The atlantic
JF-Expert Member
- Aug 1, 2023
- 390
- 670
Nimecheka kwa kweli. Iko hivi, majuzi tumetoka mwanza - Mbeya na kampuni ya Mbeya express. Kufika dodoma stendi Mkuu trafiki kazuia Basi letu kuendelea na safari Kisa tairi mbili za nyuma ni kipara. Abiria tukahamaki kucheleweshwa lakini trafiki alishikilia msimamo wake.Kati ya yote haya ni nchi Gani madereva wao wanakosa hata Moja,,!???
Note! Sheria kutokufuatwa, uwajibikaji mbovu wa trafic police na miundombinu mibovu + ujinga wa abilia ndio sababu ya ajali na vifo,,dereva anatenga elfu hamsini dar to mwanza ili aende speed ya 120 road , trafic wote wanakula elfu tanotano, wakiingia ndani ya basi utasikia vipi mwendo, abilia sasa walivo mazuzu utasikia kwa kweli ni mzuri baba!!subiri wapate ajali Sasa, utasikia Ile mwendo nilijua tu tutaanguka,. !!!!
Dereva na konda wakaomba ibadilishwe tairi moja then nyingine wangebadilisha pindi wakifika Mbeya.....wakakubaliwa japo trafiki yule akatoa tahadhali kwa abiria waliokuwa wanamlalamikia kwa kucheleweshewa safari.
Trafiki yule akasema hivi"hii tairi hamtafika nayo...."
Kweli bwana tulipovuka tu bwawa la mtera ngoma ikapasuka kwa kishindo cha kutisha japo haikuwa na madhara lakini nlimkumbuka yule trafiki.
Kuna muda lawama tunawatupia polisi lakini hata sisi abiria ni vimeo