Dereva wa bus ya kampuni ya saul T 485 DXE wamshambulia abiria kisa kureport gari ikiwa na speed meter 115-120.
Kutokana na story ya muhusika anasimulia kua alikua na app ya kusoma speed ya ggari na kutuma kwenye group la wasafiri mojawapo.
Baada ya muhusika kurecord tukio hilo kwenye group alipokea DM za vitisho kutoka kwa namba tofauti.
Baadae kidogo alipgiwa simu na dereva wa gari ilo na kumtaka asogee mbele yani atoke siti iyo akakae mbele kwa dereva,alipofika dereva alimpokonya simu na kumtishia.
Baada ya safari kwenda kwa masaa kadhaa bila muhusika kupewa simu yake ilifika hatua abiria uyo alitaka kushuka sehem inayoitwa uyole wakati anataka kushuka walimzuia na kumtaka asishuke kwamba wanampeleka polisi kwa kosa la kurec na kuwachomea maovu yao.
Abiria alijitahidi kuwaomba na na kuwasisitiza lakini waligoma na kuondoka nae pasipo kumpeleka polisi.(utekaji huu)
Baada ya kufika mwisho wa safari walishusha abiria wote na kubaki wao madereva na baadhi ya watu wachache na kuanza kumhoji na kumpiga kwa kumlazimisha kusema nani amemtuma kurecord maovu ya kampuni yao ya SAUL na ilifikia hatua ya kumlazimisha amtaje moja ya mtu wa kampuni shindani ya New force.
Baada ya kipigo na vitisho vya muda mrefu walikagua simu na kujaribu kuweka namba za baadhi za watu waliohisi wao ndio wamemtuma ila walikuta abiria uyo hana namba za wahusika hao kabisa, ndipo walipomlazimisha kuformat simu yote na vitisho juu.
Baada ya muda walimuachia abiria huyo akiwa na majeraha maeneo ya mgongoni kutokana na kipigo walichomshushia.
Kutokana na taarifa iyo inaonesha ukanda huo Dar mpk Tunduma kumekuwa na ajali nyingi sana sababu ya rushwa na madereva kujiona tyr wameshika system.