Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Madeni ya Taifa: Kuna kitu very serious CAG amekisema. Hii kitu haiko sawa. Je, tunakwenda wapi?

Duh!
Za kuambiwa changanya na za kwako!
1. deni walikopa UPDP ? kwanini hatamti kufanya vulue for mopney tujue deni lilitumika wapi na watu wawajibishwe? au ndio wenzenu?

2. kuhsu shule nadhani ujitambui aliyekuambia elimu ni madawati nani kama thamani ya elimu haipo mtu unaweza kuunga unga na ukatusua kama bashite ? kwanini utuambia kuhus mikopo elimu ya juu(hivi muaahidi nini vile?)

3. Ndege inanihusu nini mkazi w akolomije? inaweza kunisaidia kusindika nyanya znagu? je inawezxa kunisaidia kupunguza bei ya sukari? bei ya mahindi, je wajua bei ya mchele ni sawa na unga kwa sasa?

4. hayo ya bagamoyo yamefanya na ACT au? kwanini hamuwajibishi waliofanya hayo?
Ninapojadili na mwana JF wa 2007, nategemea uwezo mkubwa wa mawazo na mtindo mzuri wa uandikaji. Lazima uwe umejifunza meengi ktk kipindi hicho hata kama ulijiunga baada ya kumaliza std 7. Sasa unapoandika kama kijana wa darasa la 4, unarudia na mambo ya kolomije kama mtumishi wa Mungu, nashindwa kuendelea na majadiliano.

Nimeshaona kwa nini hupati nafuu ktk kujenga hoja. hutaki au huwezi kujifunza.
 
Hata ukifuatilia na kuwa seriuos utafanya nini kwa katiba inayompa nguvu mkuu ya kuwa juu ya sheria ama kizite


Vyote kwa pamoja, kumbuka wabunge wote wana mikopo, na rais anajua kabisa wakiacha ubunge hawana ubavu wa kulipa hiyo mikopo. Hivyo anajua hakuna yoyote yuko tayari kukosa au kuingia kwenye hilo janga la kudhalilika kwa kushindwa kulipa mkopo. Tabia hiyo wanayofanyiwa wabunge imekuwa ni fimbo ya kuwachapia walio wengi, na hali hii inawakuta mpaka vyombo vya sheria na dola. Kwa mtindo huu ndio maana unaona mkulu anaweza kuwafanya lolote na wala asiwepo wa kuhoji labda wabunge wa upinzani. Sasa hivi wakuu wa mikoa na wilaya wana nguvu kuliko wabunge na wanaweza kufanya lolote na wala bunge lisifanye lolote.

mnafanya nini kwa makonda hivi sasa?
 
Ni jukumu lake kujiuzulu kupinga kama anaona kitu hakiendi sawa na namna zote za kusahihisha zimeshindikana. Nililisema hili mwaka jana.
Wewe babu unazeeka vibaya pamoja na kukaa huko USA. Wewe unataka aondoke ili teuzi zenu za kikabila zikave hiyo nafasi ili mfiche madudu yenu hajiuzulu mtu ng'o labda mumuanzishie zingwe kama mlivyofanya kwa Mramba wa TANESCO
 
Wewe babu unazeeka vibaya pamoja na kukaa huko USA. Wewe unataka aondoke ili teuzi zenu za kikabila zikave hiyo nafasi ili mfiche madudu yenu hajiuzulu mtu ng'o labda mumuanzishie zingwe kama mlivyofanya kwa Mramba wa TANESCO
Mkuu kumbe upo upande wetu, ila hujataka tu kujipambanua, hapa hatoki mtu labda Mtakatifu avunje matakwa ya kikatiba
 
Thursday, March 16, 2017
Ofisi ya CAG iwezeshwe itimize majukumu


pic+CAG.jpg

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Juma Assad

Kwa ufupi
  • Ilielezwa kuwa ufinyu huo, siyo tu ulikuwa unakwamisha maofisa wa ofisi hiyo kusafiri kwenda kutekeleza majukumu yao kisheria, bali pia kushindwa kuwasaidia wafanyakazi katika masuala ya afya, hususani wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).
By Mwananchi

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imelalamikia ukata. Mara ya kwanza ilikuwa Mei mwaka jana ilipolalamika kuwa ilikuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu kutokana na ufinyu wa bajeti.

Ilielezwa kuwa ufinyu huo, siyo tu ulikuwa unakwamisha maofisa wa ofisi hiyo kusafiri kwenda kutekeleza majukumu yao kisheria, bali pia kushindwa kuwasaidia wafanyakazi katika masuala ya afya, hususani wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Wabunge walisikia kilio hicho. Hivyo, wakati wa mjadala wa bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2016/ 17 walipigania ofisi hiyo, ambayo ni jicho la Serikali katika usimamizi wa matumizi bora ya rasilimali za umma, iongezewe fedha ili itekeleza majukumu yake, hasa ikizingatiwa kuwa mikoa, wilaya, mashirika na maeneo mengine ya ukaguzi yameongezeka.

Ofisi ya CAG ndiyo hukagua matumizi ya hesabu za Serikali Kuu (wizara ya idara zake), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (mikoa na wilaya zake), mashirika ya umma, wakala za Serikali na miradi ya maendeleo.

Mbali ya maeneo hayo ambayo yanafahamika, ofisi ya CAG pia huitwa kufanya ukaguzi maalumu mahali popote au ofisi yoyote ambayo inatiliwa shaka kuhusu matumizi ya fedha kama vile taasisi ya umma. Vilevile, ofisi ya CAG ndiyo hukagua matumizi ya fedha ya balozi zetu nchi za nje pamoja na ofisi za mashirika ya kimataifa yaliyoko chini ya Umoja wa Mataifa (UN) ambayo Tanzania iliingia mkataba kwa miaka sita kuanzia mwaka 2013.

CAG akifanya ukaguzi, kwanza hujiridhisha kama hayo ndiyo matumizi yaliyopangwa na pia hujiridhisha kuhusu thamani ya fedha katika miradi husika. Mwishoni mwa ukaguzi wake hutoa hati chafu au safi kulingana na namna alivyoona.

Lakini katika bajeti ya mwaka 2016/ 17 ilijitokeza hofu kwamba CAG asingeweza mwaka huu kufanya ukaguzi wa maana na ikiwa angefanikiwa asingefikia ofisi nyingi kama alivyokuwa akifanya miaka ya nyuma. Haikufahamika sababu ya kutengwa kiasi kidogo cha fedha kwa ofisi hiyo hasa ikizingatiwa bajeti ilikuwa ya Sh29.5 trilioni.

Katika kipindi hiki cha kuelekea kukamilisha mwaka wa fedha wa 2016/ 17 ofisi hiyo ya CAG imelalamika kwamba inashindwa kufanya kazi kufikia kiwango cha kitaifa na kimataifa, kama inavyotakiwa licha ya kuwa na watumishi wenye ari kwa sababu ya ufinyu wa fedha.

Pia, ofisi hiyo imesema inakabiliwa na madeni makubwa ya makandarasi ambao wanajenga majengo, likiwamo la Rukwa.

Waswahili wanasema kupanga ni kuchagua. Hatua yoyote ya kutoipa nguvu ofisi hii ambayo kwa miaka iliyopita ilisaidia kufichua uovu, wizi na ufisadi hadi Serikali ikachukua hatua dhidi ya maofisa au mikoa, itakuwa inachangia kurudisha nyuma juhudi zilizofikiwa.

Sote tunafahamu kwamba tangu CAG alipoanza kuwekwa hadharini ripoti ya ukaguzi wa hesabu mbalimbali, utunzaji mbovu wa hesabu umepungua, wizi na ubadhirifu umekwisha na ofisi nyingi zilizokaguliwa hupewa hati safi. Pia, imekuwa rahisi hata kugundua maeneo ambayo kuna kiwingu katika usimamizi wa miradi.

Tunaonya kadri ofisi hii itakavyokuwa inapunguziwa uwezo wake wa kukagua kutokana na kutengewa fedha kidogo ndivyo maofisa “wajanja” au wezi wa kutumia kalamu watakuwa wanarudi taratibu na kujiimarisha. Tunashauri ofisi hii iwezeshwe itimize majukumu yake.
 
SOCIALISM: You have two cows, and you give one to your neighbor.

COMMUNISM: You have two cows, the government takes both and gives you milk.

FASCISM: You have two cows, the government takes both and sells you milk.

NAZISM: You have two cows, the government takes them and kills you.

CAPITALISM: You have two cows, you sell one and buy a male. You multiply your cows and there is economic growth. You sell them, you retire and you live on your profits.

MODERN CAPITALISM: You have two cows, you sell one and buy a male. You multiply your cows and you buy those of your neighbors. The latter become your shepherds, you pay them in monkey currencies and they die poor.

AMERICAN SOCIETY: You have two cows, you sell one and you have to make the other one to produce milk like 4 cows. By dint of producing beyond her capacity, she dies. You take a consultant to understand this death.

FRENCH SOCIETY: You have two cows, you go on strike because you want a third.

GERMAN SOCIETY: You have two cows, you modify them so that they live 100 years, eat once a month and treat themselves.

CHINESE SOCIETY: You have two cows, you sell milk to your compatriots and you produce plastic milk to export to the rest of the world.

BLACK/ AFRICAN SOCIETY: You have two cows, you eat them all the same day and you dream that donors or the international community give you others. You go to a church or a mosque pray to Jesus or Allah for them to give you other cows. You fast 40 days and 40 nights without eating or drinking so that the cows will fall from Heaven. You recite "Hail Mary" a million times without success. You look for passages that speak of cows in the Bible or the Quran hoping to see the cows appear. At the end you have no strength to read the Bible or the Quran. You become a prophet of _the good news of the cows_ that will be coming soon. You die in extreme poverty

( *Many thanks to the unknown author* )
 
CAG katoa siri nzito sana,anasema hadi sasa kuna wizara imepata 16 %ya bajet yake Wakati huo huo wizara nyingine imepata 230 % ya fedha kulingana na bajet yake! Hii ni aibu na fedheha kubwa kwa wananchi na wabunge kwa ujumla! Je ndivyo walivyopanga na kupitisha bungeni? Mbona tuna wasomi jamaniii au ndo ile idadi ya vichaa inaongezeka nchini?tunaongozwa na machizi ? Hii ni aibu
 
Ninapojadili na mwana JF wa 2007, nategemea uwezo mkubwa wa mawazo na mtindo mzuri wa uandikaji. Lazima uwe umejifunza meengi ktk kipindi hicho hata kama ulijiunga baada ya kumaliza std 7. Sasa unapoandika kama kijana wa darasa la 4, unarudia na mambo ya kolomije kama mtumishi wa Mungu, nashindwa kuendelea na majadiliano.

Nimeshaona kwa nini hupati nafuu ktk kujenga hoja. hutaki au huwezi kujifunza.

Poel sana Binti!
wewe 2008 unahoja ipi?
Badala ya kujibu hoja unaanza kudiscuss mtu!
 
Back
Top Bottom