kulivusha taifa kwenye nyanja mbalimbali za kisayansi na kiteknolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…