Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Safari ya basi, ni utalii pia, Abiria wafurahie safari yao, Siyo kupelepelekwa mputa mputa.
 
Zamani kuna njia ya Mtera pale bwawani magengeni,ile njia sidhani km kuna hotel maalum bus lisimame.
Bus ngoma ikizimishwa ipoe kuna magenge pale unakuta mpunga Samaki km wote maharage,kabichi ,mchicha ndo vinaipuliwa.
Mnakula kwa pozi hadi gari ipoze engine mshashiba.
Safari inaanza tena
 
Madereva na wahudumunwao wanakula free chochote wanataka.
 
πŸ˜€πŸ˜€, Njia ya mtera Bado hakuna hotel mkuu, ila kuna kituo, basi huwa zinasimama, mama ntilie wanapika wali, pilau, samaki wakukausha, Ni maeneo rafiki sana.
 
hili ndilo tatizo kubwa la Tanzania hakuna mtanzana ana upendo na mwenzake na ukiwepo ni wa kinafk au kimaslay! kama wewe unacho usimkebei asiye nacho!
Sasa chukulia huyo ndo amepata kuongoza mamlaka fulani 😟,, Wananchi watateseka milele.
 
Madereva na wahudumunwao wanakula free chochote wanataka.
Hata kama mkuu, kile kitu haifai kabisa, Madereva anaweza kula popote pale au akapewa posho zuri kabisa Kulingana na sehemu aliyo paki basi,
 
Madereva sio wa kulaumiwa kwasababu nao hufuata tu maelekezo sio maamuzi yao. Ila watanzania tuna upumbavu wa kupoteza sana muda. Safari ya masaa 8 huwa inafika zaidi ya masaa 10 kwa sababu ya huu ujinga wa kusimama muda mrefu kula. Ingekuwa amri yangu gari zingekuwa zinasimama stendi tu kushusha na kupakia... yaani safari ni mchakamchaka. Kusema washushe bei ni ngumu sana kwasababu hao wanategemea abiria tu kwenda kula kwahiyo wakishusha wanaweza kutomudu gharama za uendeshaji.
 
Ingekuwa amri yangu gari zingekuwa zinasimama stendi tu kushusha na kupakia, yaani safari ni mchakamchaka
Mkuu safari siyo ubabe, safari ni utalii, safari iwe yenye amani, safari iwe salama ili kuhakikisha abiria wote wanafika salama sehemu husika.

Kusema washushe bei ni ngumu sana kwasababu hao wanategemea abiria tu kwenda kula kwahiyo wakishusha wanaweza kutomudu gharama za uendeshaji.
Yaweza kuwa upo sahihi au la! Kuuza sahani ya wali 5000, 7000, 8000 unaona sahihi,? Labda chakula ingekuwa cha maana kidogo kuhusu ubora, lakini ukiangalia chakula ni cha hovyo kupita kiasi,
 
πŸ˜€πŸ˜€, Njia ya mtera Bado hakuna hotel mkuu, ila kuna kituo, basi huwa zinasimama, mama ntilie wanapika wali, pilau, samaki wakukausha, Ni maeneo rafiki sana.
Kaka umepita lini njia hiyo. Pale Mlowa kuna jamaa wamejenga hotel nzuri tu za bei za kuruka
 
Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
Muongo wewe hakuna mahali wanauza vyakula au hasa hayo maziwa yaliyolala kama kwenye hizo hotel za Mabasi.
Sikia...kuna siku nilikunywa Maziwa sehemu flani njia ya Singida huko,ila kabla sjamaliza nikagundua yanamushkeli nikauchubua,sema nilikuwa nshachukua namba ya huyo mdada ili nimtongoze,Baada ya Muda tushafahamiana yule demu alinambia huko uwa hawamwagi kitu labda kiwe kimeharibika sana.
 
Umeshawahi fikiria gharama za uendeshaji wa hizo hoteli? Pale wanakula abiria tu. Hakuna mwananchi wa maeneo yake atathubutu kwenda kula pale. Vinginevyo stendi za mabasi ziwe na migahawa inayoweza kutoa huduma bora. Stendi zikiweza kuwa na hoteli kama 3 zitafanya kuwe na ushindani na walaji kunufaika. Kinyume na hapo kilio kitaendelea.
 
Umeshawahi fikiria gharama za uendeshaji wa hizo hoteli?
Swali fikirishi πŸ€”,


Hakuna mwananchi wa maeneo yake atathubutu kwenda kula pale
Kwa nini watu wa kawaida hawaendi kula hayo maeneo ?

Vinginevyo stendi za mabasi ziwe na migahawa inayoweza kutoa huduma bora
Hii ilikuwa inafanyika tangu mwanzo, lakini mamlaka ziliwatimua kufanya biashara ya migahawa maeneo ya stendi.( uongozi wa hovyo)

Stendi zikiweza kuwa na hoteli kama 3 zitafanya kuwe na ushindani na walaji kunufaika.
Hii jibu ni zuri, tatizo wanaojenga hotel wanawekeza mbali na stendi, kwa sababu wanajua kabisa biashara yao ni ya kiwango cha chini hivo abiria hawatanunua chakula kwenye hotel zao,
 
Halafu kuna tatizo lingine, kwamba...

Mkishakaribia hotelini, wanatangaza kwamba muda wa kuchimba dawa na chakula ni dakika 10. Kumbuka kwamba kwa msongamano wa kwenye bus, wale wanaokaa siti za katikati au nyuma, hadi wafanikiwe kushuka unakuta wameshatumia dk 5 tayari.

Technically, hadi wakachimbe dawa na wanunue chakula basi wanakuwa wameshatumia dakika zaidi ya 10, this is very unfair.

Inabidi wajirekebishe kwenye hilo swala la muda pia, kwa kuwazingatia back benchers.
 
 
Ulikuwa ni uamuzi wa hovyo sana. Na sio stendi tu hata pale Airport vitu ghali sana mgahawani. Yaani chakula ni bei rahisi ukiwa Dubai Airport kuliko JK Nyerere airport Dar.
πŸ˜€πŸ˜€, Kauli ya wazee, Waafrika watauana wao kwa wao, kwa sababu ya ukosefu wa maarifa.
 


Kumbuka kwamba kwa msongamano wa kwenye bus, wale wanaokaa siti za katikati au nyuma, hadi wafanikiwe kushuka unakuta wameshatumia dk 5 tayari.
Hii inatokea sana tu, Abiria wengi wanaagiza chakula(supu) kwa sababu ya uchache wa mda inawabidi kuacha supu, ili asiachwe na Basi, .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…