IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,839
Pasco, bajeti ikiidhinishwa na Bunge kinachofuata ni utekelezaji. Haipelekwi kwa CAG kupata idhini. Ikumbukwe kuwa hata CAG mwenyewe bajeti yake inaaidhinishwa na Bunge baada ya kuwa scrutinized na Kamati husika ya Kudumu ya Bunge. Entry point ya CAG ni baada ya matumizi kufanyika yaani mwishoni mwa mwaka wa fedha. CAG akikamilisha kazi yake anawasilisha Taarifa yake Bungeni na nakala moja anawasilisha kwa RAIS for information.
Nilitaka niweke sawa hili.
...Msingi wa malalamiko ya CAG ni kwamba ofisi yake imepata pesa kidogo sana zilizoizinishwa na bunge kiasi kwamba atashindwa kukagua ofisi za serikali ya kuwasilisha ripoti yake, ambayo lazima iwasilishwe binge lijalo la bajeti. Na akaenda mbali kusema ili asikwame kuwatuma maofisa wake kwenda mikoani ilibidi amueleze mukulu hali halisi.
Pili ametahadharisha kwamba wakati kuna Wizara zimepata below 50% ya bajeti iliyoidhinishwa na bunge kuna zingine zimepata more than 200% !!! na implication ya hii ni kwamba kuna Wizara pendwa zinapata more than kilichoidhinishwa na bunge, jambo ambalo ni hatarin kwani kama una watoto 5 na kwenye mgao wako wa pesa, ambao ni fixed, ukimzidishia mmoja maana yake mwingine atapunjika hivyo malengo yake hayatatimia.