Madereva wa kampuni za Usafiri Bolt na Uber wanaongoza kuharibu biashara ya usafiri

We jamaa mzinguaji sana, sasa kama bolt inamnyonga si atumie kampuni nyingine?
 
Matatizo uliyoandika, ambayo hata mimi nayakubali, hayahalalishi madereva kufanya mambo anayolalamikia mwanzisha thread. Zaidi haya ni matatizo ya wenye hizo APP na madereva. Kwa nini madereva wasipiganie haki zao kwa wenye APP na badala yake wazihamishie kwa abiria?
 
Nyie ndiyo watanzania ninao wajua mimi, wala haihitaji DNA.
Hao madereva hawakuyaona hayo makubaliano na hizi kampuni? Kwanini kama wanaumizwa wasipiganie stahiki yao badala kuwaibia raia?
 
Kwani dereva kulazimishwa atumie bolt au Uber sini aache hayo malalamiko mwambie hao wamiliki wabolt au Uber sasa mnawalalamikia abiria ili iweje .
 
haisaidii kitu mkuu... cha msingi kuwe tu na maelewano... hayo mambo ya kukomeshana hayatotufikisha popote...!

lakini siwezi kuwatetea....! kuna baadhi ya madereva wana kera sana kwakweli...!​
dereva ukimwambia unamripot anakua na adabu kinyama naongea kwa uzoefu mkuu unafikili kwanin wanaombaga sana uwa rate 5 stars
 
Unasema bolt wanachukua 24% halafu hawafanyi kazi yoyote akili yako ndogo sana.... kaa kijiweni usubiri abiria uone moto wake.
 
wewe umepata wateja kwa sababu ya kutumia nembo yao, unatarajia utumie kibure bure? Kumbuka na wao wanalipa kodi na wanao wafanyakazi vile vile. Mimi naona mtu akiona hakuna maslahi basi aendelee kivyake vyake tu lakini asiharibu jina la kampuni ya watu.
Na pindi kampuni itakapoona haipati faida itajiondoa yenyewe.
 
Nikweli mkuu
 
Kwanini usiachane nao ufanye kazi ya Taxi kuliko huo mzigo kumwangushia mteja ambaye hahusiki.
Ki ukweli hakuna tabia inakera kama unachukua bolt halafu mtu ana cancel ionekane umelipa 1000 wakati umelipa 10,000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…