Madereva wa Formula 1, ni "Marubani" wa Jet za ardhini

Tukirudi kwenye issue ya kubadirisha tyre, kuna team ya watu zaidi ya 20 ambao wanabadirisha tyre zote nne kwa chini ya sekunde 3 kushuka chini.
View attachment 3004059
.
Ahahahah nimekipemda sana hiki kipande though hapo kwenye watu zaid ya 20 naona kama umekuza mambo chief.
Hapo nime observe;
Katika kila tyre kuna watu 3.
1. Aliyeshuka mashine ya kufungua tyre
2. Wa kuchomoa tyre
3. Wa kupachika tyre kisha yule aliye fungua ndiye anafunga tena kwa mashine.

So katika tyre 4 za gari hapo maana yale kuna watu 3x4= 12.

Halafu kingine nilicho observe hapo kuna watu wawil (2) kila ubavu wanaishikilia gari wakati zoezi la ubadilishaji wa tyres linaendelea.

So jumla ya watu hapo inakua kama 14 tu.

But all in all, uchambuzi mzuri, na haka ka kipengele kiukwel kamenifurahisha sanaa
 
Wewe ulio observer kuna wengine hawaonekani ni wale wanaoleta mataili kutoka ndani
 
Alafu nasikia katika hii ya F1 kuna mafuta yanatoa transparency flame.

Yani unakuta dereva anaungua ila nyie pembeni hamuoni moto mpaka anaanza kupiga kelele .

Zungumzia hii ipoje mkuu
Ooh nitacheki. Kwa nnavojua wanatumia unleaded gasoline sema ina high octanes. Na mwisho wa race kila team lazima ipeleke sample ya wese FIA wakacheki. Msije kua mmetumia mafuta mengine yakawasaidia kushinda.
 
Ooh nitacheki. Kwa nnavojua wanatumia unleaded gasoline sema ina high octanes. Na mwisho wa race kila team lazima ipeleke sample ya wese FIA wakacheki. Msije kua mmetumia mafuta mengine yakawasaidia kushinda.
Mbona nasikia wanasema katika kitu very secret ni hayo mafuta kila kampuni wana kua na additive zao special.

Maana ukiacha ufanisi wa dereva pia engine na mafuta ni kitu ambacho kinaangaliwa sana kama source win..

Au ipo vipi mkuu naomba kukosolewa hapa
 
Shukrani mkuu. Si unajua wengine wapo off-camera. 😂😂😂 Ila umetisha.

Hao jamaa wanalipwa vizuri kinoma. Waone ivo ivo. Wana mshahara na posho. Bado kuenjoy safari za nchi mbalimbali.

 
Hapana uko sahihi. Ni matairi tu katikati F1 ndio mnafanana ila ikija issues ya wese, engine, gari, etc kila team mnajijua kikubwa kuwe na limitations ambazo mnatakiwa mzifuate hapo ndio FIA anapokuja kukagua.

Kwahiyo ata wese haina maana kwamba wanaweka adharani majibu, ila FIA wanachukua sample wanacheki lab kisha wanajiridhia kwamba ipo ndani ya standards zetu.

FIA tuwaite kama TBS flani hivi.
 
Shukran mkuu
 
Mfano: Mercedes Benz nadhani wanatumia Petronas (sisi tunawaita Engen),

Redbull wanatumia Exxon Mobil. etc kwahiyo supplier wa mafuta ataweka "secret" additives kama ulivosema ila iwe ndani ya limitations za FIA
 
Huu mchezo napendaga kuuangalia ila sijuiagi vzr..hii mada imenifunza kdg...sasa nitaangalia kwa maelezo haya Mkuu..Ahsante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…