Madereva wa mabasi ya abiria Tanzania hawana akili ya kuendesha usiku,tutakwisha

Nimecheka kwa kweli. Iko hivi, majuzi tumetoka mwanza - Mbeya na kampuni ya Mbeya express. Kufika dodoma stendi Mkuu trafiki kazuia Basi letu kuendelea na safari Kisa tairi mbili za nyuma ni kipara. Abiria tukahamaki kucheleweshwa lakini trafiki alishikilia msimamo wake.
Dereva na konda wakaomba ibadilishwe tairi moja then nyingine wangebadilisha pindi wakifika Mbeya.....wakakubaliwa japo trafiki yule akatoa tahadhali kwa abiria waliokuwa wanamlalamikia kwa kucheleweshewa safari.
Trafiki yule akasema hivi"hii tairi hamtafika nayo...."
Kweli bwana tulipovuka tu bwawa la mtera ngoma ikapasuka kwa kishindo cha kutisha japo haikuwa na madhara lakini nlimkumbuka yule trafiki.

Kuna muda lawama tunawatupia polisi lakini hata sisi abiria ni vimeo
 
Hata kama mchana ajali zipo naogopa sana safari za usiku
 
Sure,. Huwa hatujijali tukiwa wazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…