Uchaguzi 2020 Madee adai marafiki wanamshawishi akagombee ubunge Kongwa na Dogo janja kugombea Arusha mjini

Bandiko kama hili likiwahusu sugu na jay litapendeza pia
 
Mwambie Madee na Dogo Janja kuna Ujumbe wao Kutoka kwa Dr Christopher Cyrilo:-


KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2020
013: Wasanii nendeni bungeni, wakati wenu ndio huu.
Kila mtanzania anayekidhi vigezo ana haki ya kuwakilisha wananchi kupitia ubunge, lakini si kila anayekidhi vigezo ana uwezo wa kufanya kazi za kibunge.

Si kila unapokuwa na haki ya...basi una uwezo wa...
Mwanaume asiye na nguvu za kiume kabisa ana haki ya kuwa na mke, lakini hawezi kuwa naye...
Uwezo wa kufanya kazi za kibunge ndio upi? Kwa sasa hakuna uwezo. Cha msingi ni kujua kusoma na kuandika, na vigezo vingine vyepesi tu.
Wasanii mnaojua kusoma na kuandika, huu ndio wakati wenu hasa. Mmekidhi vigezo.
Lakini si kila aliyekidhi vigezo ana uwezo wa kufanya kazi za kibunge. Hilo ni kweli.

Je! Kazi za kibunge ni zipi hizo; ambazo hata baadhi ya waliokidhi vigezo hawawezi kuzifanya?
Moja, kumpongeza na kumsifia Rais kila unapopewa nafasi na Spika.
Mbili, kumpongeza waziri anaposoma hotuba za wizara.
Tatu, kuwachamba na kuwazomea wabunge wa vyama vingine.
Nne, kugonga meza bila kujali kinachozungumzwa.
Tano, kuomba muongozo na kuzungumza utani.
Sita, kumshangilia mbunge wa chama chako anapotukana wabunge wa chama kingine
Saba, kupongeza Simba au Yanga kutegemea na ushabiki.
Ili uweze kuzifanya hizo kazi kwa ufasaha, enyi wasanii mnaotaka kuingia bungeni, nawashauri kugombea kupitia CCM. Ukiwa mbunge wa CCM, kazi hizo za kibunge zitakuwa rahisi zaidi kuliko kuwa wabunge wa vyama vingine.
Huu ndio wakati wenu.

MwanaFA, Harmonize, Shilole, Kala Jeremiah, Diamond, Steve Nyerere, na wengine.
Fanyeni sasa kazi za kuandika na kuimba nyimbo za kumsifu na kumpongeza Rais Magufuli ili siku ya kupitisha majina ya wagombea, awafikirie. Bila shaka, atatumia nguvu zake kuamuru majeshi na tume ili nyie mtangazwe kuwa washindi. Naamini atafanya hivyo kwa moyo wa dhati kabisa akiamini nyie mtamudu vema kazi za kibunge nilizotaja hapo juu.

Nendeni bungeni, muda wenu ndio huu.
Msisubiri nyakati ambazo, kazi za kibunge zitakuwa kuisimamia serikali ili ifanye kazi ya kutumikia wananchi. Msisubiri siku ambayo kazi za kibunge zitakuwa kuchambua na kujadili hoja nzito kwa maslahi ya Taifa. Msisubiri siku ambayo wabunge watatakiwa kuifokea na hata kuiwajibisha serikali inapokosea. Msisubiri siku ambayo bunge litahitaji watu mahiri wa kutunga sera, mahiri wa sheria, mahiri wa diplomasia, mahiri wa masuala ya kimataifa, mahiri wa masuala ya kijamii, mahiri mahiri mahiri...

Mkisubiri nyakati hizo ziwakute, hamtakwenda bungeni.
Nendeni bungeni wakati huu, ambapo serikali ndiyo inayosimamia bunge, huku wabunge wakishangilia kusimamiwa na serikali. Wakati ambao kiongozi wa bunge ni 'kijakazi' cha Rais. Wakati ambao wabunge wanatamani kuteuliwa uwaziri ili wawe sehemu ya serikali. Wakati ambao kumsifia Rais ni bora kuliko kuwasemea wananchi. Wakati ambao wabunge wanapitishwa na Rais, sio chama wala wananchi.
Huu ndio wakati wenu! Msisubiri.
 
Huyo Madee ajiandae kisaikolojia kweli kweli maana bwana Job huwa hataki mzaha kabisa.

Na anunue Helmet ili incase bwana Job kapandwa na mzuka basi madhara yasiwe makubwa.
 
Hivi kugombea nafasi za uwakilishi kama majimboni zinataka umaarufu au elimu pia ni muhimu, discipline, na dedication... Sio kwasababu unajua kuimba tu bas
Ndo upumbavu wanaowaza, nahisi huko mbeleni kila msanii atakuwa anagombea sababu tu anajua kushika maiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…