broh... jaribu kuifanya hiyo kazi hata kwa siku mojatu... harafu uje na hili andiko lako...!
bolt wanachukua asilimia kubwa sana ni 24% ya nauli yoyote utakayo mlipa dereva.
ukimlipa dereva shilingi 1000/= bolt wanachukua shilingi 260/= ambayo ni sawa na hiyo asilimia 24%
ukifanya trip ya shilingi 9000/= bolt yakwao ni 2,160/= sasa elfu 9000-2160=6,840
hiyo 6840/= atakayo baki nayo dereva atoe pesa ya mafuta nadhani kwa Trip hiyo atatumia Nusu Lita ambayo ni sawa 1800 hivi ...
huku uliko mpeleke huyo dereva anaweza kweli asipate abiria akajikuta anarudi hadi starting point bila abilia.
alivyoenda alitumia nusu Lita ya petroleum kurudi pia ata tumia Nusu lita.
1650+1650=3300
tuchukue sasa ile asilimia 76 aliyobaki nayo dereva tuitoe na hayo mafuta aliyo tumia...!
6840-3300=3,540
dereva anabakiwa na 3540 pekee kwenye safari ambayo wewe ulipi toa pesa yako elfu 9000/= uliiona nyingi kuwa una mfaidisha dereva mwisho wa siku ni maumivu sana kwa huyo dereva.
2160/= wanayo ichukua bolt ni ya bure tu.
awatoi mafuta kwa dereva, awamnunulii hata vocha, chombo cha usafiri ni cha dereva mwenyewe amekipata kwa mbinu zake mwenyewe kwa mkopo au kwa mbinu yoyote.
mwisho wa siku dereva huyu akipata ajari ana baki yeye na ndugu zake... Bolt hawato msaidia chochote...! bila kujali wamechukua 24% kwenye kila trip ya huyu dereva....!
tubishane kwa hoja usiwatetee hayo makampuni ni wanyonyaji sana... bora hata UBER