Uchaguzi 2020 Madee adai marafiki wanamshawishi akagombee ubunge Kongwa na Dogo janja kugombea Arusha mjini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Madee amesema ingawa hajajiandaa kisaikolojia kugombea Ubunge lakini marafiki zake wanamshawishi agombee. Madee amesema yeye ameishi sana jimbo la Kongwa linaloongozwa na Ndugai.

Naye Dogo janja amesema yuko tayari kuwatumikia Wananchi na kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya katika miaka 5 ya mwanzo.

Chanzo: Clouds media.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii nchi inaenda kuwa ya kipumbavu sana yani watu wanavaa hereni, kufuga rasita na kuvaa suluari chini ya makario kama Dogo Janja, Hamornaze, Diamond Wawe Wabunge? huu sasa utoto.

Kuwatumikia wananchi sio lazima uwe maarufu au uwe na pesa au uwe masikini au uwe na elimu kinachotakiwa umeshafanya nini kwa jamii mpaka unataka kuwa mbunge?

Maisha yamekuwa magumu mnaenda kutafuta pesa za ubunge me nadhani kipimo cha mtu kupewa ubunge apimwe kwanza ameifanyia nini jamii kwa kipindi kabla ajaingia. Sio wakina Mwana Fa, Dogo Janja Au Madee Kutwa Kucha Wapo Dar Hata shida za Kongwa, Tanga Na Arusha hawazijuwi.
 
kweli Magu ni chuma cha pua kakaza vyuma vimekaza kwelikweli basi unaambiwa kwenye gemu kumelala doro mpunga umekata jamaa wote walizoea sifa na majigambo wanajificha wanakufa njaa mashabiki wanakufa njaa sasa kila wasanii wakitafuta upenyo hamna ila kwa mbaaaali wanamuona Sugu moto chini japo anajisifia kuvuta bangi hapo chini na best wake Profesa J japo ni wahuni ila wameula bungeni basi kila msanii na kila prodyuza bongo eti anataka jimbo hivi sasa mlikuwa wapi miaka yote mbona hamkugombea? hatuwatakiiiiii!!


 
CCM ndiyo inapenda wagombea na mibunge mijinga mijinga kama made, diamond, masterj na yule mmakonde
 
Mbona Sugu na Mzee Yusuph wameweza!
 
Hivi kugombea nafasi za uwakilishi kama majimboni zinataka umaarufu au elimu pia ni muhimu, discipline, na dedication... Sio kwasababu unajua kuimba tu bas
bongo fleva imeshawshinda hawa.
 
Ajiandae na kareti pia maana jimbo la kongwa ni balaa kuna mgombea mwaka 2015 alikutana na balaa la ngumi za Ndugai
 
Si waende tu. Kama kweli watapata kitu. Nawashauri waendelee kutafuta wanawake walio vizuri wa kuwalea. Siasa hawaziwezi
 
Mtoe Mwana Fa kwenye hiyo list unamkosea heshima...havai hereni...haimbi matusi..havai suruali chini ya makalio...ana exposure...amesoma ana masters.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…