Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Dah niliudhika sana Ally's kutoka Dar-kwenda Mwanza...badala ya kupaki dodoma mjini kwenye hotel/migahawa mizuri .wameenda kulipaki basi karibu na bahi...vyakula vimepoa na vibaya kinoma.

Ok kutoka hapo ineenda kusimama tena nje ya mji wa Singida..chakula kibaya na bei kubwa vile vile..
 
Mkuu ndio maana kuna mikate na soda/juice za kopo. Kama ukigundua madreva wanapaki basi sehemu za gharama ya juu dawa ni kusafiri na mikate, viazi au mabumunda uwe unakula njiani taratibu bila shuruti mkuu.
Daah mabumunda mkuu umenikumbusha mbali sana ukiyapatia na Avocado na chai ya rangi unaweza ukatikisa free mchana ujue...
 
Ukifanya uchunguzi utagundua pia kwamba Madereva wenyewe hawali kwenye hotel hizo huwa wanalipwa hela tu , wao wanakula sehemu maalum , wana wapishi maalum humo njiani huwaletea msosi kwenye maeneo wanayoahidiana
Hii itakua kweli mkuu, Maana akisha simamisha basi tu, humuoni tena, zaidi ya konda. Mara ya kwanza nilikua nahisi labda kuna vyumba special wanakaa.
 
Hii serikali haijali wananchi hata kidogo, ni wizi kama wizi mwingine kuuza sahani ya chakula, wali boko boko 8000
Ulitaka serikali ipange bei ya chakula?Halafu mpige kelele tena kwamba ni ya kidikteta?Supply and demand ndio inaamua bei ya bidhaa.Uchumi wa kupangiana bei sio mzuri.Bei ni mapatano ya muuzaji na muuziwa.Ukiona haikufai acha.Muuzaji atateremsha bei kwa sababu ya demand ndogo.
 
Kutoka mwanza had dar wanakula nala pale Dodoma chai tu ya 200 inauzwa pale buku, chapati za mia tatu, pale buku

Serikali ilitizame hili suala vizur makampun yana waumiza wateja wao
 
kula nyama ya punda, paja la kunguru ni kawaida
Sawa kabisa siku tulipita chalinze pale kulia tukaona tukale kidogo maana tulitoka mtwara.
Aisee naagiza kuku kienyeji chips likaletwa bonge la paja.
Mmh kula kidogo likanishinda ladha.
Nikaja kuambiwa badae ni yale mandege Tai yana miguu mirefu hivi ndo nimeuziwa.
 
Hya malalamiko huwa yanaletwa hapa mara kwa mara. Tatizo watanzania ni manyumbu yanapenda kulalamika bila kuchukuwa hatua. Tungekuwa tunakomaa wakati wa uchaguzi kulinda kura hawa watawala wasingetuchezea namna hii.
 
Hizi ni story za vijiweni. Hivi wewe unadhani kuna mtu mwenye uwezo wa kukamata ndege wengi mpaka afikie hatua ya kuuza nyama yao? Au humjui tai wewe? Wanapatikana kwa wingi kiasi hicho?
 
Hao ni majambazi,Dom mngekula poa tu,Manyoni hamkosi msosi uhakika pale,Singida town popote mikuku ,nyama iko bwerere.
 
Beba chakula chako kutoka kwenu,
Mabasi hayawezi kupeleka watu kwa mama ntile kusiko hata na vyoo vya kujisaidia abiria.
Mbona zamani mabasi yalikuwa yanasimama stendi na stendi kulikuwa na hotel nzuri na zenye vyakula vizuri? Kwanza kulikuwa hakuna mama ntilie wa kuuzia wasafiri vyakula. Serikali leo ikiamuru magari kusimama stendi, nakuhakikishia watu wataweka hoteli nzuri sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…